23214 | MAT 1:1 | Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake: |
23225 | MAT 1:12 | Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaa Zerobabeli, |
23231 | MAT 1:18 | Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. |
23235 | MAT 1:22 | Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: |
23243 | MAT 2:5 | Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika: |
23249 | MAT 2:11 | Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane. |
23253 | MAT 2:15 | Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.” |
23255 | MAT 2:17 | Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia: |
23261 | MAT 2:23 | akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” |
23262 | MAT 3:1 | Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: |
23264 | MAT 3:3 | Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake.” |
23282 | MAT 4:4 | Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.” |
23284 | MAT 4:6 | akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.” |
23285 | MAT 4:7 | Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako.” |
23288 | MAT 4:10 | Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.” |
23292 | MAT 4:14 | Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya: |
23299 | MAT 4:21 | Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita, |
23302 | MAT 4:24 | Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote. |
23305 | MAT 5:2 | naye akaanza kuwafundisha: |
23324 | MAT 5:21 | “Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe. |
23325 | MAT 5:22 | Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu. |
23330 | MAT 5:27 | “Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini! |
23334 | MAT 5:31 | “Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka. |
23336 | MAT 5:33 | “Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana. |
23341 | MAT 5:38 | “Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino. |
23346 | MAT 5:43 | “Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako. |
23360 | MAT 6:9 | Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe. |
23377 | MAT 6:26 | Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao? |
23382 | MAT 6:31 | “Basi, msiwe na wasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini! |
23396 | MAT 7:11 | Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba. |
23407 | MAT 7:22 | Wengi wataniambia Siku ile ya hukumu: Bwana, Bwana! kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi. |
23408 | MAT 7:23 | Hapo nitawaambia: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu. |
23431 | MAT 8:17 | Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu.” |
23453 | MAT 9:5 | Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Simama, utembee? |
23461 | MAT 9:13 | Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.” |
23469 | MAT 9:21 | Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: “Nikigusa tu vazi lake, nitapona.” |
23478 | MAT 9:30 | Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.” |
23488 | MAT 10:2 | Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni aitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake; |
23491 | MAT 10:5 | Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria. |
23493 | MAT 10:7 | Mnapokwenda hubirini hivi: Ufalme wa mbinguni umekaribia. |
23531 | MAT 11:3 | wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?” |
23532 | MAT 11:4 | Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona: |
23535 | MAT 11:7 | Basi, hao wajumbe wa Yohane walipokuwa wanakwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu habari za Yohane: “Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo? |
23538 | MAT 11:10 | “Huyu ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: Tazama, hapa namtuma mjumbe wangu, asema Bwana, akutangulie na kukutayarishia njia yako. |
23544 | MAT 11:16 | “Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja kwa kingine: |
23546 | MAT 11:18 | Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: Amepagawa na pepo. |
23547 | MAT 11:19 | Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: Mtazameni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wahalifu! Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.” |
23548 | MAT 11:20 | Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kubadili nia zao mbaya: |
23565 | MAT 12:7 | Kama tu mngejua maana ya maneno haya: Nataka huruma wala si dhabihu, hamngewahukumu watu wasio na hatia. |
23575 | MAT 12:17 | ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: |
23602 | MAT 12:44 | Hapo hujisemea: Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka. Lakini anaporudi na kuikuta tupu, imefagiwa na kupambwa, |
23616 | MAT 13:8 | Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini. |
23622 | MAT 13:14 | Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona. |
23632 | MAT 13:24 | Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. |
23638 | MAT 13:30 | Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.” |
23639 | MAT 13:31 | Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake. |
23641 | MAT 13:33 | Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka.” |
23643 | MAT 13:35 | ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.” |
23657 | MAT 13:49 | Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema, |
23706 | MAT 15:4 | Mungu amesema: Waheshimu baba yako na mama yako, na Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe. |
23707 | MAT 15:5 | Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtolea Mungu, |
23709 | MAT 15:7 | Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu: |
23724 | MAT 15:22 | Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo.” |
23743 | MAT 16:2 | Lakini Yesu akawajibu, “Wakati wa jioni ukifika ninyi husema: Hali ya hewa itakuwa nzuri kwa maana anga ni jekundu! |
23744 | MAT 16:3 | Na alfajiri mwasema: Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda! Basi, ninyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui. |
23748 | MAT 16:7 | Lakini wao wakawa wanajadiliana: “Anasema hivyo kwa kuwa hatukuchukua mikate.” |
23759 | MAT 16:18 | Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda. |
23762 | MAT 16:21 | Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake: “Ni lazima mimi niende Yerusalemu, na huko nikapate mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Nitauawa, na siku ya tatu nitafufuliwa.” |
23763 | MAT 16:22 | Hapo Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea: “Isiwe hivyo Bwana! Jambo hili halitakupata!” |
23773 | MAT 17:4 | Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.” |
23774 | MAT 17:5 | Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.” |
23778 | MAT 17:9 | Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.” |
23789 | MAT 17:20 | Yesu akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale, nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu.” |
23836 | MAT 19:5 | na akasema: Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja? |
23843 | MAT 19:12 | Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.” |
23868 | MAT 20:7 | Wakamjibu: Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Yeye akawaambia, Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu. |
23891 | MAT 20:30 | Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!” |
23892 | MAT 20:31 | Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!” |
23899 | MAT 21:4 | Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii yatimie: |
23900 | MAT 21:5 | “Uambieni mji wa Sioni: Tazama, Mfalme wako anakujia! Ni mpole na amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda.” |
23904 | MAT 21:9 | Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaaza sauti: “Hosana Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Hosana Mungu juu mbinguni!” |
23908 | MAT 21:13 | Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala. Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.” |
23910 | MAT 21:15 | Basi, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaaza sauti zao Hekaluni wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika. |
23916 | MAT 21:21 | Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani bila kuwa na mashaka, mnaweza si tu kufanya hivyo, bali hata mkiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitose baharini, itafanyika hivyo. |
23920 | MAT 21:25 | Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa nani? Je, yalitoka mbinguni ama kwa watu?” Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi: “Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumsadiki? |
23932 | MAT 21:37 | Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: Watamheshimu mwanangu. |
23933 | MAT 21:38 | Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake! |
23942 | MAT 22:1 | Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano: |
23945 | MAT 22:4 | Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini. |
23949 | MAT 22:8 | Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili. |
23980 | MAT 22:39 | Ya pili inafanana na hiyo: Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. |
23984 | MAT 22:43 | Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema: |
23985 | MAT 22:44 | Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako. |
23994 | MAT 23:7 | Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: Mwalimu. |
24004 | MAT 23:17 | Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu? |
24006 | MAT 23:19 | Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu? |
24017 | MAT 23:30 | Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii! |
24026 | MAT 23:39 | Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.” |
24031 | MAT 24:5 | Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: Mimi ndiye Kristo, nao watawapotosha watu wengi. |
24049 | MAT 24:23 | “Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: Kristo yuko hapa au Yuko pale, msimsadiki. |