Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   T    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23216  MAT 1:3  Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
23240  MAT 2:2  wakauliza, “Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.”
23263  MAT 3:2  Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
23295  MAT 4:17  Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema,Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!”
23336  MAT 5:33  Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
23355  MAT 6:4  Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
23379  MAT 6:28  “Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
23382  MAT 6:31  “Basi, msiwe na wasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!
23417  MAT 8:3  Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, “Nataka! Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
23489  MAT 10:3  Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
23538  MAT 11:10  “Huyu ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: Tazama, hapa namtuma mjumbe wangu, asema Bwana, akutangulie na kukutayarishia njia yako.
23540  MAT 11:12  Tangu wakati wa Yohane mbatizaji mpaka leo hii, Ufalme wa mbinguni unashambuliwa vikali, na watu wakali wanajaribu kuunyakua kwa nguvu.
23545  MAT 11:17  Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza; tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!
23549  MAT 11:21  “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia na kujipaka majivu zamani, ili kuonyesha kwamba wametubu.
23550  MAT 11:22  Hata hivyo nawaambieni, Siku ya hukumu, ninyi mtapata adhabu kubwa kuliko Tiro na Sidoni.
23560  MAT 12:2  Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu,Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato.”
23569  MAT 12:11  Lakini Yesu akawaambia,Tuseme mmoja wenu ana kondoo wake ambaye ametumbukia shimoni; je, hatamshika na kumtoa humo siku ya Sabato?
23590  MAT 12:32  Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.
23644  MAT 13:36  Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia,Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani.”
23653  MAT 13:45  Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
23655  MAT 13:47  Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
23683  MAT 14:17  Lakini wao wakamwambia,Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.”
23693  MAT 14:27  Mara, Yesu akasema nao,Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
23717  MAT 15:15  Petro akadakia,Tufafanulie huo mfano.”
23723  MAT 15:21  Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni.
23762  MAT 16:21  Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake: “Ni lazima mimi niende Yerusalemu, na huko nikapate mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Nitauawa, na siku ya tatu nitafufuliwa.”
23789  MAT 17:20  Yesu akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale, nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu.”
23815  MAT 18:19  Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
23855  MAT 19:24  Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.”
23858  MAT 19:27  Kisha Petro akasema, “Na sisi je? Tumeacha yote tukakufuata; tutapata nini basi?”
23879  MAT 20:18  “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe.
23883  MAT 20:22  Yesu akajibu, “Hamjui mnaomba nini. Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa mimi?” Wakamjibu,Tunaweza.”
23900  MAT 21:5  “Uambieni mji wa Sioni: Tazama, Mfalme wako anakujia! Ni mpole na amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda.”
23920  MAT 21:25  Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa nani? Je, yalitoka mbinguni ama kwa watu?” Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi:Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumsadiki?
24005  MAT 23:18  Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
24029  MAT 24:3  Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza,Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”
24033  MAT 24:7  Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
24036  MAT 24:10  Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
24052  MAT 24:26  Basi, wakiwaambieni, Tazameni, yuko jangwani, msiende huko; au, Tazameni, amejificha ndani, msisadiki;
24085  MAT 25:8  Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.
24149  MAT 26:26  Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema,Twaeni mle; huu ni mwili wangu.”
24168  MAT 26:45  Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
24169  MAT 26:46  Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.”
24188  MAT 26:65  Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
24243  MAT 27:45  Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
24286  MRK 1:2  Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.
24299  MRK 1:15  “Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!”
24322  MRK 1:38  Yesu akawaambia,Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo.”
24353  MRK 2:24  Mafarisayo wakawaambia,Tazama! Kwa nini wanafanya jambo ambalo si halali kufanya wakati wa Sabato?”
24365  MRK 3:8  Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
24375  MRK 3:18  Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na
24379  MRK 3:22  Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.”
24382  MRK 3:25  Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.
24391  MRK 3:34  Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema,Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.
24422  MRK 4:30  Tena, Yesu akasema,Tuufananishe Utawala wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani?
24427  MRK 4:35  Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake,Tuvuke ziwa, twende ng'ambo.”
24431  MRK 4:39  Basi, akaamka, akaukemea ule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa, “Kimya! Tulia!” Hapo upepo ukakoma, kukawa shwari kabisa.
24456  MRK 5:23  akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
24474  MRK 5:41  Kisha akamshika mkono, akamwambia,Talitha, kumi,” maana yake, “Msichana, nakwambia, amka!”
24478  MRK 6:2  Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
24486  MRK 6:10  Tena aliwaambia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
24499  MRK 6:23  Tena akamwapia, “Chochote utakachoniomba, nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu.”
24507  MRK 6:31  Alisema hivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mno walikuwa wanafika hapo na kuondoka hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasi ya kula chakula. Basi, Yesu akawaambia,Twendeni peke yetu mahali pa faragha kula chakula, mkapumzike kidogo.”
24526  MRK 6:50  Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao,Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
24536  MRK 7:4  Tena hawali kitu chochote kutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
24545  MRK 7:13  Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa ajili ya mafundisho mnayopokezana. Tena mnafanya mambo mengi ya namna hiyo.”
24556  MRK 7:24  Yesu aliondoka hapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
24563  MRK 7:31  Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
24628  MRK 9:21  “Amepatwa na mambo hayo tangu lini?” Naye akamjibu,Tangu utoto wake.
24685  MRK 10:28  Petro akamwambia, “Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!”
24690  MRK 10:33  “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe na kumkabidhi kwa watu wa mataifa.
24696  MRK 10:39  Wakamjibu,Tunaweza.” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli, na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa.
24703  MRK 10:46  Basi, wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwa anatoka katika mji huo akiwa na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mwombaji aitwaye Bartimayo mwana wa Timayo alikuwa ameketi kando ya barabara.
24723  MRK 11:14  Hapo akauambia mtini, Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
24740  MRK 11:31  Wakaanza kujadiliana,Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumsadiki?
24756  MRK 12:14  Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
24790  MRK 13:4  Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?”
24794  MRK 13:8  Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
24807  MRK 13:21  “Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
24825  MRK 14:2  Lakini walisema,Tusimtie nguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
24838  MRK 14:15  Naye atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
24845  MRK 14:22  Walipokuwa wanakula, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake akisema,Twaeni; huu ni mwili wangu.”
24865  MRK 14:42  Amkeni, twendeni zetu. Tazameni, yule atakayenisaliti amekaribia.”
24881  MRK 14:58  Tulimsikia mtu huyu akisema, Nitaliharibu Hekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono.”
24885  MRK 14:62  Yesu akajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenyezi, akija katika mawingu ya mbinguni.”
24886  MRK 14:63  Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema,Tuna haja gani tena ya mashahidi?
24899  MRK 15:4  Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako.”
24928  MRK 15:33  Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
24948  MRK 16:6  Lakini huyo kijana akawaambia, “Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwa wamemlaza.
24963  LUK 1:1  Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu.
25057  LUK 2:15  Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana:Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.”
25095  LUK 3:1  Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
25104  LUK 3:10  Umati wa watu ukamwuliza,Tufanye nini basi?”
25108  LUK 3:14  Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”