3 | GEN 1:3 | Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru. |
5 | GEN 1:5 | Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza. |
6 | GEN 1:6 | Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.” |
8 | GEN 1:8 | Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili. |
9 | GEN 1:9 | Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. |
10 | GEN 1:10 | Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema. |
11 | GEN 1:11 | Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo. |
15 | GEN 1:15 | Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo. |
20 | GEN 1:20 | Mungu akasema, “maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.” |
22 | GEN 1:22 | Mungu akavibariki, akisema, “zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.” |
24 | GEN 1:24 | Mungu akasema, “ nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo. |
26 | GEN 1:26 | Mung akasema, “na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.” |
28 | GEN 1:28 | Mungu akawabariki na akawaambia, “zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,” |
30 | GEN 1:30 | Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai ni metoa kila mmea kwa ajili ya chakula.” ikawa hivyo. |
48 | GEN 2:17 | Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.” |
49 | GEN 2:18 | Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.” |
57 | GEN 3:1 | Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?” |
59 | GEN 3:3 | lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'” |
61 | GEN 3:5 | Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” |
65 | GEN 3:9 | Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “ uko wapi?” |
66 | GEN 3:10 | Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.” |
67 | GEN 3:11 | Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?” |
68 | GEN 3:12 | Mwanaume akasema, “ Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.” |
69 | GEN 3:13 | Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.” |
71 | GEN 3:15 | Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.” |
72 | GEN 3:16 | Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.” |
75 | GEN 3:19 | Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi.” |
78 | GEN 3:22 | Yahwe Mungu akasema, “ sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele.” |
81 | GEN 4:1 | Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, “ nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe.” |
88 | GEN 4:8 | Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua). |
89 | GEN 4:9 | Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” |
92 | GEN 4:12 | Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.” |
94 | GEN 4:14 | Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.” |
95 | GEN 4:15 | Yahwe akamwambia, “ikiwa mtuyeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba.” Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu awayeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie. |
104 | GEN 4:24 | Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.” |
105 | GEN 4:25 | Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, “ Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.” |
135 | GEN 5:29 | Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.” |
141 | GEN 6:3 | Yahwe akaema, “ roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.” |
145 | GEN 6:7 | Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.” |
159 | GEN 6:21 | Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao.” |
164 | GEN 7:4 | Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi.” |
201 | GEN 8:17 | Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi.” |
206 | GEN 8:22 | Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.” |
213 | GEN 9:7 | Na hivyo nanyi zaeni na kuongezeka, sambaeni katika inchi yote na muongezeke juu yake.” |
217 | GEN 9:11 | Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi.” |
222 | GEN 9:16 | Upinde wa mvua utakuwa katika mawingu na nitauona, ili kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na kila kiumbe hai cha wote wenye mwili ambacho kiko juu ya nchi.” |
223 | GEN 9:17 | Kisha Mungu akamwambia Nuhu, “ Hii ni ishara ya agano ambalo nimelithibitisha kati yangu na wenye mwili wote ambao wako juu ya nchi.” |
231 | GEN 9:25 | Hivyo akasema, “Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake.” |
233 | GEN 9:27 | Mungu na apanuwe mipaka ya Yafethi, na afanye makazi yake katika hema za Shemu. Kanaani na awe mtumwa wake.” |
244 | GEN 10:9 | Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.” |
270 | GEN 11:3 | Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa. |
271 | GEN 11:4 | Wakasema, “njoni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote.” |
274 | GEN 11:7 | Njoni, tushuke na tuvuruge lugha yao pale, ili kwamba wasielewane.” |
306 | GEN 12:7 | Yahwe akamtokea Abram, na kusema, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Kwa hiyo Abram akamjengea madhabahu, Yahwe ambaye alimtokea. |
312 | GEN 12:13 | Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumba maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako.” |
318 | GEN 12:19 | Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.” |
328 | GEN 13:9 | Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.” |
336 | GEN 13:17 | Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia.” |
357 | GEN 14:20 | Abarikiwe Mungu aliye juu sana, ambaye amekupatia adui zako katika mikono yako.” Kisha Abram akampatia sehemu ya kumi ya kila kitu. |
358 | GEN 14:21 | Mfalme wa Sodama akamwambia Abram, “Nipatie watu, na ujichukulie wewe mwenyewe mali.” |
361 | GEN 14:24 | Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula na sehemu za watu waliokwenda nami. Aneri, Eskoli, na Mamre na wachukue sehemu zao.” |
362 | GEN 15:1 | Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” |
363 | GEN 15:2 | Abram akasema, “Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?” |
364 | GEN 15:3 | Abram akasema, “Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu.” |
365 | GEN 15:4 | Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako.” |
366 | GEN 15:5 | Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa. |
368 | GEN 15:7 | Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi.” |
369 | GEN 15:8 | Akasema, “Bwana Yahwe, nitajua je kuwa nitairithi?” |
370 | GEN 15:9 | Kisha akamwambia, “Nipatie ndama wa umri wa miaka mitatu, mbuzi mke wa umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa umri wa miaka mitatu, na njiwa na mwana njiwa.” |
377 | GEN 15:16 | Katika kizazi cha nne watakuja tena hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujafikia mwisho wake.” |
384 | GEN 16:2 | Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai. |
387 | GEN 16:5 | Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe.” |
388 | GEN 16:6 | Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka. |
390 | GEN 16:8 | Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?” Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai.” |
391 | GEN 16:9 | Malaika wa Yahwe akamwambia, “ Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake.” |
392 | GEN 16:10 | Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, “Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika.” |
394 | GEN 16:12 | Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote.” |
395 | GEN 16:13 | Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, “Wewe ni Mungu unionaye mimi,” kwa kuwa alisema, “je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?” |
406 | GEN 17:8 | Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.” |
412 | GEN 17:14 | Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu.” |
415 | GEN 17:17 | Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?” |
416 | GEN 17:18 | Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!” |
419 | GEN 17:21 | Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.” |
430 | GEN 18:5 | Nami acha nilete chakula kidogo, ili kwamba mjiburudishe wenyewe. Ndipo baadae mwaweza kwenda zenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” Nao wakasema, “Fanya kama ulivyo sema.” |
431 | GEN 18:6 | Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, “Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate.” |
434 | GEN 18:9 | Wakamwambia, “Mke wako Sara yuko wapi?” akajibu. “pale hemani.” |
435 | GEN 18:10 | akasema, “Hakika nitarejea kwako majira ya machipuko, na tazama Sara mkeo atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa akisikiliza mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake. |
437 | GEN 18:12 | Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, “baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?” |
439 | GEN 18:14 | Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” |
440 | GEN 18:15 | Kisha Sara akakataa na kusema, “sikucheka,” kwa kuwa aliogopa. Yahwe akasema, “hapana ulicheka.” |
444 | GEN 18:19 | Kwa kuwa nimemchagua ili awaelekeze wanawe na nyumba yake baada yake waishike njia ya Yahwe, watende utakatifu na haki, ili kwamba Yahwe ampatie Abraham yale aliyo yasema kwake.” |
446 | GEN 18:21 | sasa nitashuka pale na kuona kilio kilicho nifikia dhidi yake, ikiwa kweli wamefanya au hawakufanya, nitajua.” |
450 | GEN 18:25 | Hasha usifanye hivyo, kuwauwa watakatifu pamoja na waovu, ili kwamba watakatifu watendewe sawa na waovu. Hasha! Je muhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?” |
451 | GEN 18:26 | Yahwe akasema, “Katika Sodoma nikipata watakatifu hamsini kwenye mji, nita uacha mji wote kwa ajili ya hao.” |
453 | GEN 18:28 | Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?” Akasema, “Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale.” |
454 | GEN 18:29 | Akaongea naye tena, na kusema, “Itakuwaje ikiwa arobaini watapatikana pale?” Akajibu, “Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.” |
455 | GEN 18:30 | Akasema, Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale.” Akajibu, 'Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale.” |
456 | GEN 18:31 | Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.” |
457 | GEN 18:32 | Akasema, “Tafadhali usikasirike, Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule.” Na akasema, sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi.” |
460 | GEN 19:2 | Akasema, Tafadhari Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke.” Nao wakasema, “Hapana, usiku tutalala mjini.” |