Wildebeest analysis examples for:   swh-swh1850   Word—Word    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

25408  LUK 9:38  Hapo, mtu mmoja katika lile kundi akapaaza sauti, akasema, “Mwalimu! Ninakusihi umwangalie mwanangu—mwanangu wa pekee!
25879  LUK 20:31  na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba—wote walikufa bila kuacha watoto.
25901  LUK 21:6  “Haya yote mnayoyaona—zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
26560  JHN 10:10  Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili.
26676  JHN 12:27  “Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja—ili nipite katika saa hii.
27715  ACT 20:21  Niliwaonya wote—Wayahudi kadhalika na watu wa mataifa, wamgeukie Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu.
28107  ROM 4:17  Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.” Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu alimwamini—Mungu ambaye huwapa wafu uzima, na kwa amri yake, vitu ambavyo havikuwapo huwa.
28138  ROM 6:2  Hata kidogo! Kuhusu dhambi sisi tumekufa—tutaendeleaje kuishi tena katika dhambi?
28146  ROM 6:10  Hivyo, kwa kuwa alikufa—mara moja tu—dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
28152  ROM 6:16  Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo—au watumwa wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.
28153  ROM 6:17  Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini—namshukuru Mungu—mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
28551  1CO 6:16  Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye—kama ilivyoandikwa: “Nao wawili watakuwa mwili mmoja.”
28714  1CO 12:12  Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote—ingawaje ni vingi—hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.
28801  1CO 15:15  Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua—kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.
28849  1CO 16:5  Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia—maana nataraji kupitia Makedonia.
28891  2CO 1:23  Mungu ndiye shahidi wangu—yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
28895  2CO 2:3  Ndiyo maana niliwaandikia—sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na ninyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba, mimi nikifurahi, ninyi nyote pia mnafurahi.
28897  2CO 2:5  Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi—ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
28902  2CO 2:10  Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe—kama kweli ninacho cha kusamehe—nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
29028  2CO 9:4  Isije ikawa kwamba watu wa Makedonia watakapokuja pamoja nami tukawakuta hamko tayari, hapo sisi tutaaibika—bila kutaja aibu mtakayopata ninyi wenyewe—kwa sababu tutakuwa tumewatumainia kupita kiasi.
29047  2CO 10:8  Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa—uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa—hata hivyo sijutii hata kidogo.
29078  2CO 11:21  Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu—nasema kama mtu mpumbavu—mimi nathubutu pia.
29080  2CO 11:23  Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi—nanena hayo kiwazimu—ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
29088  2CO 11:31  Mungu na Baba wa Bwana Yesu—jina lake litukuzwe milele—yeye anajua kwamba sisemi uongo.
29154  GAL 2:6  Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi—kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje—watu hawa hawakuwa na kitu cha kuongeza katika Habari hii Njema kama niihubirivyo.
29239  GAL 5:10  Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni—awe nani au nani—hakika ataadhibiwa.
29271  GAL 6:16  Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli—Wateule wa Mungu.
29711  1TH 5:23  Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu—roho, mioyo na miili yenu—mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
29780  1TI 1:17  Kwake yeye aliye Mfalme wa milele na asiyekufa, yeye aliye Mungu pekee—kwake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina.
30066  HEB 3:4  Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani—na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
30393  JAS 3:7  Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote—wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini.
30586  2PE 2:19  Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu—maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.
30601  2PE 3:12  mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi—Siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
30639  1JN 2:22  Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha. Mtu wa namna hiyo ni adui wa Kristo—anamkana Baba na Mwana.
30711  1JN 5:20  Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli—katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uzima wa milele.
30860  REV 5:13  Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini—viumbe vyote ulimwenguni—vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele.”
31003  REV 14:8  Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake—divai kali ya uzinzi wake!”
31109  REV 20:2  Akalikamata lile joka—nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani—akalifunga kwa muda wa miaka elfu moja.