Wildebeest analysis examples for:   swh-swhonen   k    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

2  GEN 1:2  Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
3  GEN 1:3  Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.
4  GEN 1:4  Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6  GEN 1:6  Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
7  GEN 1:7  Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.
8  GEN 1:8  Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.
9  GEN 1:9  Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo.
10  GEN 1:10  Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.
11  GEN 1:11  Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.
12  GEN 1:12  Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.
13  GEN 1:13  Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14  GEN 1:14  Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka,
15  GEN 1:15  nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo.
16  GEN 1:16  Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota.
17  GEN 1:17  Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia,
18  GEN 1:18  itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
19  GEN 1:19  Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.
20  GEN 1:20  Mungu akasema, Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.”
21  GEN 1:21  Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
22  GEN 1:22  Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.”
23  GEN 1:23  Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.
24  GEN 1:24  Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.