Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   “    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23233  MAT 1:20  Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
23236  MAT 1:23  Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa Emanueli” (maana yake, Mungu yu pamoja nasi”).
23240  MAT 2:2  wakauliza, Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.”
23242  MAT 2:4  Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria, akawauliza, Kristo atazaliwa wapi?”
23243  MAT 2:5  Nao wakamjibu, Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:
23246  MAT 2:8  Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu.”
23251  MAT 2:13  Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode anakusudia kumwua huyu mtoto.”
23253  MAT 2:15  Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”
23256  MAT 2:18  Sauti imesikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
23258  MAT 2:20  akamwambia, Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.”
23261  MAT 2:23  akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: Ataitwa Mnazare.”
23263  MAT 3:2  Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
23264  MAT 3:3  Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake.”
23268  MAT 3:7  Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
23275  MAT 3:14  Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.”
23276  MAT 3:15  Lakini Yesu akamjibu, Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka.” Hapo Yohane akakubali.
23278  MAT 3:17  Sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye.”
23281  MAT 4:3  Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
23282  MAT 4:4  Yesu akamjibu, Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.”
23284  MAT 4:6  akamwambia, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.”
23285  MAT 4:7  Yesu akamwambia, Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako.”
23287  MAT 4:9  akamwambia, Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu.”
23288  MAT 4:10  Hapo, Yesu akamwambia, Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.”
23293  MAT 4:15  Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
23295  MAT 4:17  Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!”
23297  MAT 4:19  Basi, akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu.”
23306  MAT 5:3  Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
23314  MAT 5:11  Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
23316  MAT 5:13  Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
23317  MAT 5:14  Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
23320  MAT 5:17  Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
23324  MAT 5:21  Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
23328  MAT 5:25  Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
23330  MAT 5:27  Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
23334  MAT 5:31  Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
23336  MAT 5:33  Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
23341  MAT 5:38  Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
23346  MAT 5:43  Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
23352  MAT 6:1  Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.
23353  MAT 6:2  Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23356  MAT 6:5  Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23358  MAT 6:7  Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
23365  MAT 6:14  Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia.
23367  MAT 6:16  Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23370  MAT 6:19  Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
23373  MAT 6:22  Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga.
23375  MAT 6:24  Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
23376  MAT 6:25  Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
23379  MAT 6:28  Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
23382  MAT 6:31  Basi, msiwe na wasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!
23386  MAT 7:1  Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
23391  MAT 7:6  Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua ninyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.
23392  MAT 7:7  Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
23397  MAT 7:12  Watendeeni wengine yale mnayotaka wao wawatendee ninyi. Hii ndiyo maana ya Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.
23398  MAT 7:13  Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi.
23400  MAT 7:15  Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
23406  MAT 7:21  Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
23409  MAT 7:24  Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
23411  MAT 7:26  Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
23416  MAT 8:2  Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”
23417  MAT 8:3  Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, Nataka! Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
23418  MAT 8:4  Kisha Yesu akamwambia, Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
23420  MAT 8:6  akisema, Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana.”
23421  MAT 8:7  Yesu akamwambia, Nitakuja kumponya.”
23422  MAT 8:8  Huyo ofisa akamwambia, Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
23424  MAT 8:10  Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii.
23427  MAT 8:13  Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini.” Na mtumishi wake akapona saa ileile.
23431  MAT 8:17  Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu.”
23433  MAT 8:19  Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako.”
23434  MAT 8:20  Yesu akamjibu, Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.”
23435  MAT 8:21  Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu.”
23436  MAT 8:22  Lakini Yesu akamwambia, Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao.”
23439  MAT 8:25  Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia!”
23440  MAT 8:26  Yesu akawaambia, Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.
23441  MAT 8:27  Watu wakashangaa, wakasema, Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!”
23443  MAT 8:29  Nao wakaanza kupiga kelele, Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?”
23445  MAT 8:31  Basi, hao pepo wakamsihi, Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale.”
23446  MAT 8:32  Yesu akawaambia, Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.
23450  MAT 9:2  Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.”
23451  MAT 9:3  Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, Mtu huyu anamkufuru Mungu!”
23452  MAT 9:4  Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
23454  MAT 9:6  Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”
23457  MAT 9:9  Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, Nifuate.” Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
23459  MAT 9:11  Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
23460  MAT 9:12  Yesu aliwasikia, akasema, Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.
23462  MAT 9:14  Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
23463  MAT 9:15  Yesu akawajibu, Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
23464  MAT 9:16  Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
23466  MAT 9:18  Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi.”
23469  MAT 9:21  Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: Nikigusa tu vazi lake, nitapona.”
23470  MAT 9:22  Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya.” Mama huyo akapona saa ileile.
23472  MAT 9:24  akasema, Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Nao wakamcheka.
23475  MAT 9:27  Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
23476  MAT 9:28  Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?” Nao wakamjibu, Naam, Mheshimiwa.”
23477  MAT 9:29  Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
23478  MAT 9:30  Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: Msimwambie mtu yeyote jambo hili.”
23481  MAT 9:33  Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!”
23482  MAT 9:34  Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya.”
23485  MAT 9:37  Hapo akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache.
23491  MAT 10:5  Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.