Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   N    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23217  MAT 1:4  Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa Salmoni,
23238  MAT 1:25  Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.
23243  MAT 2:5  Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:
23246  MAT 2:8  Kisha akawatuma Bethlehemu akisema,Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu.”
23253  MAT 2:15  Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie:Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”
23255  MAT 2:17  Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia:
23260  MAT 2:22  Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya,
23261  MAT 2:23  akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.”
23268  MAT 3:7  Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
23270  MAT 3:9  Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, Baba yetu ni Abrahamu! Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
23288  MAT 4:10  Hapo, Yesu akamwambia,Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.”
23291  MAT 4:13  Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
23292  MAT 4:14  Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
23293  MAT 4:15  Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
23294  MAT 4:16  Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!”
23297  MAT 4:19  Basi, akawaambia,Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu.”
23301  MAT 4:23  Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
23316  MAT 5:13  Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
23317  MAT 5:14  Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
23323  MAT 5:20  Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
23333  MAT 5:30  Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.
23340  MAT 5:37  Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
23357  MAT 6:6  Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
23367  MAT 6:16  “Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
23369  MAT 6:18  ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika atakutuza.
23376  MAT 6:25  Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
23378  MAT 6:27  Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
23379  MAT 6:28  Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
23389  MAT 7:4  Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako, wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
23417  MAT 8:3  Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema,Nataka! Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
23421  MAT 8:7  Yesu akamwambia,Nitakuja kumponya.”
23423  MAT 8:9  Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda! naye huenda; na mwingine, Njoo! naye huja; na mtumishi wangu, Fanya kitu hiki! naye hufanya.”
23427  MAT 8:13  Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma,Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini.” Na mtumishi wake akapona saa ileile.
23436  MAT 8:22  Lakini Yesu akamwambia,Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao.”
23441  MAT 8:27  Watu wakashangaa, wakasema,Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!”
23443  MAT 8:29  Nao wakaanza kupiga kelele, “Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?”
23453  MAT 9:5  Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Simama, utembee?
23457  MAT 9:9  Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia,Nifuate.” Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
23461  MAT 9:13  Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
23469  MAT 9:21  Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: Nikigusa tu vazi lake, nitapona.”
23471  MAT 9:23  Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
23472  MAT 9:24  akasema, “Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Nao wakamcheka.
23476  MAT 9:28  Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, “Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?” Nao wakamjibu,Naam, Mheshimiwa.”
23477  MAT 9:29  Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema,Na iwe kwenu kama mnavyoamini.”
23478  MAT 9:30  Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.”
23483  MAT 9:35  Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
23504  MAT 10:18  Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
23507  MAT 10:21  Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe, nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
23513  MAT 10:27  Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong'onezwa, litangazeni hadharani.
23522  MAT 10:36  Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
23532  MAT 11:4  Yesu akawajibu,Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona:
23533  MAT 11:5  vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa na viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
23537  MAT 11:9  Basi, mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.
23544  MAT 11:16  “Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja kwa kingine:
23551  MAT 11:23  Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka Kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
23553  MAT 11:25  Wakati huo Yesu alisema,Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima mambo haya, ukawafumbulia watoto wadogo.
23554  MAT 11:26  Naam Baba, ndivyo ilivyokupendeza.
23556  MAT 11:28  Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
23562  MAT 12:4  Yeye aliingia katika Nyumba ya Mungu pamoja na wenzake, wakala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
23565  MAT 12:7  Kama tu mngejua maana ya maneno haya: Nataka huruma wala si dhabihu, hamngewahukumu watu wasio na hatia.
23571  MAT 12:13  Kisha akamwambia yule mtu,Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, nao ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.
23576  MAT 12:18  “Hapa ni mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka Roho yangu juu yake, naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.
23585  MAT 12:27  Ninyi mnasema ati nawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli; je, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo wao ndio watakaowahukumu ninyi.
23597  MAT 12:39  Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara; hamtapewa ishara nyingine, ila tu ile ishara ya nabii Yona.
23599  MAT 12:41  Watu wa Ninewi watatokea siku ya hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!
23602  MAT 12:44  Hapo hujisemea: Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka. Lakini anaporudi na kuikuta tupu, imefagiwa na kupambwa,
23603  MAT 12:45  huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”
23606  MAT 12:48  Lakini Yesu akamjibu mtu huyo, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni kina nani?”
23613  MAT 13:5  Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
23615  MAT 13:7  Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.
23619  MAT 13:11  Yesu akawajibu,Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
23621  MAT 13:13  Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
23637  MAT 13:29  Naye akawajibu, La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang'oa na ngano pia.
23643  MAT 13:35  ili jambo lililonenwa na nabii litimie:Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
23657  MAT 13:49  Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema,
23659  MAT 13:51  Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu,Naam.”
23660  MAT 13:52  Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”
23664  MAT 13:56  Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?”
23665  MAT 13:57  Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia,Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
23674  MAT 14:8  Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba,Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji.”
23684  MAT 14:18  Yesu akawaambia,Nileteeni hapa.”
23692  MAT 14:26  Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema,Ni mzimu!” Wakapiga kelele kwa hofu.
23708  MAT 15:6  basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.
23729  MAT 15:27  Huyo mama akajibu,Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
23734  MAT 15:32  Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema,Nawaonea watu hawa huruma kwa sababu kwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende bila kula wasije wakazimia njiani.”
23744  MAT 16:3  Na alfajiri mwasema: Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda! Basi, ninyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.
23756  MAT 16:15  Yesu akawauliza,Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?”