92 | GEN 4:12 | Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.” |
156 | GEN 6:18 | Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao. |
222 | GEN 9:16 | Upinde wa mvua utakuwa katika mawingu na nitauona, ili kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na kila kiumbe hai cha wote wenye mwili ambacho kiko juu ya nchi.” |
247 | GEN 10:12 | na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa. |
258 | GEN 10:23 | Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi. |
262 | GEN 10:27 | Hadoram, Uzali, Dikla, |
295 | GEN 11:28 | Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo. |
298 | GEN 11:31 | Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale. |
362 | GEN 15:1 | Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” |
368 | GEN 15:7 | Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi.” |
374 | GEN 15:13 | Kisha Yahwe akamwambia Abram, “Ujuwe kwa hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si ya kwao, na watatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne. |
399 | GEN 17:1 | Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu. |
402 | GEN 17:4 | “Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi. |
505 | GEN 20:9 | Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, “Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa.” |
526 | GEN 21:12 | Lakini Mungu akamwambia Abraham, “Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa. |
531 | GEN 21:17 | Mungu akasikia kilio cha kijana, na malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, “Nini kinakusumbua? Usiogope, kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha kijana mahali alipo. |
569 | GEN 22:21 | Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu, |
629 | GEN 24:37 | Bwana wangu aliniapisha, akisema, “Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi. |
683 | GEN 25:24 | Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake. |
695 | GEN 26:2 | Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, “Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia. |
717 | GEN 26:24 | Yahwe akamtokea usiku huohuo na akasema, “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi nipo pamoja nawe na nitakubariki na kuvidisha vizazi vyako, kwa ajili ya mtumishi wangu Ibrahimu.” |
732 | GEN 27:4 | Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo, uniletee ili nikile na kukubariki kabla sijafa. |
738 | GEN 27:10 | Utakipeleka kwa baba yako, ili kwamba akile, na kukubariki kabla hajafa.” |
746 | GEN 27:18 | Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, “Babangu.” Yeye akasema, “Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?” |
757 | GEN 27:29 | Watu na wakutumikie na mataifa yainame chini yako. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wainame chini yako. Kila anayekulaani na alaaniwe; na kila anayekubariki abarikiwe.” |
760 | GEN 27:32 | Isaka baba yake akamwambia, “U nani wewe? Akasema, “Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.” |
762 | GEN 27:34 | Esau aliposikia maneno ya baba yake, akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana, na akamwambia baba yake, “Unibariki nami, mimi pia, babangu.” |
772 | GEN 27:44 | Ukae naye kitambo, mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua, |
775 | GEN 28:1 | Isaka akamwita Yakobo, akambariki, na kumwagiza, “Usichukuwe mwanamke katika wanawake wa Kikanaani. |
780 | GEN 28:6 | Basi Esau alipoona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, “Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani.” |
788 | GEN 28:14 | Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi, na utaenea mbali kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini. Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa. |
860 | GEN 30:29 | Yakobo akamwambia, “Unajua nilivyokutumikia, na jinsi ambavyo mifugo wako wamekuwa nami. |
862 | GEN 30:31 | Hivyo Labani akasema, “Je nikulipe nini? Yakobo akasema, 'Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza. |
864 | GEN 30:33 | Uadilifu wangu utashuhudia kwa ajili yangu hapo baadaye, utakapokuja kuangalia ujira wangu. Kila ambaye hana milia na hana madoa miongoni mwa mbuzi, na mweusi kati ya kondoo, ikiwa wataonekana kwangu, watahesabiwa kuwa wameibwa.” |
898 | GEN 31:24 | Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, “Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya.” |
900 | GEN 31:26 | Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita? |
909 | GEN 31:35 | Akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu, kwamba siwezi kusimama mbele yako, kwani nipo katika kipindi changu.” Hivyo akatafuta lakini hakuiona miungu ya nyumbani mwake. |
911 | GEN 31:37 | Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili. |
915 | GEN 31:41 | Miaka hii ishirini nimekuwa katika nyumba yako. Nilikufanyia kazi miaka kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya wanyama wako. Umebadili ujira wangu mara kumi. |
969 | GEN 33:8 | Esau akasema, Unamaanisha nini kwa makundi haya yote niliyokutana nayo?” Yakobo akasema, “Kutafuta kibali mbele za bwana wangu. |
1013 | GEN 35:1 | Mungu akamwambia Yakobo, “Inuka, panda kwenda Betheli, na ukae pale. Unijengee madhabahu pale, niliyekutokea pale ulipomkimbia Esau kaka yako.” |
1023 | GEN 35:11 | Mungu akamwambia, “Mimi ni Mungu Mwenyezi, Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka. Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako. |
1029 | GEN 35:17 | Akawa na utungu mzito. Alipokuwa katika utungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume.” |
1069 | GEN 36:28 | Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani. |
1099 | GEN 37:15 | Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni. Yule mtu akamwuliza, “Unatafuta nini?” |
1131 | GEN 38:11 | Kisha Yuda akamwambia Tamari, mkwewe, “Ukakae mjane katika nyumb aya baba yako hadi Shela, mwanangu, atakapokuwa.” Kwani aliogopa, “Asije akafa pia, kama nduguze.” Tamari akaondoka na kuishi katika nyumba ya babaye. |
1136 | GEN 38:16 | Akamwendea kando ya njia na kusema, “Njoo, tafadhari uniruhusu kulala nawe” - kwani hakujua kwamba alikuwa ni mkwewe - naye akasema, “Utanipa nini ili ulale nami? |
1149 | GEN 38:29 | Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka kwanza. Mkunga akasema, “Umetokaje” Na akaitwa Peresi. |
1183 | GEN 40:10 | Na kulikuwa na matawi matatu katika mzabibu huo. Ulipochipua, ukachanua maua na kuzaa vichala vya zabibu. |
1186 | GEN 40:13 | Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake. |
1187 | GEN 40:14 | Lakini unikumbuke ukifanikiwa, na unionesha wema. Unitaje kwa Farao na kuniondoa hapa gerezani. |
1227 | GEN 41:31 | Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana. |
1233 | GEN 41:37 | Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote. |
1236 | GEN 41:40 | Utakuwa juu ya nyumba yangu, watu wangu watatawaliwa kwa kadili ya neno lako. Katika kiti cha enzi peke yake mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe.” |
1290 | GEN 42:37 | Rubeni akamwambia baba yake, kusema, “Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha Benjamini kwako. Mweke mikononi mwangu, nami nitamrudisha tena kwako.” |
1300 | GEN 43:9 | Mimi nitakuwa mdhamini wake. Utaniwajibisha mimi. Kama nisipomleta na kumweka mbele yako, basi nibebe lawama daima. |
1327 | GEN 44:2 | Uweke kikombe changu, cha fedha, katika mdomo wa gunia la mdogo, na pesa yake ya chakula pia.” Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyosema. |
1369 | GEN 45:10 | Utaishi katika nchi ya Gosheni, nawe utakuwa karibu nami, wewe na watoto wako na watoto wa watoto wako, na kondoo wako na mbuzi wako, na yote uliyonayo. |
1390 | GEN 46:3 | Akasema, “Mimi hapa.” Akasema, “Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko. |
1429 | GEN 47:8 | Farao akamwambia Yakobo, “Umeishi kwa muda gani?” |
1440 | GEN 47:19 | Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu. |
1446 | GEN 47:25 | Wakasema, “Umeokoa maisha yetu. Na tupate kibali machoni pako. Tutakuwa watumishi wa Farao.” |
1470 | GEN 48:18 | Yusufu akamwambia baba yake, “Sivyo babangu; kwani huyu ndiye mzaliwa wa kwanza. Uweke mkono wako juu ya kichwa chake.” |
1512 | GEN 50:5 | 'Baba yangu aliniapisha, kusema, “Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika.” Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi.” |
1569 | EXO 2:14 | Lakini yule mtu alisema, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi juu yetu? Unataka kuniua na mimi kama ulivyomuua yule mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kusema, “Hakika niliyoyafanya yamejulikana.” |
1585 | EXO 3:5 | Mungu akasema, “Usinikaribie! Vua viatu katika miguu yako, kwa kuwa mahali uliposimama ni mahali palipowekwa wakfu kwa ajili yangu.” |
1592 | EXO 3:12 | Mungu akamjibu, “Hakika nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako ya kuwa nimekutuma. Utakapokuwa umewatoa watu kutoka Misri, mtaniabubu mimi katika mlima huu.” |
1619 | EXO 4:17 | Utachukua hii fimbo pamoja nawe mkononi mwako. Kwa fimbo hii utafanya ishara.” |
1623 | EXO 4:21 | Yahwe akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, jitahidi kufanya ishara zote nilizokupa kufanya mbele ya Farao. Lakini nitaufanya moyo wake kuwa mgumu, naye hawatawaacha watu waende. |
1657 | EXO 6:1 | Kisha Yahweh akasema na Musa, “Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, ata waondoa nje ya nchi.” |
1678 | EXO 6:22 | Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri. |
1688 | EXO 7:2 | Utasema kila kitu nitacho kuamuru kusema. Aruni kaka yako ata sema na Farao iliawaachie watu wa Israeli watoke kwenye nchi yake. |
1713 | EXO 7:27 | Ukikataa kuwaruhusu waende, nitaidhuru nchi yako yote kwa vyura. |
1720 | EXO 8:5 | Musa akamwambia Farao, “Unaweza chukuwa fursa ya kuniambia lini nikuombee wewe, watumishi wako, na watu wako, ili vyura waondolewe kwako na nyumbani kwako na wabaki tu kwenye mito.” |
1728 | EXO 8:13 | Wakanya hivyo: Aruni akanyoosha mkono wake na gongo lake. Akaupiga udongo wa ardhi. Chawa wakaja juu ya watu na wanyama. Udongo wote kwenye ardhi ukawa chawa katika nchi ya Misri. |
1731 | EXO 8:16 | Yahweh akamwambia Musa, “Inuka asubui mapema na usimame mbele ya Farao anapoenda mtoni. Umwambie, 'Yahweh anasema hivi: “Acha watu wangu waende wakaniabudu mimi. |
1822 | EXO 12:5 | Mwana kondoo wako au mbuzi wako mdogo lazima asiwe na upungufu, dume mwenye mwaka mmoja. Unaweza kuchukuwa mmoja wa kondoo au mbuzi. |
1826 | EXO 12:9 | Usiile mbichi au imechemshwa kwenye maji. Badala yake, choma kwenye moto na kichwa chake, miguu na sehemu za ndani. |
1827 | EXO 12:10 | Usiache ata kidogo kubaki mpaka asubui. Lazima uchome chochote kilicho baki asubui. |
1832 | EXO 12:15 | Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli. |
1834 | EXO 12:17 | Lazima uadhimishe hii Sherehe ya Mkate Usiotiwa Chachu kwasababu ni siku hii ambayo nitawaleta watu wako, makundi yaliyo na silaha, kwa makundi yaliyo na silaha, kutoka nchi ya Misri. Lazima uadhimishe hii siku kwa vizazi vyote vya watu wako. Hii itakuwa sheria kwako. |
1842 | EXO 12:25 | Utakapo ingia nchi Yahweh atakayo kupa, kama alivyo ahidi kufanya, lazima uadhimishe hili tendo la ibada. |
1856 | EXO 12:39 | Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira walio utoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula. |
1889 | EXO 13:21 | Yahweh alitangulia mbele yao mchana kama nguzo ya wingu kuwaongoza njiani. Usiku alienda kama nguzo ya moto kuwapa mwanga. Kwa namna hii waliweza kusafiri mchana na usiku. |
1902 | EXO 14:12 | Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, 'Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.' Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani.” |
1928 | EXO 15:7 | Kwa utukufu mkubwa umewapindua walio inuka dhidi yako. Umetuma gadhabu; imewateketeza kama karatasi. |
1933 | EXO 15:12 | Ulinyoosha mkono wako wa kulia, na dunia ikawameza. |
1938 | EXO 15:17 | Utawaleta na kuwapanda kwenye mlima wa urithi wako, sehemu, Yahweh, ulio jenga ya kuishi, sehemu takatifu, Bwana wetu, mikono yako iliyo jenga. |
1956 | EXO 16:8 | Musa pia akasema, “Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa tele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayo tamka dhidi yake. Nani ni Aruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh.” |
1962 | EXO 16:14 | Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyo ganda kwenye ardhi. |
2017 | EXO 18:17 | Baba mkwe wake Musa alimwambia, “Unachofanya sicho kizuri sana. |
2023 | EXO 18:23 | Ukifanya hivi, na kama Mungu akikuamuru kufanya al kadhalika, basi utaweza kuvumilia, na watu wote watarudi nyumbani wameridhika.” |
2031 | EXO 19:4 | Uliona nilicho fanya kwa Wamisri, jinsi nilivyo kubeba kwa mabawa ya tai na kukuleta kwangu. |
2033 | EXO 19:6 | Utakuwa ufalme wa kikuhani na taifa takatifu langu. Haya ni maneno wapaswa kuwaambia Waisraeli. |
2039 | EXO 19:12 | Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, 'Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakaye shika mlima ata uawa.' |
2059 | EXO 20:7 | Usilitaje bure jina la Yahweh Mungu wako, sitkuwa na hatia kwa yeyote atakaye taja jina langu bure. |
2065 | EXO 20:13 | Usiue. |
2066 | EXO 20:14 | Usifanye uasherati (usizini). |