110 | GEN 5:4 | Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake. |
113 | GEN 5:7 | Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake. |
116 | GEN 5:10 | Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake. |
119 | GEN 5:13 | Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake. |
122 | GEN 5:16 | Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake. |
125 | GEN 5:19 | Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake. |
132 | GEN 5:26 | Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake. |
138 | GEN 5:32 | Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi. |
234 | GEN 9:28 | Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka miatatu na hamsini. |
245 | GEN 10:10 | Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari. |
253 | GEN 10:18 | Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa. |
276 | GEN 11:9 | Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote. |
293 | GEN 11:26 | Baada ya Tera kuishi miaka sabini, akamzaa Abram, Nahori, na Haran. |
307 | GEN 12:8 | Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe. |
322 | GEN 13:3 | Aliendelea na safari yake kutoka Negebu hadi Betheli, mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo, kati ya Betheli na mji wa Ai. |
339 | GEN 14:2 | walifanya vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha, mfalme wa Gomora, Shinabu, mfalme wa Adma, Shemeberi, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela(pia ikiitwa Soari). |
345 | GEN 14:8 | Kisha mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari) walikwenda na kuandaa vita |
354 | GEN 14:17 | Baada ya Abram kurudi kutoka kumpiga Kadorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae, mfalme wa Sodoma akatoka kuonana nae katika bonde la Shawe (pia iliitwa bonde la mfalme). |
362 | GEN 15:1 | Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” |
363 | GEN 15:2 | Abram akasema, “Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?” |
369 | GEN 15:8 | Akasema, “Bwana Yahwe, nitajua je kuwa nitairithi?” |
396 | GEN 16:14 | Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi. |
413 | GEN 17:15 | Mungu akamwambia Abraham, “kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara. |
428 | GEN 18:3 | Akasema, “Bwana, kama nimepata upendelea machoni pako, nakuomba usinipite na kuniacha mtumishi wako. |
452 | GEN 18:27 | Abraham akajibu na kusema, “Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu! |
455 | GEN 18:30 | Akasema, Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale.” Akajibu, 'Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale.” |
456 | GEN 18:31 | Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.” |
457 | GEN 18:32 | Akasema, “Tafadhali usikasirike, Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule.” Na akasema, sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi.” |
460 | GEN 19:2 | Akasema, Tafadhari Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke.” Nao wakasema, “Hapana, usiku tutalala mjini.” |
470 | GEN 19:12 | Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je una mtu mwingine yeyote hapa? wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa. |
489 | GEN 19:31 | Yule wa kwanza akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali popote wa kulala na sisi kulingana na desturi ya dunia yote. |
491 | GEN 19:33 | Kwa hiyo wakamnywesha baba yako mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka. |
493 | GEN 19:35 | Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule pia, na yule mdogo akaenda na akalala naye. Baba yake hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka. |
494 | GEN 19:36 | Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. |
496 | GEN 19:38 | Nayule mdogo naye akazaa mwana wa kiume, na akamwita Benami. Huyu ndiye baba wa watu wa Waamoni hata leo. |
500 | GEN 20:4 | Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, “Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki? |
510 | GEN 20:14 | Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham. |
528 | GEN 21:14 | Abraham akaamka asubuhi na mapema, akachukua mkate na kiriba cha maji, akampatia Hajiri, akiweka juu ya bega lake. Akamtoa kijana akampatia Hajiri na akawaondoa. Hajiri akaondoka akapotea katika jangwa la Beerisheba. |
545 | GEN 21:31 | Kwa hiyo akaita mahali pale Beerisheba, kwa sababu mahali pale wote wawili wali apa kiapo. |
546 | GEN 21:32 | Walifanya agano hapo Bersheba, kisha Abimeleki na Fikoli, amiri wa jeshi, wakarudi katika nchi ya Wafilisti. |
547 | GEN 21:33 | Abraham akapanda mti wa mkwaju katika Beerisheba. Na pale akamwabudu Yahwe, Mungu wa milele. |
555 | GEN 22:7 | Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “ Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” |
567 | GEN 22:19 | Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba. |
569 | GEN 22:21 | Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu, |
570 | GEN 22:22 | Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli. |
571 | GEN 22:23 | Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham. |
591 | GEN 23:19 | Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. |
593 | GEN 24:1 | Basi Abraham alikuwa mzee sana na Yahwe akawa amembariki katika mambo yote. |
607 | GEN 24:15 | Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham. |
616 | GEN 24:24 | Akamwambia, “Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori.” |
629 | GEN 24:37 | Bwana wangu aliniapisha, akisema, “Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi. |
630 | GEN 24:38 | Badala yake, lazima uende kwa familia ya baba yangu, na kwa ndugu zangu, na kupata mke kwa ajili ya mwanangu.' |
639 | GEN 24:47 | Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake. |
642 | GEN 24:50 | Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, “Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri. |
654 | GEN 24:62 | Nyakati hizo Isaka alikuwa anakaa katika Negebu, na alikuwa tu amerejea kutoka Beerlahairoi. |
670 | GEN 25:11 | Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanae, na Isaka akaishi karibu na Beerlalahairoi. |
685 | GEN 25:26 | Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto. |
694 | GEN 26:1 | Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari. |
695 | GEN 26:2 | Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, “Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia. |
701 | GEN 26:8 | Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake. |
708 | GEN 26:15 | Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwawamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kwa kuvijaza kifusi. |
716 | GEN 26:23 | Kisha Isaka akaenda Beersheba. |
726 | GEN 26:33 | Akakiita kile kisima Shiba, hivyo jina la mji ule ni Beersheba hata leo. |
727 | GEN 26:34 | Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akajitwalia mke, Yudithi binti Beeri Mhiti, na Basemathi binti Eloni Mhiti. |
733 | GEN 27:5 | Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo. |
746 | GEN 27:18 | Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, “Babangu.” Yeye akasema, “Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?” |
747 | GEN 27:19 | Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki.” |
759 | GEN 27:31 | Yeye pia akaandaa chakula kitamu na kukileta kwa baba yake. Akamwambia baba yake, “Baba, inuka na ule baadhi ya mawindo ya mwanao, ili uweze kunibariki.” |
776 | GEN 28:2 | Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako. |
779 | GEN 28:5 | Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau. |
780 | GEN 28:6 | Basi Esau alipoona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, “Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani.” |
784 | GEN 28:10 | Yakobo akatoka Beersheba na akaelekea Harani. |
793 | GEN 28:19 | Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu. |
812 | GEN 29:16 | Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli. |
825 | GEN 29:29 | Lakini pia Labani akampa Raheli binti yake Bilha, kuwa mjakazi wake. |
834 | GEN 30:3 | Akasema, “Tazama, kuna mjakazi wangu Bilha. Lala naye, hivyo aweze kuzaa watoto magotini pangu, nami nitapata watoto kwake. |
835 | GEN 30:4 | Hivyo akampa Bilha mjakazi kama mke wake, na Yakobo akalala naye. |
836 | GEN 30:5 | Bilha akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana. |
838 | GEN 30:7 | Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili. |
852 | GEN 30:21 | Baadaye akazaa binti na kumwita jina lake Dina. |
856 | GEN 30:25 | Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, “Niache niande, ili kwamba niende nyumbani kwetu na katika nchi yangu. |
875 | GEN 31:1 | Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, “Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu, na ni kutoka katika mali ya baba yetu amepata utajiri wake.” |
881 | GEN 31:7 | Baba yenu amenidanganya na amebadilisha ujira wangu mara kumi, lakini Mungu hakumruhusu kunidhuru. |
887 | GEN 31:13 | Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa. |
898 | GEN 31:24 | Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, “Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya.” |
899 | GEN 31:25 | Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi. |
902 | GEN 31:28 | Haukuniacha niwabusu wajukuu wangu na binti zangu kwa kuwaaga. Basi umefanya upumbavu. |
908 | GEN 31:34 | Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona. |
913 | GEN 31:39 | Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea. Badala yake, nilichukua upotevu huo, kwamba wameibwa mchana au usiku. |
974 | GEN 33:13 | Yakobo akamwambia, “Bwana wangu anajua kwamba watoto ni wadogo, na kwamba kondoo na ng'ombe wananyonyesha ndama wao. Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moja, wanyama wote watakufa. |
976 | GEN 33:15 | Esau akasema, haya nikuachie baadhi ya watu wangu waliopamoja nami.” Yakobo akasema, “Kwa nini kufanya hivyo? Bwana wangu amekuwa mkalimu kwangu kiasi cha kutosha.” |
982 | GEN 34:1 | Basi Dina, Binti wa Lea aliyemzalia Yakobo, akaenda kuwaona wasichana wa nchi. |