23513 | MAT 10:27 | Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong'onezwa, litangazeni hadharani. |
24610 | MRK 9:3 | mavazi yake yakang'aa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe. |
25451 | LUK 10:19 | Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng'e, na uwezo juu ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru. |
26178 | JHN 2:14 | Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao. |
26558 | JHN 10:8 | Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. |
28545 | 1CO 6:10 | wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang'anyi, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu. |
28645 | 1CO 10:10 | Wala msinung'unike kama baadhi yao walivyonung'unika, wakaangamizwa na Mwangamizi! |
28946 | 2CO 5:1 | Maana tunajua kwamba hema hii ambayo ndani yake tunaishi sasa hapa duniani, yaani mwili wetu, itakapong'olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono. |
29110 | 2CO 12:20 | Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyano, kunong'ona, majivuno na fujo kati yenu. |
30184 | HEB 9:12 | Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa amechukua damu ya mbuzi wala ng'ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele. |
30843 | REV 4:7 | Kiumbe cha kwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng'ombe, cha tatu kilikuwa na sura kama mtu, na cha nne kilikuwa kama tai anayeruka. |
30918 | REV 9:10 | Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano. |
31021 | REV 15:6 | Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, na kanda za dhahabu vifuani mwao. |