360 | GEN 14:23 | kwamba sitachukua uzi wala gidamu ya kiatu, au kitu chochote ambacho ni chako, 'ili kwamba usiseme, nimemfanya Abram kuwa tajiri.' |
501 | GEN 20:5 | Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.” |
507 | GEN 20:11 | Abraham akasema, “Ni kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.' |
630 | GEN 24:38 | Badala yake, lazima uende kwa familia ya baba yangu, na kwa ndugu zangu, na kupata mke kwa ajili ya mwanangu.' |
631 | GEN 24:39 | Nikamwambia bwana wangu, pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami.' |
637 | GEN 24:45 | Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.' |
638 | GEN 24:46 | Ndipo kwa haraka alipoushusha mtungi wake begani mwake na akasema, 'Kunywa, na pia nitawapatia maji ngamia wak.' Kwa hiyo nikanywa, na akawanywesha ngamia pia. |
639 | GEN 24:47 | Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake. |
735 | GEN 27:7 | 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.' |
885 | GEN 31:11 | Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.' |
903 | GEN 31:29 | Iko katika uwezo wangu kukudhuru, lakini Mungu wa baba yako alisema nami usiku wa leo na kuniambia, 'Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari.' |
1104 | GEN 37:20 | Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje.” |
1294 | GEN 43:3 | Yuda akamwambia, “Yule mtu alituonya kwa ukali, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi.' |
1345 | GEN 44:20 | Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba, ni mzee, na mwana wa uzee wake, ni mdogo. Na ndugu yake alishakufa, na yeye peke yake ndiye amebaki kwa mama yake, na baba yake anampenda.' |
1346 | GEN 44:21 | Nawe ukawambia matumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.' |
1347 | GEN 44:22 | Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi kumwacha babaye. Kwani akimwacha babaye baba yake angekufa.' |
1348 | GEN 44:23 | Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.' |
1350 | GEN 44:25 | Na baba yetu akasema, Nendeni tena, mkatununulie chakula.' |
1351 | GEN 44:26 | Nasi tukasema, “Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu atakuwa nasi, ndipo tutakaposhuka, kwani hatuwezi kuuona uso wa mtu yule mdogo wetu asipokuwa pamoja nasi.' |
1377 | GEN 45:18 | Mchukueni baba yenu na nyumba zenu mnijie. Nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.' |
1419 | GEN 46:32 | Watu hawa ni wafugaji, kwani wamekuwa watunza wanyama. Wamekuja na makundi yao ya kondoo, na mbuzi, na vyote walivyonavyo.' |
1421 | GEN 46:34 | mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa watunza wanyama tangu ujana wetu mpaka sasa, sisi, na baba zetu.' Fanyeni hivyo ili mweze kuishi katika nchi ya Gosheni, kwani kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri.” |
1456 | GEN 48:4 | kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele.' |
1595 | EXO 3:15 | Pia Mungu akamwambia Musa, “Lazima uwaambie Waisraeli, 'Yahwe, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma mimi kwenu. Hili ndio jina langu milele, na hivi ndivyo nitakavyokumbukwa na vizazi vyote.' |
1598 | EXO 3:18 | Watakusikiliza. Wewe pamoja na wazee wa Israeeli itawapasa kwenda kwa mfalme wa Misri, na imewapasa kumwambia, 'Yahwe, Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Hivyo tuache sisi twende safari ya siku tatu katika jangwa ili tupate kutoa sadaka kwa Yahwe Mungu wetu.' |
1641 | EXO 5:8 | Ingawa wanapaswa kuleta hesabu sawa ya matofali watakayotengeneza kama ilivyokuwa awali. Msipokee pungufu, kwasababu wao ni wavivu. Ndiyo maana wanapiga kelele na kusema, 'turuhusu tuende tukamtolee sadaka Mungu wetu.' |
1650 | EXO 5:17 | Lakini Farao akasema, “Ninyi ni wavivu! Wavivu ninyi! Ninyi mwasema, 'Turuhusu twende kumtolea Yahwe sadaka.' |
1814 | EXO 11:7 | Lakini ata mbwa hata bweka kwa watu wa Israeli, dhidi ya mtu au mnyama. Kwa hili utajuwa kuwa nina watendea Wamisri na Waisraeli tofauti.' |
1876 | EXO 13:8 | Hiyo siku utasema kwa watoto wako, 'Hii ni kwasababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipo taka Misri.' |
1883 | EXO 13:15 | Farao alipo kataa kwa ujeuri kutuachia twende, Yahweh aliwaua wazaliwa wa kwanza wa nchi ya Misri, wazaliwa wa kwanza wa watu na wa wanyama. Ndio sababu ninatoa dhabihu kwa Yahweh kwa kila mzaliwa wa kwanza wa kila mnyama, na pia sababu nina nunua wazaliwa wa kwanza wa wanangu tena.' |
1893 | EXO 14:3 | Farao atasema kuhusu Waisraeli, 'Wanaangaika kwenye nchi. Nyikani imewafunika.' |
1902 | EXO 14:12 | Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, 'Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.' Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani.” |
1930 | EXO 15:9 | Adui alisema, 'Nitakimbiza, nitapita, nitagawa nitakacho chukuwa; tamanio langu litatimizwa kwao; nitavuta upanga wangu; mkono wangu utawaharibu wao.' |
2039 | EXO 19:12 | Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, 'Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakaye shika mlima ata uawa.' |
2462 | EXO 32:23 | Maana waliniambia, 'Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu. Kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.' |
2486 | EXO 33:12 | Musa alisema na Yahweh, “Ona, umekuwa ukisema na mimi, 'Chukuwa watu hawa safarini,' lakini hauja niambia nani utamtuma na mimi. Umesema, 'Nina kujua kwa jina, na umepata upendeleo kwangu.' |
2949 | LEV 8:31 | Kwa hiyo Musa akawambia Aruni na wanawe, “Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyoamriwa, kusema, 'Aroni na wanawe wataila.' |
3098 | LEV 13:45 | Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, 'Najisi, najisi.' |
3245 | LEV 17:9 | na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.' |
3815 | NUM 5:22 | Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,' mwanamke alitakiwa kujibu, 'Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.' |
4038 | NUM 11:13 | Naweza kupata wapi nyama za kuwapa watu wote hawa? Wanalia mbele zangu na wanasema, 'tupe nyama tule.' |
4125 | NUM 14:16 | “Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.' |
4127 | NUM 14:18 | 'BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyovyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazao wao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.' |
4732 | NUM 32:12 | Ni Kalebu na Joshua tu ndio walionifuata kwa ukamilifu.' |
4887 | NUM 36:6 | Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.' |
4908 | DEU 1:14 | Mlinijibu na kusema, 'Jambo ulilolisema ni zuri kwetu kufanya.' |
4925 | DEU 1:31 | na pia katika jangwa, ambapo mmekwisha muona Yahwe Mungu wenu jinsi alivyowabeba, kama mtu abebavyo mtoto wake, kokote mlikoenda mpaka kufika hapa.' |
4930 | DEU 1:36 | kasoro Kalebu mwana wa Jephuneeh; yeye ataiona. Yeye nitampa nchi ambayo amekwisha kuikanyanga, na watoto wake, kwa sababu alimfuata Yahwe kwa ukamilifu.' |
4999 | DEU 3:22 | Hamtawaogopa, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye atakaoawapigania.' |
5012 | DEU 4:6 | Kwa hiyo washikilieni na kuwafanya, kwa kuwa hii ni hekima yenu na uelewa wenu mbele ya macho ya watu watakaosikia amri hizi zote na kusema, “Hakika taifa hili kubwa lina watu wa hekima na uelewa.' |
5082 | DEU 5:27 | Kwenu ninyi, mnapaswa kwenda na kusikiliza kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema; rudia kwetu kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema kwenu; tutamsikiliza na kumtii.' |
5086 | DEU 5:31 | Lakini kwenu, simama karibu nami, na nitakuambia amri zote, sheria, na maagizo ambayo mtawafundisha, ili kwamba waweze kuyashika katika nchi ambayo nitawapa kumiliki.' |
5199 | DEU 10:11 | Yahwe alisema nami, “Inuka, nenda mbele ya watu uwaongoze katika safari yao; wataingia na kumiliki nchi ambayo niliapa kwa mababu zao kuwapa.' |
5382 | DEU 17:16 | Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, 'Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.' |
5604 | DEU 27:17 | Alaaniwe mwanamume anayetoa alama ya ardhi.' Kisha watu wote na waseme, 'Amina'. |
5866 | JOS 1:13 | “Kumbukeni maneno ambayo Musa, mtumishi wa Yahweh, aliwaaagiza aliposema, 'Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi pumziko, naye awapeni ninyi nchi hii.' |
6010 | JOS 8:6 | Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, “Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.' Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali. |
6453 | JOS 22:25 | Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh. |
6589 | JDG 3:19 | Hata hivyo Ehudi mwenyewe, alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali, akageuka na kurudi, akasema, 'Nina ujumbe wa siri kwako, mfalme wangu.' Eglon akasema, 'Nyamazeni kimya!' Kwa hiyo wote waliomtumikia wakatoka kwenye chumba. |
6590 | JDG 3:20 | Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake. |
6594 | JDG 3:24 | Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, 'Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.' |
6609 | JDG 4:8 | Baraka akamwambia, 'Ikiwa utakwenda nami, nitakwenda, lakini ikiwa huendi pamoja nami, sitaenda.' |
6766 | JDG 9:10 | Miti hiyo ikamwambia mtini, 'Njoo utawale juu yetu.' |
6768 | JDG 9:12 | Miti hiyo ikamwambia mzabibu, 'Njoo utawale juu yetu.' |
6770 | JDG 9:14 | Kisha miti yote ikawaambia mchanga, 'Njoo utawale juu yetu.' |
6785 | JDG 9:29 | Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, 'liondoe nje jeshi lako lote.' |
6804 | JDG 9:48 | Abimeleki akaenda mpaka mlima wa Salmoni, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Abimeleki akachukua shoka na kukata matawi. Akaweka juu ya bega lake na kuwaagiza watu waliokuwa pamoja naye, 'Mlichoona nimekifanya fanyeni kama nilivyofanya.' |
6850 | JDG 11:19 | Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni; Israeli akamwambia, 'Tafadhali, tunaomba tupite katika nchi yako hata mahali petu.' |
6914 | JDG 14:3 | Baba yake na mama yake wakamwambia, “Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote? Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Samsoni akamwambia baba yake, “Nichukulie kwa ajili yangu, kwa maana wakati nilipomwangalia, alinipendeza.' |
6929 | JDG 14:18 | Na watu wa mji wakamwambia, siku ya saba kabla ya jua kuzama, 'Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba? ' Samsoni akawaambia, 'Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu, hamtapata jibu la kitendawili changu.' |
6934 | JDG 15:3 | Samsoni akawaambia, 'Wakati huu sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza.' |
6976 | JDG 16:25 | Walipokuwa wakisherehekea, wakasema, 'Mwite Samsoni, aje kutufurahisha.' Walimwita Samsoni nje ya jela na akawafanya wacheke. Walimsimamisha katikati ya nguzo. |
6997 | JDG 18:2 | Watu wa Dani walituma watu watano kutoka kwa idadi yote ya kabila lao, wanaume wenye ujasiri kutoka Sora na kutoka Eshtaoi, ili kukagua ardhi kwa miguu, na kuiangalia. Wakawaambia, “Nendeni mkaangalie nchi.' Wakafika nchi ya mlima wa Efraimu, kwa nyumba ya Mika wakalala huko. |
7032 | JDG 19:6 | Basi hao wawili wakaketi kula na kunywa pamoja. Kisha baba ya msichana akasema, “Tafadhali uwe tayari kukaa usiku huu na kuwa na wakati mzuri.' |
7034 | JDG 19:8 | Siku ya tano aliamka mapema kuondoka, lakini baba wa msichana akasema, 'Jitie nguvu mwenyewe, na kusubiri mpaka alasiri.' Kwa hiyo hao wawili wakala chakula. |
7158 | RUT 2:7 | Aliniambia, 'Tafadhali niruhusu kuvuna na kukusanya mabaki ya wavunaji.' Hivyo alikuja na ameendelea kuvuna toka asubuhi mpaka sasa, isipokuwa amepumzika kidogo katika nyumba.” |
7196 | RUT 4:4 | Nilifikiria kukujulisha na kukwambia, 'Inunue mbele ya hawa waliokaa hapa, na mbele ya viongozi wa watu wangu.' Ikiwa utapenda kuikomboa, ikomboe. Lakini ikiwa hauhitaji kuikomboa, uniambie, ili nijue, kwa kuwa hakuna mwingine wa kuikomboa isipokuwa wewe, na mimi ni mdogo wako.” Ndipo huyo mtu mwingine akasema, “Nitalikomboa.” |
7438 | 1SA 10:18 | Akwaambia watu wa Israeli, “Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli asemavyo: 'Niliwatoa Israeli kutoka Misri, na niliwaokoa kutoka nchi ya Wamisri, na kutoka mkono wa falme zote zilizowaonea.' |
7472 | 1SA 12:10 | Wakamlilia BWANA mkasema, 'Tumefanya dhambi, kwa sababu tumemwacha BWANA na tumewatumikia Mabaali na Mashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya maadui zetu, na tutakutumikia.' |
7499 | 1SA 13:12 | nikasema, 'Sasa Wafilisti watashuka dhidi yangu huko Gilgali, na sijaomba kibali cha BWANA.' Kwa hiyo nikajilazimisha mwenyewe kutoa sadaka ya kuteketezwa.” . |
7580 | 1SA 15:18 | BWANA alikutuma katika safari yako akisema, 'nenda na uangamize kabisa wenye dhambi, Waamaleki, na upigane dhidi yao hadi wameangamizwa.' |
7599 | 1SA 16:2 | Samweli akasema, “Jinsi gani nitaenda? Kama Sauli akisikia jambo hili, ataniua.” BWANA akasema, “chukua mtamba na useme, 'Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA.' |
7735 | 1SA 20:3 | Bado Daudi aliapa tena na akasema, “Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, 'Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.' Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.” |
7738 | 1SA 20:6 | Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, 'Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.' |
7753 | 1SA 20:21 | Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, 'Nenda utafute hiyo mishale.' Kama nitamwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue,” ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo. |
7761 | 1SA 20:29 | Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii.” |
7777 | 1SA 21:3 | Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, “Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, 'Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.' Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani. |
7852 | 1SA 24:11 | Leo macho yako yameona jinsi BWANA alivyokuweka mkononi mwangu tulipokuwa ndani ya pango. Wengine waliniambia nikuuwe, lakini nilikuacha hai. Nikasema, 'Sitanyoosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa kuwa ni masihi wa BWANA.' |
7855 | 1SA 24:14 | Kama mithali ya wazee isemavyo, 'Katika waovu hutoka uovu.' Lakini mkono wangu hautakuwa juu yako. |
7927 | 1SA 26:19 | Kwa hiyo sasa, nakusihi, bwana wangu mfalme asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama ni BWANA ndiye amekuchochea dhidi yangu, na aikubali sadaka; lakini kama ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA, maana leo wamenifukuza, nisishikamane na urithi wa BWANA; wameniambia, 'Nenda ukaabudu miungu mingine.' |
7979 | 1SA 29:9 | Akishi akajibu na kumwambia Daudi, “Najua kwamba hauna lawama mbele zangu kama alivyo malaika wa Mungu; hata hivyo, wale wakuu wa Wafilisti wamesema, Kamwe hatapanda pamoja nasi hadi vitani.' |
8032 | 2SA 1:7 | Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, 'Mimi hapa.' |
8034 | 2SA 1:9 | Akaniambia, Tafadhari simama juu yangu uniuwe, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.' |
8287 | 2SA 11:25 | Kisha Daudi akamwambia mjumbe, “Mwambie hivi Yoabu, 'Usiruhusu jamba hili likuhuzunishe, kwa maana upanga huangamiza huyu kama uangamizavyo na mwingine. Vifanye vita vyako kuwa vyenye nguvu zaidi dhidi ya mji, na uuteke.' Mtie moyo Yoabu.” |
8299 | 2SA 12:10 | Hivyo basi upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria mhiti kuwa mke wako.' |
8366 | 2SA 14:7 | Na sasa ukoo wote umeinuka juu ya mtumishi wako, wanasema, 'Mtoe aliyempiga nduguye, ili tumwue kulipe uhai wa nduguye aliyeuawa.' Na hivyo watamwangamiza mrithi. Hivyo watalizima kaa liwakalo nililobakiwa, hata kumwondolea mme wangu jina na mzao juu ya uso wa nchi.” |
8376 | 2SA 14:17 | Kisha mtumishi wako akaomba, 'Yahwe, tafadhari ruhusu neno la bwana wangu mfalme linipe msaada, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu kwa kutofautisha wema na ubaya.' Yahwe, Mungu na awe pamoja nawe.” |
8439 | 2SA 16:10 | Lakini mfalme akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya? Pengine ananilaani kwa kuwa Yahwe amemwambia, 'Mlaani Daudi.' Nani sasa awezaye kumwambia, 'Kwa nini unamlaani mfalme.” |
8461 | 2SA 17:9 | Tazama, kwa wakati huu pengine amejificha katika shimo fulani au mahali pengine. Itakuwa kwamba baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa mwanzoni mwa shambulio hata kila mtu atakayesikia atasema, mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu.' |
8493 | 2SA 18:12 | Yule mtu akamjibu Yoabu, “Hata kama ningepewa shekeli elfu za fedha hata hivyo nisingeinua mkono wangu juu ya mwana wa mfalme, kwa maana sisi sote tulimsikia mfalme akiwaagiza wewe, Abishai na Itai kusema, mtu asimguse huyo kijana Absalomu.' |