5 | GEN 1:5 | Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza. |
7 | GEN 1:7 | Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo. |
8 | GEN 1:8 | Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili. |
9 | GEN 1:9 | Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. |
11 | GEN 1:11 | Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo. |
13 | GEN 1:13 | Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu. |
15 | GEN 1:15 | Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo. |
19 | GEN 1:19 | Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne. |
23 | GEN 1:23 | Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano. |
24 | GEN 1:24 | Mungu akasema, “ nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo. |
31 | GEN 1:31 | Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita. |
70 | GEN 3:14 | Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako. |
83 | GEN 4:3 | Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe. |
98 | GEN 4:18 | Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki. |
104 | GEN 4:24 | Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.” |
139 | GEN 6:1 | Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao, |
170 | GEN 7:10 | Ikawa kwamba baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya nchi. |
190 | GEN 8:6 | Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza. |
197 | GEN 8:13 | Ikawa kwamba katika mwaka wa mia sita na moja, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, Tazama, uso wa nchi ulikuwa umekauka. |
269 | GEN 11:2 | Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale. |
272 | GEN 11:5 | Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga. |
296 | GEN 11:29 | Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska. |
313 | GEN 12:14 | Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana. |
328 | GEN 13:9 | Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.” |
336 | GEN 13:17 | Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia.” |
338 | GEN 14:1 | Ikiwa katika siku za Amrafeli, mfalme wa shinari, Arioko, mfalme wa Elasari, Kedorlaoma, mfalme wa Elam na Tidali, mfalme wa Goimu, |
384 | GEN 16:2 | Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai. |
385 | GEN 16:3 | Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake. |
393 | GEN 16:11 | Malaika wa Yahwe pia akamwambia, “ Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako. |
397 | GEN 16:15 | Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli. |
398 | GEN 16:16 | Abram alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram. |
416 | GEN 17:18 | Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!” |
417 | GEN 17:19 | Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake. |
418 | GEN 17:20 | Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu. |
419 | GEN 17:21 | Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.” |
421 | GEN 17:23 | Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema. |
423 | GEN 17:25 | Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele. |
424 | GEN 17:26 | Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo |
439 | GEN 18:14 | Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” |
443 | GEN 18:18 | Ikiwa kwa hakika Abraham atakuwa mkuu na taifa lenye nguvu, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? |
453 | GEN 18:28 | Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?” Akasema, “Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale.” |
454 | GEN 18:29 | Akaongea naye tena, na kusema, “Itakuwaje ikiwa arobaini watapatikana pale?” Akajibu, “Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.” |
492 | GEN 19:34 | Siku iliyo fuata yule wa kwanza akamwambia mdogowake, “Sikiliza, usiku wa jana nililala na baba yangu. Na tumnyweshe mvinyo usiku wa leo pia, na uingie ukalale naye. Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu.” |
517 | GEN 21:3 | Abraham akamwita jina mwanawe, ambaye alizaliwa kwake, na Sara, Isaka. |
518 | GEN 21:4 | Abraham akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. |
519 | GEN 21:5 | Abraham alikuwa na umri wa miaka mia moja wakati mwanawe Isaka anazaliwa kwake. |
522 | GEN 21:8 | Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya, na Abraham akafanya sherehe kubwa katika siku ambayo Isaka aliachishwa. |
524 | GEN 21:10 | Kwa hiyo akamwambia Abraham, “Mfukuze huyu mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake: kwa kuwa mtoto huyu wa mwanamke mtumwa hawezi kuwa mrithi pamoja na mwanangu Isaka.” |
526 | GEN 21:12 | Lakini Mungu akamwambia Abraham, “Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa. |
532 | GEN 21:18 | Inuka msimamishe mtoto, na umtie moyo; kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.” |
536 | GEN 21:22 | Ikawa kwamba katika wakati ule Abimeleki na Fikoli kamanda wa jeshi lake akamwambia Abraham, akisema, “Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo. |
549 | GEN 22:1 | Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, “Abraham!” Abraham akasema, “Mimi hapa.” |
550 | GEN 22:2 | Kisha Mungu akasema, “Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia.” |
551 | GEN 22:3 | Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia. |
553 | GEN 22:5 | Abraham akawambia vijana wake, “kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu.” |
554 | GEN 22:6 | Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja. |
555 | GEN 22:7 | Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “ Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” |
557 | GEN 22:9 | Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. |
568 | GEN 22:20 | Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, “Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori.” |
596 | GEN 24:4 | Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke.” |
597 | GEN 24:5 | Yule mtumwa wake akamwambia, “Itakuwaje ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kufuatana nami hadi katika nchi hii? Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka?” |
603 | GEN 24:11 | Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji. Ilikuwa jioni wakati ambao wanawake huenda kuchota maji. |
606 | GEN 24:14 | Na itokee hivi kwamba. Nikimwambia msichana, tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,' na akiniambia, 'Kunywa, na kwamba nitawanywesha ngamia wako pia,' huyo ndiye awe ambaye umemchagulia mtumwa wako Isaka. Kwa njia hii nitajua kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu.” |
607 | GEN 24:15 | Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham. |
637 | GEN 24:45 | Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.' |
654 | GEN 24:62 | Nyakati hizo Isaka alikuwa anakaa katika Negebu, na alikuwa tu amerejea kutoka Beerlahairoi. |
655 | GEN 24:63 | Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija! |
656 | GEN 24:64 | Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia. |
658 | GEN 24:66 | Mtumwa akamwambia Isaka mambo yote ambayo amefanya. |
659 | GEN 24:67 | Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake. |
661 | GEN 25:2 | Akamzalia Zimrani, Jokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. |
664 | GEN 25:5 | Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo. |
665 | GEN 25:6 | Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanae. |
668 | GEN 25:9 | Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre. |
670 | GEN 25:11 | Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanae, na Isaka akaishi karibu na Beerlalahairoi. |
671 | GEN 25:12 | Na sasa hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, mwana wa Abraham, ambaye Hajiri Mmisri mtumishi wake Sara, alizaa kwa Abraham. |
672 | GEN 25:13 | Haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Ishimaeli, kuanzia mzaliwa wa kwanza: Nebayothi - mzaliwa wa kwanza wa Ishimaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, |
675 | GEN 25:16 | Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao. |
676 | GEN 25:17 | Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake. |
678 | GEN 25:19 | Haya ndiyo yalikuwa matukio kumuhusu Isaka, mwana wa Abraham: Abraham alimzaa Isaka. |
679 | GEN 25:20 | Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami. |
680 | GEN 25:21 | Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba. |
685 | GEN 25:26 | Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto. |
687 | GEN 25:28 | Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo. |
694 | GEN 26:1 | Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari. |
696 | GEN 26:3 | Kaa katika nchi hii hii niliyokuambia, nami nitakuwa pamoja nawe na kukubariki; kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote, nami nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. |
698 | GEN 26:5 | Nitalifanya hili kwa sababu Ibrahimu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu.” |
699 | GEN 26:6 | Hivyo Isaka akakaa Gerari. |
701 | GEN 26:8 | Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake. |
702 | GEN 26:9 | Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, “Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?” Isaka akamwambia, “Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue.” |
705 | GEN 26:12 | Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo na kuvuna mwaka huo vipimo mia, kwa kuwa Yahwe alimbariki. |
708 | GEN 26:15 | Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwawamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kwa kuvijaza kifusi. |
709 | GEN 26:16 | Abimeleki akamwambia Isaka, “Ondoka kati yetu, kwa kuwa wewe una nguvu kuliko sisi.” |
710 | GEN 26:17 | Hivyo Isaka akaondoka pale na kukaa katika bonde la Gerari, na kuishi pale. |
711 | GEN 26:18 | Kwa mara nyingine tena Isaka akachimba visima vya maji, vilivyokuwa vimechimbwa siku za Ibrahimu baba yake. Wafilisiti walikuwa wamevizuia baada ya kufa kwake Ibrahimu. Isaka akaviita visima kwa majina aliyokuwa ameviita baba yake. |