Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   V    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

23319  MAT 5:16  Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”
23803  MAT 18:7  Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
23909  MAT 21:14  Vipofu na vilema walimwendea huko Hekaluni, naye Yesu akawaponya.
23997  MAT 23:10  Wala msiitwe Viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo.
24011  MAT 23:24  Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!
24098  MAT 25:21  Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
24100  MAT 25:23  Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.
24485  MRK 6:9  Vaeni viatu lakini msivae kanzu mbili.”
24774  MRK 12:32  Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia,Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
25460  LUK 10:28  Yesu akawaambia,Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi.”
25655  LUK 14:33  Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho.
25817  LUK 19:17  Naye akamwambia: Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!
25926  LUK 21:31  Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.
26042  LUK 23:38  Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake: “Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.”
26183  JHN 2:19  Yesu akawaambia,Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu.”
26399  JHN 7:2  Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
26408  JHN 7:11  Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: “Yuko wapi?”
26432  JHN 7:35  Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?
26527  JHN 9:18  Viongozi wa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwa kipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaita wazazi wake.
26810  JHN 16:15  Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.
26972  JHN 21:5  Basi, Yesu akawauliza,Vijana, hamjapata samaki wowote sio?” Wao wakamjibu, “La! Hatujapata kitu.”
27099  ACT 4:8  Hapo, Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akawaambia,Viongozi na wazee wa watu!
27134  ACT 5:6  Vijana wakafika wakaufunika mwili wake, wakamtoa nje, wakamzika.
27218  ACT 7:33  Bwana akamwambia: Vua viatu vyako maana hapa unaposimama ni mahali patakatifu.
27235  ACT 7:50  Ni nyumba ya namna gani basi mnayoweza kunijengea, na ni mahali gani nitakapopumzika? Vitu hivi vyote ni mimi nimevifanya, au sivyo?
27414  ACT 12:8  Malaika akamwambia, “Jifunge mshipi wako, vaa viatu vyako.” Akafanya hivyo. Kisha huyo malaika akamwambia,Vaa koti lako, unifuate.”
27561  ACT 16:9  Usiku huo, Paulo aliona ono ambalo alimwona mtu mmoja wa Makedonia amesimama pale na kumwomba:Vuka, uje Makedonia ukatusaidie.”
27612  ACT 17:20  Vitu vingine tulivyosikia kwa masikio yetu vinaonekana kuwa viroja kwetu. Tungependa kujua mambo haya yana maana gani.”
28073  ROM 3:14  Vinywa vyao vimejaa laana chungu.
28102  ROM 4:12  Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.
28203  ROM 8:19  Viumbe vyote vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.
28368  ROM 14:20  Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya ubishi juu ya chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.
28569  1CO 7:14  Kwa maana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mkewe; na huyo mke asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwa si wa Mungu; kumbe sasa ni watoto wake Mungu.
28658  1CO 10:23  Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.
28693  1CO 11:25  Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
28706  1CO 12:4  Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.
28747  1CO 14:1  Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
28813  1CO 15:27  Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema:Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
29363  EPH 4:24  Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.
29415  EPH 6:11  Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
29548  COL 1:16  Maana kwa njia yake vitu vyote viliumbwa duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye mamlaka. Vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.
29597  COL 3:13  Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe ninyi.
29612  COL 4:3  Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
29855  1TI 5:25  Vivyo hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo si dhahiri hayawezi kufichika.
30193  HEB 9:21  Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada.
30195  HEB 9:23  Vitu hivi ambavyo ni mfano tu wa mambo halisi ya mbinguni, vililazimika kutakaswa kwa namna hiyo. Lakini vitu vya mbinguni huhitaji dhabihu iliyo bora zaidi.
30286  HEB 12:7  Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea ninyi kama wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake?
30344  JAS 1:11  Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake.
30377  JAS 2:17  Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
30391  JAS 3:5  Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
30545  1PE 5:13  Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
30633  1JN 2:16  Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.
30800  REV 2:15  Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
30842  REV 4:6  Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo vilikuwa vimejaa macho mbele na nyuma.
30844  REV 4:8  Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”
30917  REV 9:9  Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafara wa magari ya farasi wengi wanaokimbilia vitani.
30925  REV 9:17  Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao.
31043  REV 16:20  Visiwa vyote vikatoweka, nayo milima haikuonekena tena.
31053  REV 17:9  “Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.