Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   GENERAL_PUNCTUATION    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23233  MAT 1:20  Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
23234  MAT 1:21  Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.
23236  MAT 1:23  Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa Emanueli (maana yake, Mungu yu pamoja nasi).
23240  MAT 2:2  wakauliza, Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.
23242  MAT 2:4  Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria, akawauliza, Kristo atazaliwa wapi?
23243  MAT 2:5  Nao wakamjibu, Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:
23244  MAT 2:6  Ewe Bethlehemu katika nchi ya Yuda, kwa vyovyote wewe si mdogo kabisa kati ya viongozi wa Yuda; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu, Israeli.
23246  MAT 2:8  Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu.
23251  MAT 2:13  Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode anakusudia kumwua huyu mtoto.
23253  MAT 2:15  Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.
23256  MAT 2:18  Sauti imesikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.
23258  MAT 2:20  akamwambia, Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.
23261  MAT 2:23  akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: Ataitwa Mnazare.
23263  MAT 3:2  Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.
23264  MAT 3:3  Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake.
23268  MAT 3:7  Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
23273  MAT 3:12  Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.
23275  MAT 3:14  Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.
23276  MAT 3:15  Lakini Yesu akamjibu, Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka. Hapo Yohane akakubali.
23278  MAT 3:17  Sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye.
23281  MAT 4:3  Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.
23282  MAT 4:4  Yesu akamjibu, Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.
23284  MAT 4:6  akamwambia, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.
23285  MAT 4:7  Yesu akamwambia, Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako.
23287  MAT 4:9  akamwambia, Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu.
23288  MAT 4:10  Hapo, Yesu akamwambia, Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.
23293  MAT 4:15  Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
23294  MAT 4:16  Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!
23295  MAT 4:17  Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!
23297  MAT 4:19  Basi, akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu.
23306  MAT 5:3  Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
23314  MAT 5:11  Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
23316  MAT 5:13  Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
23317  MAT 5:14  Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
23319  MAT 5:16  Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
23320  MAT 5:17  Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
23324  MAT 5:21  Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
23328  MAT 5:25  Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
23330  MAT 5:27  Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
23334  MAT 5:31  Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
23336  MAT 5:33  Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
23341  MAT 5:38  Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
23346  MAT 5:43  Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
23352  MAT 6:1  Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.
23353  MAT 6:2  Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23356  MAT 6:5  Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23358  MAT 6:7  Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
23365  MAT 6:14  Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia.
23367  MAT 6:16  Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23370  MAT 6:19  Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
23373  MAT 6:22  Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga.
23375  MAT 6:24  Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
23376  MAT 6:25  Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
23379  MAT 6:28  Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
23382  MAT 6:31  Basi, msiwe na wasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!
23386  MAT 7:1  Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
23391  MAT 7:6  Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua ninyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.
23392  MAT 7:7  Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
23397  MAT 7:12  Watendeeni wengine yale mnayotaka wao wawatendee ninyi. Hii ndiyo maana ya Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.
23398  MAT 7:13  Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi.
23400  MAT 7:15  Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
23406  MAT 7:21  Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
23409  MAT 7:24  Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
23411  MAT 7:26  Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
23412  MAT 7:27  Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena kwa kishindo kikubwa.
23416  MAT 8:2  Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!
23417  MAT 8:3  Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, Nataka! Takasika. Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
23418  MAT 8:4  Kisha Yesu akamwambia, Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.
23420  MAT 8:6  akisema, Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana.
23421  MAT 8:7  Yesu akamwambia, Nitakuja kumponya.
23422  MAT 8:8  Huyo ofisa akamwambia, Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
23423  MAT 8:9  Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda! naye huenda; na mwingine, Njoo! naye huja; na mtumishi wangu, Fanya kitu hiki! naye hufanya.
23424  MAT 8:10  Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii.
23426  MAT 8:12  Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno.
23427  MAT 8:13  Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini. Na mtumishi wake akapona saa ileile.
23431  MAT 8:17  Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu.
23433  MAT 8:19  Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako.
23434  MAT 8:20  Yesu akamjibu, Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.
23435  MAT 8:21  Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu.
23436  MAT 8:22  Lakini Yesu akamwambia, Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao.
23439  MAT 8:25  Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia!
23440  MAT 8:26  Yesu akawaambia, Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa? Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.
23441  MAT 8:27  Watu wakashangaa, wakasema, Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!
23443  MAT 8:29  Nao wakaanza kupiga kelele, Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?
23445  MAT 8:31  Basi, hao pepo wakamsihi, Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale.
23446  MAT 8:32  Yesu akawaambia, Haya, nendeni. Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.
23450  MAT 9:2  Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.
23451  MAT 9:3  Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, Mtu huyu anamkufuru Mungu!
23452  MAT 9:4  Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
23454  MAT 9:6  Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani. Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.
23457  MAT 9:9  Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, Nifuate. Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
23459  MAT 9:11  Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
23460  MAT 9:12  Yesu aliwasikia, akasema, Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.
23461  MAT 9:13  Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.
23462  MAT 9:14  Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?
23463  MAT 9:15  Yesu akawajibu, Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
23464  MAT 9:16  Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
23465  MAT 9:17  Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.
23466  MAT 9:18  Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi.
23469  MAT 9:21  Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: Nikigusa tu vazi lake, nitapona.
23470  MAT 9:22  Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya. Mama huyo akapona saa ileile.
23472  MAT 9:24  akasema, Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu. Nao wakamcheka.
23475  MAT 9:27  Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, Mwana wa Daudi, utuhurumie!
23476  MAT 9:28  Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo? Nao wakamjibu, Naam, Mheshimiwa.
23477  MAT 9:29  Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, Na iwe kwenu kama mnavyoamini.
23478  MAT 9:30  Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: Msimwambie mtu yeyote jambo hili.
23481  MAT 9:33  Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!
23482  MAT 9:34  Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya.
23485  MAT 9:37  Hapo akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache.
23486  MAT 9:38  Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
23491  MAT 10:5  Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.
23497  MAT 10:11  Mkiingia katika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtu yeyote aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeni naye mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
23502  MAT 10:16  Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
23507  MAT 10:21  Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe, nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
23509  MAT 10:23  Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.
23510  MAT 10:24  Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.
23512  MAT 10:26  Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na kila kilichofichwa kitafichuliwa.
23518  MAT 10:32  Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
23520  MAT 10:34  Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
23523  MAT 10:37  Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
23526  MAT 10:40  Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
23528  MAT 10:42  Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwe kupata tuzo lake.
23531  MAT 11:3  wamwulize: Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?
23532  MAT 11:4  Yesu akawajibu, Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona:
23534  MAT 11:6  Heri mtu yule asiyekuwa na mashaka nami.
23535  MAT 11:7  Basi, hao wajumbe wa Yohane walipokuwa wanakwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu habari za Yohane: Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
23538  MAT 11:10  Huyu ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: Tazama, hapa namtuma mjumbe wangu, asema Bwana, akutangulie na kukutayarishia njia yako.
23544  MAT 11:16  Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja kwa kingine:
23547  MAT 11:19  Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: Mtazameni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wahalifu! Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.
23549  MAT 11:21  Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia na kujipaka majivu zamani, ili kuonyesha kwamba wametubu.
23552  MAT 11:24  Lakini nawaambieni, Siku ya hukumu itakuwa nafuu zaidi kwa watu wa Sodoma, kuliko kwako wewe.
23553  MAT 11:25  Wakati huo Yesu alisema, Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima mambo haya, ukawafumbulia watoto wadogo.
23555  MAT 11:27  Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumjulisha.
23558  MAT 11:30  Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
23560  MAT 12:2  Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato.
23561  MAT 12:3  Yesu akawajibu, Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa?
23566  MAT 12:8  Maana Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato.
23568  MAT 12:10  Kulikuwa na mtu mmoja mwenye mkono uliopooza. Basi, watu wakamwuliza Yesu, Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato? Walimwuliza hivyo wapate kisa cha kumshtaki.
23569  MAT 12:11  Lakini Yesu akawaambia, Tuseme mmoja wenu ana kondoo wake ambaye ametumbukia shimoni; je, hatamshika na kumtoa humo siku ya Sabato?
23570  MAT 12:12  Mtu ana thamani kuliko kondoo! Basi, ni halali kutenda mema siku ya Sabato.
23571  MAT 12:13  Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha, nao ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.
23576  MAT 12:18  Hapa ni mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka Roho yangu juu yake, naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.
23579  MAT 12:21  Katika jina lake mataifa yatakuwa na tumaini.
23581  MAT 12:23  Umati wote wa watu ulishangaa ukasema, Je, huenda ikawa huyu ndiye Mwana wa Daudi?
23582  MAT 12:24  Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, wakasema, Mtu huyu anawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo.
23583  MAT 12:25  Yesu, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, Ufalme wowote uliogawanyika makundimakundi yanayopingana, hauwezi kudumu, na mji wowote au jamaa yoyote iliyogawanyika makundimakundi yanayopingana, itaanguka.
23587  MAT 12:29  Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake.
23588  MAT 12:30  Yeyote asiyejiunga nami, anapingana nami; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
23591  MAT 12:33  Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mema; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
23594  MAT 12:36  Basi, nawaambieni, Siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema.
23595  MAT 12:37  Maana kwa maneno yako, utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako, utahukumiwa kuwa na hatia.
23596  MAT 12:38  Kisha baadhi ya walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamwambia Yesu, Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.
23597  MAT 12:39  Naye akawajibu, Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara; hamtapewa ishara nyingine, ila tu ile ishara ya nabii Yona.
23601  MAT 12:43  Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzika asipate.
23603  MAT 12:45  huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.
23605  MAT 12:47  Basi, mtu mmoja akamwambia, Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kusema nawe.
23606  MAT 12:48  Lakini Yesu akamjibu mtu huyo, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni kina nani?
23607  MAT 12:49  Kisha akaunyosha mkono wake kuelekea wanafunzi wake, akasema, Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu!
23608  MAT 12:50  Maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu.
23611  MAT 13:3  naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
23617  MAT 13:9  Mwenye masikio na asikie!
23618  MAT 13:10  Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, Kwa nini unasema na watu kwa mifano?
23619  MAT 13:11  Yesu akawajibu, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
23624  MAT 13:16  Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
23626  MAT 13:18  Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
23631  MAT 13:23  Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini.
23632  MAT 13:24  Yesu akawaambia watu mfano mwingine: Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
23638  MAT 13:30  Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.
23639  MAT 13:31  Yesu akawaambia watu mfano mwingine: Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake.
23640  MAT 13:32  Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.
23641  MAT 13:33  Yesu akawaambia mfano mwingine: Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka.
23643  MAT 13:35  ili jambo lililonenwa na nabii litimie: Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.
23644  MAT 13:36  Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani.
23645  MAT 13:37  Yesu akawaambia, Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
23652  MAT 13:44  Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
23653  MAT 13:45  Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
23655  MAT 13:47  Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
23658  MAT 13:50  na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno.
23659  MAT 13:51  Yesu akawauliza, Je, mmeelewa mambo haya yote? Wakamjibu, Naam.
23660  MAT 13:52  Naye akawaambia, Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.
23662  MAT 13:54  akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
23664  MAT 13:56  Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?
23665  MAT 13:57  Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!
23668  MAT 14:2  Basi, akawaambia watumishi wake, Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake.
23670  MAT 14:4  kwamba alikuwa amemwambia Herode, Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!
23674  MAT 14:8  Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji.
23681  MAT 14:15  Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.
23682  MAT 14:16  Yesu akawaambia, Si lazima waende, wapeni ninyi chakula.
23683  MAT 14:17  Lakini wao wakamwambia, Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.
23684  MAT 14:18  Yesu akawaambia, Nileteeni hapa.
23692  MAT 14:26  Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, Ni mzimu! Wakapiga kelele kwa hofu.
23693  MAT 14:27  Mara, Yesu akasema nao, Tulieni, ni mimi. Msiogope!
23694  MAT 14:28  Petro akamwambia, Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako.
23695  MAT 14:29  Yesu akasema, Haya, njoo. Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
23696  MAT 14:30  Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, Bwana, niokoe!
23697  MAT 14:31  Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?
23699  MAT 14:33  Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.
23704  MAT 15:2  Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!
23705  MAT 15:3  Yesu akawajibu, Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?
23711  MAT 15:9  Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.