29 | GEN 1:29 | Mungu akasema, “tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu. |
175 | GEN 7:15 | Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina. |
181 | GEN 7:21 | Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu. |
182 | GEN 7:22 | Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa. |
183 | GEN 7:23 | Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa mchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia. |
208 | GEN 9:2 | Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai juu ya nchi, juu ya kila ndege wa angani, juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi, na juu ya samaki wote wa baharini. Vimetolewa katika mikono yenu. |
686 | GEN 25:27 | Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema. |
911 | GEN 31:37 | Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili. |
1191 | GEN 40:18 | Yusufu akajibu na kusema, “Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu. |
1494 | GEN 49:20 | Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme. |
1516 | GEN 50:9 | Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu. |
1585 | EXO 3:5 | Mungu akasema, “Usinikaribie! Vua viatu katika miguu yako, kwa kuwa mahali uliposimama ni mahali palipowekwa wakfu kwa ajili yangu.” |
1616 | EXO 4:14 | Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha. |
1715 | EXO 7:29 | Vyura watakushambulia wewe, watu wako, na watumishi wako wote."”' |
1722 | EXO 8:7 | Vyura wataondoka kutoka kwako, nyumbani mwako, kwa watumishi wako, na kwa watu wako. Watabaki tu kwenye mito.” |
1724 | EXO 8:9 | Yahweh akafanya kama Musa alivyo omba: Vyura wakafa kwenye nyumba, nyuani, na mashambani. |
1970 | EXO 16:22 | siku ya sita walikusanya mkate mara mbili zaidi, lita mbili kwa kila mtu. Viongozi wote wa jamii walikuja na kumwambia hili kwa Musa. |
1971 | EXO 16:23 | Aliwaambia, “Hili ndilo Yahweh alililo lisema: 'Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyo baki, jihifadhie hadi asubui.”' |
2223 | EXO 25:27 | Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza. |
2225 | EXO 25:29 | Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi. |
2229 | EXO 25:33 | Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara. |
2240 | EXO 26:4 | Lazima ufanye tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake. Vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili. |
2255 | EXO 26:19 | Lazima nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile fremu ishirini. Vitako viwili chini ya fremu moja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya fremu nyingine kupokea zile ndimi zake mbili. |
2261 | EXO 26:25 | Fremu zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha. Vitako kumi na sita, vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili. |
2276 | EXO 27:3 | Lazima vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake. Vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba. |
2292 | EXO 27:19 | Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba. |
2314 | EXO 28:20 | Na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi. Vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake. |
2559 | EXO 35:27 | Viongozi walileta mawe ya shohamu na mawe mengine kwaajili ya kuwekwa kwenye hiyo naivera na hicho kifuko cha kifuani; |
2576 | EXO 36:9 | Urefu wa kila pazia ulikuwa mikono ishirini na nane, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa vyote hivyo vilikuwa na kipimo kimoja. |
2581 | EXO 36:14 | Bezaleli akafanya vitambaa vya mahema vya manyoya ya mbuzi kwa ajili ya hema lililo juu ya maskani. Vitambaa kumi na moja ndivyo alivyofanyiza. |
2582 | EXO 36:15 | Urefu wa kila kitambaa ulikuwa mikono thelathini, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa hivyo kumi na moja vilikuwa na kipimo kimoja. |
2593 | EXO 36:26 | na vikalio vyake arobaini vya fedha. Vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kiunzi kingine |
2624 | EXO 37:19 | Vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kikundi kimoja cha matawi, vifundo na maua yakifuatana; na vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kile kikundi kingine cha matawi, vifundo na maua yakifuatana. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa yale matawi sita yaliyokuwa yakitoka katika kile kinara cha taa. |
2627 | EXO 37:22 | Vifundo vyake na matawi yake vilitoka kwake, vyote vilikuwa kitu kimoja cha kazi ya kufua, cha dhahabu safi. |
2637 | EXO 38:3 | Baada ya hilo akavifanya vyombo vyote vya madhabahu, yale makopo na zile sepetu na yale mabakuli, zile nyuma na vile vyetezo. Vyombo vyake vyote alivifanya kwa shaba. |
2651 | EXO 38:17 | Navyo vikalio vya nguzo vilikuwa vya shaba. Vibanio vya vikalio na viungo vyake vilikuwa vya fedha navyo vilifunikwa kwa shaba sehemu ya juu, na kulikuwa na viungo vya shaba kwa ajili ya nguzo zote za ua. |
2661 | EXO 38:27 | Na talanta mia moja za fedha zilitumiwa kutengeneza vikalio vya mahali patakatifu na vikalio vya lile pazia. Vikalio mia moja vilitoshana na talanta mia moja, talanta moja kwa kikalio kimoja. |
3032 | LEV 11:34 | Vyakula vyote ambavyo ni safi na kilichuhusiwa kuliwa, lakini kikaingiwa na maji kutoka kwenye chungu najisi kilichoanguka, nacho kitakuwa najisi. |
3111 | LEV 13:58 | Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi. |
3574 | LEV 27:3 | Viwango vyenu vya thamani kwa mwanaume aliye na umri kati ya miaka ishirini na miaka sitini yaweza kuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na vipimo vya shekeli ya mahali pa patakatifu. |
3758 | NUM 4:14 | Watavieka kwenye miti ya kubebea vyombo vyote wanavyovitumia kwa kazi ya madhabahuni. Vyombo hivi ni vyetezo, majembe, mabakuli na vitu vingine vya madhabahuni. Wataifuniks madhabahu na ngozi za pomboo na kuweka ile miti ya kubebea. |
3861 | NUM 7:10 | Viongozi walitoa bidhaa zo zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo. |
3864 | NUM 7:13 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3870 | NUM 7:19 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga. |
3882 | NUM 7:31 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3888 | NUM 7:37 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli mojala fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3894 | NUM 7:43 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga. |
3900 | NUM 7:49 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3906 | NUM 7:55 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3912 | NUM 7:61 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja yafedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3918 | NUM 7:67 | Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3924 | NUM 7:73 | Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabani, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3930 | NUM 7:79 | Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. |
3935 | NUM 7:84 | Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na vili vya dhahabu. |
3936 | NUM 7:85 | Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ye fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedh vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2, 400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. |
3937 | NUM 7:86 | Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120. |
4090 | NUM 13:14 | kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi; |
4233 | NUM 17:3 | Vitwae vile vyetezo vya wale waliopoteza maisha yao kwa sababu ya dhambi zao. Na vifanyike kuwa mbao za kufuliwa ili viwe vifuniko vya madhabahu. Kwa kuwa wale watu walivitoa kwangu, kwa hiyo ni vitakatifu. Vitakuwa ishara ya uwepo wangu kwa wana wa Israeli.” |
4251 | NUM 17:21 | Kwa hiyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo. |
4306 | NUM 19:16 | Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi—mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba. |
4692 | NUM 31:26 | “Vihesabu vitu vyote vilivyochukuliwa nyara, wote watu na wanyama. Wewe, Eliazari kuhani, na viongozi wa watu kufuata koo |
4718 | NUM 31:52 | Vitu vyote vya sadaka ya dhahabu ambavyo walimpa BWANA- sadaka toka kwa makamanda wa maelfu na kutoka kwa makepteni wa mamia - vilikuwa na uzito wa shekeli 16, 750. |
5414 | DEU 19:6 | Vinginevyo damu ya mlipiza kisasi atamfuata yeye aliyetoa uhai, na kwa hasira kali anampita kwa sababu ilikuwa safari ndefu. Na anampiga na kumuua, ijapokuwa mtu huyo akustahili kufa; na hata akustahili adhabu ya kifo kwa sababu hakumchukia jirani yake kabla hili halijatokea. |
5711 | DEU 30:1 | Vitu hivi vitakavyokuja juu yako, baraka na laana nilizoziweka mbele yako, na utakapozirejea akilini miongoni mwa mataifa mengine ambapo Yahwe Mungu wako kawapeleka, |
5740 | DEU 31:10 | Musa aliwaamuru na kusema, “Katika kila mwisho wa miaka saba, kwa muda uliowekwa wa kudumu kwa ajili ya kufuta madeni, katika Sikukuu ya Vibanda, |
5823 | DEU 33:11 | Bariki mali zake, Yahwe, na kubali kazi ya mikono yake. Vunja viuno vya wale wanaoinuka dhidi yake, na wale watu wanaomchukia, ili wasiinuke tena. |
5837 | DEU 33:25 | Vyuma vya mji wako na viwe chuma na shaba; kama vile siku zako zitakavyokuwa, ndivyo usalama wako utakavyokuwa. |
5951 | JOS 5:15 | Amiri wa jeshi la Yahweh akamwambia Musa, “Vua viatu vyako miguuni mwako, kwasababu sehemu uliyosimama ni takatifu.” Na Yoshua akafanya hivyo. |
5999 | JOS 7:21 | Nilichofanya ni hiki: Nilipoona miongoni mwa nyara mkoti mzuri kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu chenye uzito wa shekeli hamsini, nilivitamani na nikavichukua. Vimefichwa chini ardhini katikati ya hema langu, na fedha iko chini yake.” |
6052 | JOS 9:13 | Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwasababu ya safari ndefu.” |
6054 | JOS 9:15 | Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia. |
6060 | JOS 9:21 | Viongozi wakawaambia watu, “Waacheni waishi.” Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao. |
6084 | JOS 10:18 | Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda. |
6329 | JOS 19:6 | Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile |
6366 | JOS 19:43 | Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni, |
6476 | JOS 23:14 | Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana. |
6489 | JOS 24:11 | Mlivuka Yordani na mkafika Yeriko. Viongozi wa Yeriko waliinuka wapigane nanyi, pamoja na Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi. Niliwapa ninyi ushindi dhidi yao na niliwaweka chini ya mamlaka yenu. |
6627 | JDG 5:2 | 'Viongozi wanapoongoza mbele ya Israeli, watu wanapojitolea kupigana vita, tunamsifu Bwana! |
6716 | JDG 7:20 | Vikosi vitatu vilipiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Walikuwa na taa katika mikono yao ya kushoto na tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuwapiga. Walipiga kelele, “Upanga wa Bwana na wa Gideoni.” |
6779 | JDG 9:23 | Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu. Viongozi wa Shekemu walisaliti uaminifu waliokuwa nao kwa Abimeleki. |
6782 | JDG 9:26 | Gaali mwana wa Ebedi akenda pamoja na ndugu zake, wakavuka Shekemu. Viongozi wa Shekemu walimwamini. |
6800 | JDG 9:44 | Abimeleki na vitengo vilivyokuwa pamoja naye vilishambulia na kuzuia maingilio ya lango la mji. Vitengo vingine viwili vilishambulia wote waliokuwa katika shamba na wakawaua. |
6831 | JDG 10:18 | Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana, 'Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Yeye atakuwa kiongozi juu ya wote wanaoishi Gileadi. |
7058 | JDG 20:2 | Viongozi wa watu wote, wa kabila zote za Israeli, wakachukua nafasi zao kwenye kusanyiko la watu wa Mungu-watu 400, 000 waendao kwa miguu, ambao walikuwa tayari kupigana na upanga. |
7156 | RUT 2:5 | Ndipo Boazi akamwambia mtumishi wake aliyekuwa akiwasimamia wavunaji, “Vipi bwana huyu msichana ni wa nani?” |
7301 | 1SA 4:2 | Nao Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita dhidi ya Waisraeli. Vita ilipopamba moto, Israeli ilishindwa na Wafilisti, wakauawa watu wapatao elfu nne kwenye uwanja wa vita. |
7345 | 1SA 6:12 | Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata nija moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hwakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi. |
7510 | 1SA 13:23 | Vikosi vya Wafilisti wakatokeza katika nija ya Mikmashi. |
7873 | 1SA 25:9 | Vijana wa Daudi walipofika, walimwambia Nabali yote haya kwa niaba ya Daudi na kisha wakasubiri. |
8015 | 1SA 31:3 | Vita vikamwelemea Sauli, na wapiga upinde wakampata. Akapata maumivu makali kwa sababu yao. |
8016 | 1SA 31:4 | Kisha Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Chomoa upanga wako unichome nao. Vinginevyo, hawa wasiotahiriwa watakuja na kuninyanyasa.” Lakini mbeba silaha wake hakukubali, kwa kuwa aliogopa sana. Hivyo Sauli alichukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. |
8069 | 2SA 2:17 | Vita ikawa kali sana siku ile na Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watumishi wa Daudi. |
8097 | 2SA 3:13 | Daudi akajibu, “Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomuleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami.” |
8143 | 2SA 5:8 | Wakati huo Daudi akasema, “Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie virema na vipofu ambao ni adui wa Daudi.” Hii ndiyo maana watu husema, “Vipofu na virema wasingie katika kasri.” |
8287 | 2SA 11:25 | Kisha Daudi akamwambia mjumbe, “Mwambie hivi Yoabu, 'Usiruhusu jamba hili likuhuzunishe, kwa maana upanga huangamiza huyu kama uangamizavyo na mwingine. Vifanye vita vyako kuwa vyenye nguvu zaidi dhidi ya mji, na uuteke.' Mtie moyo Yoabu.” |
8489 | 2SA 18:8 | Vita ikaenea katika eneo lote na watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga. |
8504 | 2SA 18:23 | “Vyovyote itakavyokuwa niache niende,” Ahimaasi alijibu. Hivyo Yoabu akamjibu, “Nenda.” Ndipo Ahimaasi akakimbia kwa njia ya tambarare na akampita Mkushi. |
8611 | 2SA 22:6 | Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa. |