Wildebeest analysis examples for:   swh-swhonen   ”    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

3  GEN 1:3  Mungu akasema, “Iwepo nuru, nayo nuru ikawepo.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “mchana, na giza akaliita “usiku. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6  GEN 1:6  Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.
8  GEN 1:8  Mungu akaiita hiyo nafasi “anga. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.
9  GEN 1:9  Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu. Ikawa hivyo.
10  GEN 1:10  Mungu akaiita nchi kavu “ardhi, nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari. Mungu akaona kuwa ni vyema.
11  GEN 1:11  Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali. Ikawa hivyo.
15  GEN 1:15  nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia. Ikawa hivyo.
20  GEN 1:20  Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.
22  GEN 1:22  Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.
24  GEN 1:24  Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake. Ikawa hivyo.
26  GEN 1:26  Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.
28  GEN 1:28  Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.
30  GEN 1:30  Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula. Ikawa hivyo.
48  GEN 2:17  lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.
49  GEN 2:18  Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.
54  GEN 2:23  Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.
57  GEN 3:1  Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?
59  GEN 3:3  lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’
61  GEN 3:5  Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
65  GEN 3:9  Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?
66  GEN 3:10  Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.
67  GEN 3:11  Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?
68  GEN 3:12  Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.
69  GEN 3:13  Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya? Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.
71  GEN 3:15  Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.
72  GEN 3:16  Kwa mwanamke akasema, “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto. Tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.
75  GEN 3:19  Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.
78  GEN 3:22  Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.
81  GEN 4:1  Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.
87  GEN 4:7  Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.
88  GEN 4:8  Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani. Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.
89  GEN 4:9  Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi? Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
92  GEN 4:12  Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.
94  GEN 4:14  Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.
95  GEN 4:15  Lakini Bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi. Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue.
104  GEN 4:24  Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba, basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.
105  GEN 4:25  Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimuua.
108  GEN 5:2  Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.
135  GEN 5:29  Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.
141  GEN 6:3  Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.
145  GEN 6:7  Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.
159  GEN 6:21  Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.
164  GEN 7:4  Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.
201  GEN 8:17  Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.
206  GEN 8:22  “Kwa muda dunia idumupo, wakati wa kupanda na wa kuvuna, wakati wa baridi na wa joto, wakati wa kiangazi na wa masika, usiku na mchana kamwe havitakoma.
213  GEN 9:7  Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.
217  GEN 9:11  Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.
222  GEN 9:16  Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.
223  GEN 9:17  Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.
231  GEN 9:25  akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini sana kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.
233  GEN 9:27  Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, na Kanaani na awe mtumwa wake.
244  GEN 10:9  Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.
270  GEN 11:3  Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto. Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.
271  GEN 11:4  Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.
274  GEN 11:7  Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.
302  GEN 12:3  Nitawabariki wale wanaokubariki, na yeyote akulaaniye nitamlaani; na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.
306  GEN 12:7  Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii. Hivyo hapa akamjengea madhabahu Bwana aliyekuwa amemtokea.
312  GEN 12:13  Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.
318  GEN 12:19  Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!
328  GEN 13:9  Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.
336  GEN 13:17  Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.
357  GEN 14:20  Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana, ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako. Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.
358  GEN 14:21  Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.
361  GEN 14:24  Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.
362  GEN 15:1  Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
363  GEN 15:2  Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?
364  GEN 15:3  Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.
365  GEN 15:4  Ndipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.
366  GEN 15:5  Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu. Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.
368  GEN 15:7  Pia akamwambia, “Mimi ndimi Bwana, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.
369  GEN 15:8  Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?
370  GEN 15:9  Ndipo Bwana akamwambia, “Niletee mtamba wa ngʼombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.
377  GEN 15:16  Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.
382  GEN 15:21  Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.
384  GEN 16:2  hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake. Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.
387  GEN 16:5  Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Bwana na aamue kati yako na mimi.
388  GEN 16:6  Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi. Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.
390  GEN 16:8  Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi? Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.
391  GEN 16:9  Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.
392  GEN 16:10  Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.
394  GEN 16:12  Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.
395  GEN 16:13  Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi, kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.
400  GEN 17:2  Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
406  GEN 17:8  Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.
412  GEN 17:14  Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.
414  GEN 17:16  Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.
415  GEN 17:17  Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?
416  GEN 17:18  Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!
419  GEN 17:21  Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.
430  GEN 18:5  Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu. Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.
431  GEN 18:6  Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.
434  GEN 18:9  Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo? Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.
435  GEN 18:10  Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana. Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.
437  GEN 18:12  Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?
439  GEN 18:14  Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.
440  GEN 18:15  Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka. Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!
444  GEN 18:19  Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.
446  GEN 18:21  kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.
450  GEN 18:25  Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?