Wildebeest analysis examples for:   swh-swhonen   a    February 25, 2023 at 01:16    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

1  GEN 1:1  Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
2  GEN 1:2  Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
3  GEN 1:3  Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.
4  GEN 1:4  Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6  GEN 1:6  Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
7  GEN 1:7  Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.
8  GEN 1:8  Mungu akaiita hiyo nafasi anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.
9  GEN 1:9  Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo.
10  GEN 1:10  Mungu akaiita nchi kavu ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.
11  GEN 1:11  Kisha Mungu akasema, Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.