1 | GEN 1:1 | Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. |
2 | GEN 1:2 | Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji. |
3 | GEN 1:3 | Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. |
4 | GEN 1:4 | Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. |
5 | GEN 1:5 | Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza. |
6 | GEN 1:6 | Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” |
7 | GEN 1:7 | Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. |
8 | GEN 1:8 | Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili. |
9 | GEN 1:9 | Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo. |
10 | GEN 1:10 | Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. |
11 | GEN 1:11 | Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo. |
12 | GEN 1:12 | Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema. |
13 | GEN 1:13 | Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu. |
14 | GEN 1:14 | Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, |