23265 | MAT 3:4 | Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. |
23340 | MAT 5:37 | Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu. |
23875 | MAT 20:14 | Chukua haki yako, uende zako. Napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. |
24041 | MAT 24:15 | “Basi, mtakapoona Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), |
24099 | MAT 25:22 | “Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata. |
24102 | MAT 25:25 | Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako. |
24140 | MAT 26:17 | Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?” |
24290 | MRK 1:6 | Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. |
24338 | MRK 2:9 | Ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, Umesamehewa dhambi zako, au kumwambia, Inuka! Chukua mkeka wako utembee? |
24499 | MRK 6:23 | Tena akamwapia, “Chochote utakachoniomba, nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu.” |
24657 | MRK 9:50 | Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu na kudumisha amani kati yenu.” |
24800 | MRK 13:14 | “Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani. |
24824 | MRK 14:1 | Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. |
24835 | MRK 14:12 | Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?” |
25331 | LUK 8:17 | “Chochote kilichofichwa kitafichuliwa na siri yoyote itagunduliwa na kujulikana hadharani. |
25552 | LUK 12:24 | Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Ninyi mna thamani zaidi kuliko ndege! |
25656 | LUK 14:34 | “Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? |
25695 | LUK 16:6 | Yeye akamjibu: Mapipa mia ya mafuta ya zeituni. Yule karani akamwambia: Chukua hati yako ya deni, keti haraka, andika hamsini. |
25696 | LUK 16:7 | Kisha akamwuliza mdeni mwingine: Wewe unadaiwa kiasi gani? Yeye akamjibu: Magunia mia ya ngano. Yule karani akamwambia: Chukua hati yako ya deni, andika themanini. |
25820 | LUK 19:20 | “Mtumishi mwingine akaja, akasema: Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa, |
26259 | JHN 4:34 | Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake. |
26290 | JHN 5:11 | Lakini yeye akawaambia, “Yule mtu aliyeniponya ndiye aliyeniambia: Chukua mkeka wako, tembea.” |
26291 | JHN 5:12 | Nao wakamwuliza, “Huyo mtu aliyekwambia: Chukua mkeka wako, tembea, ni nani?” |
27338 | ACT 10:10 | Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, alipatwa na usingizi mzito akaona maono. |
28322 | ROM 12:9 | Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema. |
28548 | 1CO 6:13 | Unaweza kusema: “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula.” Sawa; lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mtu si kwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili ya kumtumikia Bwana, naye Bwana ni kwa ajili ya mwili. |
28653 | 1CO 10:18 | Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu. |
28663 | 1CO 10:28 | Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile. |
29175 | GAL 3:6 | Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu. |
29580 | COL 2:19 | na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu. |
29896 | 2TI 2:2 | Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia. |
30398 | JAS 3:12 | Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu. |