549 | GEN 22:1 | Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.” |
5602 | DEU 27:15 | “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5603 | DEU 27:16 | “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5604 | DEU 27:17 | “Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5605 | DEU 27:18 | “Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5606 | DEU 27:19 | “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5607 | DEU 27:20 | “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5608 | DEU 27:21 | “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5609 | DEU 27:22 | “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5610 | DEU 27:23 | “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5611 | DEU 27:24 | “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5612 | DEU 27:25 | “Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
5613 | DEU 27:26 | “Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
7284 | 1SA 3:6 | Bwana akaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.” Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.” |
8236 | 2SA 9:6 | Mefiboshethi mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, alipofika kwa Daudi, akainama kumpa mfalme heshima. Daudi akamwita, “Mefiboshethi!” Mefiboshethi akajibu, “Ndimi mtumishi wako.” |
9191 | 1KI 13:4 | Mfalme Yeroboamu aliposikia kile mtu wa Mungu alichosema, alipopiga kelele dhidi ya madhabahu huko Betheli, akanyoosha mkono wake kutoka madhabahuni na kusema, “Mkamate!” Lakini mkono aliokuwa ameunyoosha kumwelekea yule mtu ukasinyaa na kubaki hapo hapo, kiasi kwamba hakuweza kuurudisha. |
14334 | PSA 29:9 | Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” |
15766 | PSA 106:48 | Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana. |
20643 | EZK 6:11 | “ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni. |
20837 | EZK 16:6 | “ ‘Ndipo nilipopita karibu nawe nikakuona ukigaagaa kwenye damu yako, nawe ulipokuwa umelala hapo penye hiyo damu nikakuambia, “Ishi!” |
21155 | EZK 25:3 | Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni, |
22302 | HOS 10:8 | Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!” |
22802 | HAB 1:2 | Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada, lakini wewe husikilizi? Au kukulilia, “Udhalimu!” Lakini hutaki kuokoa? |
23446 | MAT 8:32 | Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji. |
24220 | MAT 27:22 | Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote, “Msulubishe!” |
24221 | MAT 27:23 | Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!” |
24273 | MAT 28:9 | Ghafula, Yesu akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu. |
24566 | MRK 7:34 | Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akavuta hewa ndani kwa nguvu akamwambia, “Efatha!” (yaani, “Funguka!”) |
24718 | MRK 11:9 | Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” |
24888 | MRK 14:65 | Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi. |
24908 | MRK 15:13 | Wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe!” |
24909 | MRK 15:14 | Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!” |
25984 | LUK 22:51 | Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya. |
26034 | LUK 23:30 | Ndipo “ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!” na vilima, “Tufunikeni!” ’ |
26662 | JHN 12:13 | Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!” |
26952 | JHN 20:16 | Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu). |
26986 | JHN 21:19 | Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate!” |
27295 | ACT 9:10 | Huko Dameski alikuwepo mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana alimwita katika maono, “Anania!” Akajibu, “Mimi hapa Bwana.” |
27331 | ACT 10:3 | Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!” |
30861 | REV 5:14 | Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu. |
30862 | REV 6:1 | Kisha nikaangalia wakati Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!” |
30864 | REV 6:3 | Alipoivunja ile lakiri ya pili, nikamsikia yule kiumbe wa pili mwenye uhai akisema, “Njoo!” |
30866 | REV 6:5 | Mwana-kondoo alipoivunja ile lakiri ya tatu, nikamsikia yule kiumbe wa tatu mwenye uhai akisema, “Njoo!” Nikatazama, na mbele yangu alikuwepo farasi mweusi! Yeye aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. |
30868 | REV 6:7 | Alipovunja ile lakiri ya nne, nikasikia sauti ya yule kiumbe wa nne mwenye uhai ikisema, “Njoo!” |
31166 | REV 22:17 | Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Yeyote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure. |