31 | GEN 1:31 | Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita. |
58 | GEN 3:2 | Mwanamke akamwambia nyoka, “Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani, |
72 | GEN 3:16 | Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.” |
102 | GEN 4:22 | Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama. |
152 | GEN 6:14 | Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje. |
154 | GEN 6:16 | Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu. |
195 | GEN 8:11 | Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi. |
197 | GEN 8:13 | Ikawa kwamba katika mwaka wa mia sita na moja, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, Tazama, uso wa nchi ulikuwa umekauka. |
200 | GEN 8:16 | “Toka nje ya safina, wewe, mke wako, wanao wa kiume, na wake wa wanao pamoja nawe. |
217 | GEN 9:11 | Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi.” |
237 | GEN 10:2 | Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi. |
238 | GEN 10:3 | Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama. |
239 | GEN 10:4 | Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu. |
273 | GEN 11:6 | Yahwe akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Hivikaribuni halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya. |
291 | GEN 11:24 | Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. |
292 | GEN 11:25 | Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
293 | GEN 11:26 | Baada ya Tera kuishi miaka sabini, akamzaa Abram, Nahori, na Haran. |
294 | GEN 11:27 | Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera alimzaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu. |
295 | GEN 11:28 | Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo. |
297 | GEN 11:30 | Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto. |
298 | GEN 11:31 | Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale. |
299 | GEN 11:32 | Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani. |
338 | GEN 14:1 | Ikiwa katika siku za Amrafeli, mfalme wa shinari, Arioko, mfalme wa Elasari, Kedorlaoma, mfalme wa Elam na Tidali, mfalme wa Goimu, |
344 | GEN 14:7 | Kisha wakarudi wakaja En Misifati (Pia ikiitwa Kadeshi), na kuishinda nchi yote ya Waamaleki, na pia Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari. |
346 | GEN 14:9 | dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafme wanne dhidi ya wale watano. |
366 | GEN 15:5 | Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa. |
384 | GEN 16:2 | Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai. |
388 | GEN 16:6 | Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka. |
393 | GEN 16:11 | Malaika wa Yahwe pia akamwambia, “ Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako. |
396 | GEN 16:14 | Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi. |
418 | GEN 17:20 | Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu. |
452 | GEN 18:27 | Abraham akajibu na kusema, “Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu! |
455 | GEN 18:30 | Akasema, Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale.” Akajibu, 'Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale.” |
456 | GEN 18:31 | Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.” |
457 | GEN 18:32 | Akasema, “Tafadhali usikasirike, Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule.” Na akasema, sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi.” |
460 | GEN 19:2 | Akasema, Tafadhari Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke.” Nao wakasema, “Hapana, usiku tutalala mjini.” |
466 | GEN 19:8 | Tazama, nina mabinti wawili ambao hawajawahi kulala na mwanaume yeyote. Nawaomba tafadhari niwalete kwenu, na muwafanyie lolote muonalo kuwa jema machoni penu. Msitende lolote kwa wanaume hawa, kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha dari yangu.” |
475 | GEN 19:17 | Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, “jiponye nafsi yako! usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali.” |
478 | GEN 19:20 | Tazama, ule mji pale uko karibu nijisalimishe pale, na ni mdogo. Tafadhari niacheni nikimbilie pale ( Je Siyo mdogo ule?), na maisha yangu yataokolewa.” |
499 | GEN 20:3 | Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.” |
511 | GEN 20:15 | Abimeleki akasema, Tazama, Nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapopendezewa.” |
512 | GEN 20:16 | Na kwa Sara akasema, Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki.” |
553 | GEN 22:5 | Abraham akawambia vijana wake, “kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu.” |
555 | GEN 22:7 | Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “ Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” |
572 | GEN 22:24 | Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka. |
576 | GEN 23:4 | “Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhari nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu.” |
578 | GEN 23:6 | “Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako.” |
587 | GEN 23:15 | “Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako.” |
605 | GEN 24:13 | Tazama, nimesimama hapa karibu na chemchemi ya maji na binti za watu wa mji wanakuja kuteka maji. |
609 | GEN 24:17 | Kisha mtumwa yule akakimbia kumlaki yule msichana, na kusema, “Tafadhari nipatie maji kidogo ya kunywa kutoka katika mtungi wako.” |
617 | GEN 24:25 | Akasema pia, “Tunayo malisho tele na chakula, na iko nafasi kwa ajili yako kulala usiku.” |
622 | GEN 24:30 | Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, “Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia,” alikwenda kwa yule mtu, na, Tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani. |
635 | GEN 24:43 | tazama niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji - na iwe kwamba binti ajaye kuchota maji, nitakaye mwambia, “Tafadhari unipatie maji kidoka kutoka kwenye mtungi wako ninywe,” mwanamke atakaye niabia, |
637 | GEN 24:45 | Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.' |
643 | GEN 24:51 | Tazama, Rebeka yu mbele yako. Mchukue na uende, ili awe mke wa mtoto wa bwana wako, kama Yahwe alivyosema.” |
649 | GEN 24:57 | Wakasema, “Tutamwita binti na kumuuliza.” |
674 | GEN 25:15 | Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi, na Kedema. |
682 | GEN 25:23 | Yahwe akamwambia, “Mataifa mawili yako katika tumbo lako, na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako. Taifa moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, na yule mkubwa atamtumikia mdogo. |
689 | GEN 25:30 | Esau akamwambia Yakobo, “Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!” Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu. |
691 | GEN 25:32 | Esau akasema, “Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?” |
701 | GEN 26:8 | Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake. |
702 | GEN 26:9 | Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, “Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?” Isaka akamwambia, “Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue.” |
721 | GEN 26:28 | Nao wakasema, “Tumeona yakini kwamba Yahwe amekuwa nawe. Hivyo tukaamua kwamba kuwe na kiapo kati yetu, ndiyo, kati yetu nawe. Hivyo na tufanye agano nawe, |
725 | GEN 26:32 | Siku hiyohiyo watumishi wake wakaja na kumwambia juu ya kisima walichokuwa wamekichimba. Wakasema, “Tumeona maji.” |
730 | GEN 27:2 | Akamwambia, “Tazama, mimi nimezeeka. Sijui siku ya kufa kwangu. |
734 | GEN 27:6 | Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, “Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema, |
739 | GEN 27:11 | Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Tazama, Ndugu yangu Esau ni mtu mwenye manyoya, na mimi ni mtu laini. |
755 | GEN 27:27 | Yakobo akasogea na kumbusu, naye akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki. Akasema, “Tazama, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilolibariki Yahwe. |
765 | GEN 27:37 | Isaka akajibu na kumwambia Esau, “Tazama, nimemfanya kuwa bwana wako, na nimempa ndugu zake kuwa watumishi wake. Na nimempa nafaka na divai. Je nikufanyie nini mwanangu? |
767 | GEN 27:39 | Isaka baba yake akajibu na kumwambia, “Tazama, mahali unapoishi patakuwa mbali na utajiri wa nchi, mbali na umande juu angani. |
770 | GEN 27:42 | Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa. Hivyo akatuma na kumwita Yakobo mwanawe mdogo na kumwambia, “Tazama, Esau ndugu yako anajifariji juu yako kwa kupanga kukuuwa. |
787 | GEN 28:13 | Tazama, Yahwe amesimama juu yake na kusema, “Mimi ni Yahwe, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi uliyolala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. |
789 | GEN 28:15 | Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi.” |
800 | GEN 29:4 | Yakobo akawambia, “Ndugu zangu, ninyi mnatokea wapi?” nao wakasema, “Tunatoka Harani.” |
801 | GEN 29:5 | Akawambia, “Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?” Wakasema, “Tunamfahamu.” |
803 | GEN 29:7 | Yakobo akasema, “Tazama, ni mchana. Siyo wakati wa kukusanya kondoo pamoja. Mnapaswa kuwanywesha kondoo na kisha mkaenda na kuwaacha wachunge.” |
823 | GEN 29:27 | Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba.” |
834 | GEN 30:3 | Akasema, “Tazama, kuna mjakazi wangu Bilha. Lala naye, hivyo aweze kuzaa watoto magotini pangu, nami nitapata watoto kwake. |
859 | GEN 30:28 | Kisha akasema, “Taja ujira wako, nami nitalipa.” |
925 | GEN 31:51 | Labani akamwambia Yakobo, Tazama rundo hili, na tazama nguzo, nililoliweka kati yako nami. |
935 | GEN 32:7 | Wajumbe wakarudi kwa Yakobo na kusema, “Tulikwenda kwa Esau ndugu yako. Anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye.” |
940 | GEN 32:12 | Tafadhari niokoe kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau, kwa maana namwogopa, kwamba atakuja na kunishambulia mimi na wamama na watoto. |
945 | GEN 32:17 | Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake. Akawambia watumishi, “Tangulieni mbele yangu na mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama.” |
958 | GEN 32:30 | Yakobo akamwambia, “Tafadhari niambie jina lako.” Akasema, “Kwa nini kuniuliza jina langu?” Kisha akambariki pale. |
970 | GEN 33:9 | Esau akasema, “Ninayo ya kutosha, ndugu yangu. Tunza uliyonayo kwa ajili yako mwenyewe.” |
972 | GEN 33:11 | Tafadhari pokea zawadi yangu uliyoletewa, kwa sababu Mungu amenitendea kwa neema, na kwa sababu ninavyo vya kutosha.” Hivyo Yakobo akamsihi, na Esau akamkubali. |
975 | GEN 33:14 | Tafadhari bwana wangu na amtangulie mtumishi wake. Nitasafiri polopole, kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu, na kadili ya watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.” |
989 | GEN 34:8 | Hamori akaongea nao, akisema, “Shekemu mwanangu anampenda binti yenu. Tafadhari mpeni kuwa mke wake. |
1023 | GEN 35:11 | Mungu akamwambia, “Mimi ni Mungu Mwenyezi, Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka. Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako. |
1052 | GEN 36:11 | Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi. |
1053 | GEN 36:12 | Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau. |
1056 | GEN 36:15 | Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora, |
1063 | GEN 36:22 | Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani. |
1081 | GEN 36:40 | Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi, |
1083 | GEN 36:42 | Kenazi, Temani, Mbza, |
1090 | GEN 37:6 | Aliwambia, “Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota. |