72 | GEN 3:16 | Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.” |
73 | GEN 3:17 | Kwa Adam akasema, “kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, “ usile matunda yake', ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako. |
103 | GEN 4:23 | Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua. |
145 | GEN 6:7 | Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.” |
150 | GEN 6:12 | Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi. |
176 | GEN 7:16 | Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango. |
297 | GEN 11:30 | Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto. |
318 | GEN 12:19 | Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.” |
327 | GEN 13:8 | Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia. |
346 | GEN 14:9 | dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafme wanne dhidi ya wale watano. |
365 | GEN 15:4 | Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako.” |
396 | GEN 16:14 | Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi. |
491 | GEN 19:33 | Kwa hiyo wakamnywesha baba yako mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka. |
508 | GEN 20:12 | Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu. |
520 | GEN 21:6 | Sara akasema, “Mungu amenifanya nicheke; kila mtu atakaye sikia atacheka pamoja na nami.” |
532 | GEN 21:18 | Inuka msimamishe mtoto, na umtie moyo; kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.” |
540 | GEN 21:26 | Abimeleki akasema, “Sijui ni nani amefanya jambo hili. Hukuniambia mapema; na sijalisikia ila leo hii.” |
554 | GEN 22:6 | Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja. |
565 | GEN 22:17 | hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao. |
642 | GEN 24:50 | Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, “Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri. |
660 | GEN 25:1 | Abraham akaoa mke mwingine; jina lake aliitwa Ketura. |
675 | GEN 25:16 | Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao. |
686 | GEN 25:27 | Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema. |
695 | GEN 26:2 | Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, “Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia. |
696 | GEN 26:3 | Kaa katika nchi hii hii niliyokuambia, nami nitakuwa pamoja nawe na kukubariki; kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote, nami nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. |
737 | GEN 27:9 | Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo. |
746 | GEN 27:18 | Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, “Babangu.” Yeye akasema, “Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?” |
747 | GEN 27:19 | Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki.” |
750 | GEN 27:22 | Yakobo akamkaribia Isaka baba yake; na Isaka akamgusa na kusema, “Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mkikono ya Esau.” |
757 | GEN 27:29 | Watu na wakutumikie na mataifa yainame chini yako. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wainame chini yako. Kila anayekulaani na alaaniwe; na kila anayekubariki abarikiwe.” |
769 | GEN 27:41 | Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka ambayo baba yake alimpa. Esau akajisemea moyoni, “Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia; baada ya hapo nitamwua Yakobo ndugu yangu.” |
789 | GEN 28:15 | Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi.” |
816 | GEN 29:20 | Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake. |
828 | GEN 29:32 | Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, “Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda.” |
831 | GEN 29:35 | Akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Wakati huu nitamsifu Yahwe.” Kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; kisha akaacha kuzaa watoto. |
870 | GEN 30:39 | Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa. |
914 | GEN 31:40 | Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi. |
995 | GEN 34:14 | Wakawambia, “Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu mtu yeyote ambaye hajatailiwa; kwani hiyo ni aibu kwetu. |
1043 | GEN 36:2 | Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na |
1051 | GEN 36:10 | Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau. |
1267 | GEN 42:14 | Yusufu akawambia, “Ndivyo nilivyowambia; ninyi ni wapelelezi. |
1293 | GEN 43:2 | Ikawa walipokuwa wametumia chakula chote walichokitoa Misri, baba yao akawambia, “Nendeni tena; mtununulie chakula.” |
1395 | GEN 46:8 | Haya ni majina ya watoto wa Israeli waliokuja Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo; |
1396 | GEN 46:9 | wana wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi; |
1397 | GEN 46:10 | wana wa Simoni, Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli, wana wa mwanamke Mkanaani; |
1400 | GEN 46:13 | Wana wa Isakari walikuwa Tola, Puva, Lobu, na Shimroni; |
1404 | GEN 46:17 | Wana wa Asheri walikuwa Imna, Ishva, Ishvi, na Beria; na Sera alikuwa dada yao. Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malkieli. |
1434 | GEN 47:13 | Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa. |
1458 | GEN 48:6 | Watoto utakaowapata baada ya hapo ni wako; watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao. |
1470 | GEN 48:18 | Yusufu akamwambia baba yake, “Sivyo babangu; kwani huyu ndiye mzaliwa wa kwanza. Uweke mkono wako juu ya kichwa chake.” |
1478 | GEN 49:4 | Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia. |
1480 | GEN 49:6 | Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe. |
1495 | GEN 49:21 | Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri. |
1505 | GEN 49:31 | Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea. |
1531 | GEN 50:24 | Yusufu akawambia ndugu zake, “Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nch aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo.” |
1548 | EXO 1:15 | Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kiebrania; mmoja wao aliitwa jina lake Shifra, na mwingine aliitwa Puha. |
1549 | EXO 1:16 | Akasema, “Wakati mnapowasaidia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni wanapozaa. Ikiwa ni mtoto wa kiume, basi muueni; bali ikiwa ni mtoto wa kike, basi mwacheni aishi.” |
1550 | EXO 1:17 | Lakini wale Wakunga walimwogopa Mungu na hawakufanya kama mfalme wa Misri alivyowaagiza; badala yake waliwaacha watoto wa kiume waishi. |
1577 | EXO 2:22 | Alizaa mtoto wa kiume, na Musa akamwita jina lake Geshomu; akisema; “Nimekuwa mkazi katika nchi ya ugeni.” |
1588 | EXO 3:8 | Nimekuja chini kuwaokoa dhidi ya mamlaka ya Wamisri na kuwatoa katika nchi ile na kuwaleta katika nchi nzuri, pana, nchi ijaayo maziwa na asali; kwenye ukanda wa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi. |
1635 | EXO 5:2 | Farao akasema, “Yahwe ni nani? Kwa nini mimi nisikiliz sauti yake na kuwaacha Israeli waende? Mimi simjui Yahwe; na la zaidi, sitawaacha Israeli waende.” |
1659 | EXO 6:3 | Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao. |
1692 | EXO 7:6 | Musa na Aruni wakafanya hivyo; walifanya kama Yahweh alivyo waamuru. |
1748 | EXO 9:5 | Yahweh ametenga muda; amesema, “Ni kesho ambapo nitafanya ilitukio katika nchi."”' |
1776 | EXO 9:33 | Musa alipo muacha Farao na mji, alitanua mikono yake kwa Yahweh; mngurumo na barafu ya mawe ikasimama, na mvua haikunyesha tena. |
1797 | EXO 10:19 | Yahweh akaleta upepo mkali wa magharibi ulio wachukuwa wale nzige na kuwapeleka Bahari ya Shamu; hakuna nzige ata mmoja aliye baki eneo la Misri. |
1801 | EXO 10:23 | Hakuna aliye muona mwingine; hakuna aliye toka nyumbani mwake kwa siku tatu. Walakini, Waisraeli wote walikuwa na taa katika sehemu walizo ishi. |
1804 | EXO 10:26 | Mifugo yetu lazima iende na sisi; ata mmoja hawezi kubaki, lazima tuwapeleke wakamuabudu Yahweh Mungu wetu. Kwa kuwa hatujui tutakacho muabudu nacho Yahweh mpaka tufike pale. |
1874 | EXO 13:6 | Kwa siku saba utakula mkate bila hamira; siku ya saba kutakuwa na maakuli ya kumuadhimisha Yahweh. |
1875 | EXO 13:7 | Mkate usio na hamira wapaswa kuliwa kwa siku saba zote; hakuna mkate ulio na hamira wapaswa kuliwa miongoni mwenu. Hakuna hamira yapaswa kuonekana kwenye mipaka yenu. |
1922 | EXO 15:1 | Kisha Musa na watu wa Israeli wakaimba hii nyimbo kwa Yahweh. Waliimba, “Nitaimba kwa Yahweh, kwa kuwa ameshinda kwa utukufu; farasi na dereva wake amewatupa kwenye bahari. |
1924 | EXO 15:3 | Yahweh ni shujaa; Yahweh ni jina lake. |
1926 | EXO 15:5 | Kina kiliwafunika; walienda kwenye kina kama jiwe. |
1927 | EXO 15:6 | Mkono wako wakulia, Yahweh, una nguvu ya utukufu; mkono wako, Yahweh, umewavunja adui. |
1928 | EXO 15:7 | Kwa utukufu mkubwa umewapindua walio inuka dhidi yako. Umetuma gadhabu; imewateketeza kama karatasi. |
1929 | EXO 15:8 | Kwa pumzi ya pua yako maji yalijaa; maji yanayo tembea yalisimama wima na kujaa juu; maji yalikuwa manene ndani ya kilindi cha bahari. |
1930 | EXO 15:9 | Adui alisema, 'Nitakimbiza, nitapita, nitagawa nitakacho chukuwa; tamanio langu litatimizwa kwao; nitavuta upanga wangu; mkono wangu utawaharibu wao.' |
1931 | EXO 15:10 | Lakini ulipuliza kwa upepo wako, na bahari ikawafunika wao; walizama kama chuma nzito kwenye maji mengi. |
1935 | EXO 15:14 | Watu watasikia, na watatetemeka; hofu itawakumba wakazi wa Filistia. |
1936 | EXO 15:15 | Kisha wazee wa Edomu wataogopa; wanajeshi wa Moabu watetemeka; wakazi wote wa Kanani watayayuka. |
1956 | EXO 16:8 | Musa pia akasema, “Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa tele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayo tamka dhidi yake. Nani ni Aruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh.” |
1977 | EXO 16:29 | Tazama, Yahweh amekupa Sabato. Hivyo siku ya sita anakupa mkate wa siku mbili. Kila mmoja wenu lazima akae kwenye sehemu yake; hakuna hata mmoja wa kutoka sehemu yake siku ya saba.” |
1995 | EXO 17:11 | Wakati Musa alipo kuwa ameshikilia mikono yake juu, Israeli ilikuwa yashinda; alipo acha mikono yake ipumzike, Ameleki alianza kushinda. |
2003 | EXO 18:3 | na wana wake wawili; jina mmoja lilikuwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” |
2042 | EXO 19:15 | Aliwaambia watu, “Kuweni tayari siku ya tatu; msiwakaribie wake zenu.” |
2069 | EXO 20:17 | Usitaman nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wakiume, mtumishi wake mwanamke, ng'ombe wake, punda wake, au chochote cha jirani yako. |
2071 | EXO 20:19 | Wakamwambia Musa, ongea na sisi, na tutakusikiliza; lakini usiruhusu Mungu kuongea nasi, ama tutakufa. |
2078 | EXO 20:26 | msije juu ya madhabahu yangu kwa hatua zenu; hii ni ili msioneshe sehemu zenu za siri.” |
2081 | EXO 21:3 | Kama alikuja mwenyewe, ataenda huru kwa ridhaa yake; |
2083 | EXO 21:5 | Lakini kama mtumishi atasema waziwazi, “Nampenda bwana wangu, mke wangu, na watoto; sitaenda nje,” |
2092 | EXO 21:14 | Lakini mtu akimwendea mwenzake kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata kama ni madhabahuni pangu, ili auawe. |
2096 | EXO 21:18 | Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani; |
2097 | EXO 21:19 | kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliye mpiga lazima alipe muda aliye mpotezea; na lazima alipe matibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji. |
2106 | EXO 21:28 | Kama ng'ombe akimpiga mwanaume au mwanamke akafa, ng'ombe lazima apigwe mawe, na nyama yake hairuhusiwi kuliwa; lakini mmiliki wa ng'ombe lazima awe huru kwa hatia. |
2129 | EXO 22:14 | Lakini kama mmiliki alikuwa nae, mwanaume mwengine haitaji kulipa; kama mnyama aliazimwa, atalipwa kwa gharama ya kuazima. |
2138 | EXO 22:23 | Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba. |
2184 | EXO 24:6 | Musa allichukuwa nusu ya damu na kuweka kwenye mabeseni; alinyunyuzia nusu ingine kwenye madhabahu. |
2199 | EXO 25:3 | Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba, |
2200 | EXO 25:4 | buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi; |
2202 | EXO 25:6 | mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; |