Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   O    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23218  MAT 1:5  Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu). Boazi na Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi, Obedi alimzaa Yese,
23269  MAT 3:8  Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
23390  MAT 7:5  Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
23392  MAT 7:7  Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
23472  MAT 9:24  akasema,Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Nao wakamcheka.
23549  MAT 11:21  Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia na kujipaka majivu zamani, ili kuonyesha kwamba wametubu.
23764  MAT 16:23  Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, Ondoka mbele yangu Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungu bali ni ya kibinadamu!”
23803  MAT 18:7  Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
24000  MAT 23:13  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.
24001  MAT 23:14  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
24002  MAT 23:15  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.
24003  MAT 23:16  Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika.
24010  MAT 23:23  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
24012  MAT 23:25  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
24014  MAT 23:27  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
24016  MAT 23:29  Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
24045  MAT 24:19  Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
24046  MAT 24:20  Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!
24118  MAT 25:41  “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
24602  MRK 8:33  Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema,Ondoka mbele yangu, Shetani! Fikira zako si za kimungu ila ni za kibinadamu!”
24803  MRK 13:17  Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
24804  MRK 13:18  Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
25126  LUK 3:32  mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
25184  LUK 5:8  Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema,Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!”
25240  LUK 6:25  Ole wenu ninyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia.
25241  LUK 6:26  Ole wenu ninyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.
25445  LUK 10:13  Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo, na kukaa katika majivu kuonyesha kwamba wametubu.
25517  LUK 11:43  Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
25518  LUK 11:44  Ole wenu, kwa sababu mko kama makaburi yaliyofichika; watu hutembea juu yake bila kufahamu.”
25521  LUK 11:47  Ole wenu, kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii wale ambao wazee wenu waliwaua.
25526  LUK 11:52  Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie.”
25618  LUK 13:31  Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia,Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua.”
25799  LUK 18:42  Yesu akamwambia,Ona! Imani yako imekuponya.”
25918  LUK 21:23  Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
26180  JHN 2:16  Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa,Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!”
26400  JHN 7:3  Basi ndugu zake wakamwambia,Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
26631  JHN 11:39  Yesu akasema,Ondoeni hilo jiwe!” Martha, dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, “Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!”
26819  JHN 16:24  Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
27188  ACT 7:3  Mungu alimwambia: Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonyesha!
27785  ACT 22:13  Yeye alikuja kuniona, akasimama karibu nami, akasema: Ndugu Saulo! Ona tena. Papo hapo nikaona tena, nikamwangalia.
27790  ACT 22:18  Nilimwona Bwana akiniambia: Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa binadamu hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.
28402  ROM 15:31  Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi, nayo huduma yangu huko Yerusalem ipate kukubaliwa na watu wa Mungu walioko huko.
28419  ROM 16:15  Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olumpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.
28983  2CO 6:17  Kwa hiyo Bwana asema pia:Ondokeni kati yao, mkajitenge nao, msiguse kitu najisi, nami nitawapokea.
29424  EPH 6:20  Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
29618  COL 4:9  Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika hapa.
29747  2TH 3:2  Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanaoamini ujumbe huu.
29892  2TI 1:16  Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
29956  2TI 4:19  Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
30015  PHM 1:10  Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
30016  PHM 1:11  Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia.
30020  PHM 1:15  Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena kuwa naye daima.
30412  JAS 4:8  Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!
30413  JAS 4:9  Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa.
30647  1JN 3:1  Oneni basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
30717  2JN 1:5  Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.
30751  JUD 1:11  Ole wao! Watu hao wamefuata mwenendo uleule wa Kaini. Kwa ajili ya fedha, wamejiingiza katika mkosi uleule wa Baalamu. Wameasi kama Kora alivyoasi na wameangamizwa kama yeye alivyoangamizwa.
30773  REV 1:8  “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
30908  REV 8:13  Kisha nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani anasema kwa sauti kubwa,Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!”
31072  REV 18:10  Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake, na kusema,Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”
31078  REV 18:16  wakisema,Ole! Ole kwa mji huu mkuu. Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi ya zambarau na nyekundu, na kujipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu!
31081  REV 18:19  Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!”
31128  REV 21:6  Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima.
31162  REV 22:13  Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”