26 | GEN 1:26 | Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.” |
29 | GEN 1:29 | Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. |
30 | GEN 1:30 | Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo. |
49 | GEN 2:18 | Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” |
57 | GEN 3:1 | Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?” |
63 | GEN 3:7 | Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. |
64 | GEN 3:8 | Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. |
66 | GEN 3:10 | Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” |
67 | GEN 3:11 | Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?” |
69 | GEN 3:13 | Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.” |
71 | GEN 3:15 | Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.” |
72 | GEN 3:16 | Kwa mwanamke akasema, “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto. Tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.” |
89 | GEN 4:9 | Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?” Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” |
94 | GEN 4:14 | Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.” |
96 | GEN 4:16 | Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni. |
102 | GEN 4:22 | Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. |
103 | GEN 4:23 | Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza. |
106 | GEN 4:26 | Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi. Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Bwana. |
135 | GEN 5:29 | Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.” |
136 | GEN 5:30 | Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. |
138 | GEN 5:32 | Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi. |
141 | GEN 6:3 | Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.” |
145 | GEN 6:7 | Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” |
146 | GEN 6:8 | Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana. |
147 | GEN 6:9 | Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. |
148 | GEN 6:10 | Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. |
151 | GEN 6:13 | Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. |
155 | GEN 6:17 | Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia. |
160 | GEN 6:22 | Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru. |
161 | GEN 7:1 | Ndipo Bwana akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. |
165 | GEN 7:5 | Noa akafanya yote kama Bwana alivyomwamuru. |
166 | GEN 7:6 | Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. |
167 | GEN 7:7 | Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. |
169 | GEN 7:9 | wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa. |
171 | GEN 7:11 | Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. |
173 | GEN 7:13 | Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. |
174 | GEN 7:14 | Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. |
175 | GEN 7:15 | Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina. |
176 | GEN 7:16 | Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo Bwana akamfungia ndani. |
181 | GEN 7:21 | Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. |
183 | GEN 7:23 | Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. |
185 | GEN 8:1 | Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. |
190 | GEN 8:6 | Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina |
193 | GEN 8:9 | Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. |
194 | GEN 8:10 | Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. |
195 | GEN 8:11 | Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. |
196 | GEN 8:12 | Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa. |
197 | GEN 8:13 | Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. |
199 | GEN 8:15 | Ndipo Mungu akamwambia Noa, |
201 | GEN 8:17 | Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.” |
202 | GEN 8:18 | Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. |
204 | GEN 8:20 | Kisha Noa akamjengea Bwana madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. |
207 | GEN 9:1 | Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia. |
211 | GEN 9:5 | Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake. |
214 | GEN 9:8 | Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye: |
216 | GEN 9:10 | pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani. |
217 | GEN 9:11 | Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.” |
219 | GEN 9:13 | Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. |
223 | GEN 9:17 | Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.” |
224 | GEN 9:18 | Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) |
225 | GEN 9:19 | Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia. |
226 | GEN 9:20 | Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. |
229 | GEN 9:23 | Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao. |
230 | GEN 9:24 | Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, |
234 | GEN 9:28 | Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350. |
235 | GEN 9:29 | Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa. |
236 | GEN 10:1 | Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. |
243 | GEN 10:8 | Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. |
244 | GEN 10:9 | Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” |
246 | GEN 10:11 | Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, |
247 | GEN 10:12 | na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa. |
265 | GEN 10:30 | Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki. |
267 | GEN 10:32 | Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika. |
270 | GEN 11:3 | Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. |
271 | GEN 11:4 | Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” |
274 | GEN 11:7 | Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” |
276 | GEN 11:9 | Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote. |
289 | GEN 11:22 | Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. |
290 | GEN 11:23 | Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. |
291 | GEN 11:24 | Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. |
292 | GEN 11:25 | Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. |
293 | GEN 11:26 | Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. |
294 | GEN 11:27 | Hawa ndio wazao wa Tera. Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. |
296 | GEN 11:29 | Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. |
301 | GEN 12:2 | “Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka. |
302 | GEN 12:3 | Nitawabariki wale wanaokubariki, na yeyote akulaaniye nitamlaani; na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.” |
306 | GEN 12:7 | Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa akamjengea madhabahu Bwana aliyekuwa amemtokea. |
308 | GEN 12:9 | Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. |
310 | GEN 12:11 | Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. |