Wildebeest analysis examples for:   swh-swhonen   Word:    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

11  GEN 1:11  Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.
12  GEN 1:12  Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.
16  GEN 1:16  Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota.
24  GEN 1:24  Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.
30  GEN 1:30  Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.
37  GEN 2:6  lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:
148  GEN 6:10  Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
153  GEN 6:15  Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini.
181  GEN 7:21  Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.
201  GEN 8:17  Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”
214  GEN 9:8  Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye:
216  GEN 9:10  pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani.
217  GEN 9:11  Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”
218  GEN 9:12  Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo:
224  GEN 9:18  Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)
236  GEN 10:1  Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
237  GEN 10:2  Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
238  GEN 10:3  Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
239  GEN 10:4  Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
241  GEN 10:6  Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.
242  GEN 10:7  Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.
248  GEN 10:13  Misraimu alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
250  GEN 10:15  Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,
257  GEN 10:22  Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
258  GEN 10:23  Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
260  GEN 10:25  Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
261  GEN 10:26  Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
330  GEN 13:11  Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana:
362  GEN 15:1  Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
365  GEN 15:4  Ndipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.”
393  GEN 16:11  Pia malaika wa Bwana akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.
395  GEN 16:13  Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
402  GEN 17:4  “Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.
408  GEN 17:10  Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa.
418  GEN 17:20  Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
448  GEN 18:23  Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu?
452  GEN 18:27  Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu;
509  GEN 20:13  Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ”
568  GEN 22:20  Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana:
572  GEN 22:24  Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.
588  GEN 23:16  Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.
672  GEN 25:13  Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
736  GEN 27:8  Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia:
756  GEN 27:28  Mungu na akupe umande kutoka mbinguni na utajiri wa duniani: wingi wa nafaka na divai mpya.
764  GEN 27:36  Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?”
771  GEN 27:43  Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani.
914  GEN 31:40  Hii ndiyo iliyokuwa hali yangu: Niliumia kwa joto la mchana na baridi usiku, pia usingizi ulinipa.
933  GEN 32:5  Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema, nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwako huko mpaka sasa.
942  GEN 32:14  Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake:
1034  GEN 35:22  Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili. Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:
1035  GEN 35:23  Wana wa Lea walikuwa: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.
1036  GEN 35:24  Wana wa Raheli walikuwa: Yosefu na Benyamini.
1037  GEN 35:25  Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa: Dani na Naftali.
1038  GEN 35:26  Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa: Gadi na Asheri. Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.
1043  GEN 36:2  Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi,
1051  GEN 36:10  Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
1052  GEN 36:11  Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.
1054  GEN 36:13  Wana wa Reueli ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
1055  GEN 36:14  Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: Yeushi, Yalamu na Kora.
1056  GEN 36:15  Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi,
1058  GEN 36:17  Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
1059  GEN 36:18  Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.
1061  GEN 36:20  Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
1063  GEN 36:22  Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
1064  GEN 36:23  Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
1065  GEN 36:24  Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.
1066  GEN 36:25  Watoto wa Ana walikuwa: Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
1067  GEN 36:26  Wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
1068  GEN 36:27  Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani.
1069  GEN 36:28  Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.
1070  GEN 36:29  Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
1072  GEN 36:31  Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:
1081  GEN 36:40  Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: Timna, Alva, Yethethi,
1090  GEN 37:6  Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota:
1167  GEN 39:17  Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki.
1185  GEN 40:12  Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu.
1189  GEN 40:16  Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yosefu amefasiri ikiwa na maana nzuri, akamwambia Yosefu, “Mimi pia niliota ndoto: Kichwani mwangu kulikuwepo vikapu vitatu vya mikate.
1191  GEN 40:18  Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu.
1193  GEN 40:20  Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
1197  GEN 41:1  Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili,
1201  GEN 41:5  Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja.
1209  GEN 41:13  Nayo mambo yakawa sawa kabisa na jinsi alivyotufasiria ndoto zetu: Mimi nilirudishwa kazini mwangu na huyo mtu mwingine akaangikwa.”
1224  GEN 41:28  “Ni kama vile nilivyomwambia Farao: Mungu amemwonyesha Farao jambo analokusudia kufanya karibuni.
1267  GEN 42:14  Yosefu akawaambia, “Ni sawa kabisa kama nilivyowaambia: Ninyi ni wapelelezi!
1268  GEN 42:15  Na hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa mpaka ndugu yenu mdogo aje hapa.
1271  GEN 42:18  Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu:
1286  GEN 42:33  “Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu pamoja nami hapa, kisha nendeni mpeleke chakula kwa ajili ya jamaa yenu inayoteseka kwa njaa.
1302  GEN 43:11  Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi.
1326  GEN 44:1  Kisha Yosefu akampa yule msimamizi wa nyumbani mwake maagizo haya: “Jaza magunia ya watu hawa kiasi cha chakula ambacho wanaweza kuchukua, na uweke fedha ya kila mtu kwenye mdomo wa gunia lake.
1343  GEN 44:18  Ndipo Yuda akamwendea na kumwambia: “Tafadhali bwana wangu, mruhusu mtumishi wako aseme neno kwa bwana wangu. Usimkasirikie mtumishi wako, ingawa wewe ni sawa na Farao mwenyewe.
1368  GEN 45:9  Sasa rudini haraka kwa baba yangu na mwambieni, ‘Hili ndilo mwanao Yosefu asemalo: Mungu amenifanya mimi kuwa bwana wa Misri yote. Shuka uje kwangu, wala usikawie.
1376  GEN 45:17  Farao akamwambia Yosefu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Pakieni wanyama wenu mrudi mpaka nchi ya Kanaani,
1378  GEN 45:19  “Mnaagizwa pia kuwaambia, ‘Fanyeni hivi: Chukueni magari ya kukokotwa kutoka Misri, kwa ajili ya watoto wenu na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje.
1382  GEN 45:23  Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari.
1395  GEN 46:8  Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.
1396  GEN 46:9  Wana wa Reubeni ni: Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.
1397  GEN 46:10  Wana wa Simeoni ni: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani.
1398  GEN 46:11  Wana wa Lawi ni: Gershoni, Kohathi na Merari.
1399  GEN 46:12  Wana wa Yuda ni: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi ni: Hesroni na Hamuli.
1400  GEN 46:13  Wana wa Isakari ni: Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.