37 | GEN 2:6 | Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi. |
48 | GEN 2:17 | Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.” |
51 | GEN 2:20 | Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye. |
98 | GEN 4:18 | Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki. |
99 | GEN 4:19 | Lameki akajitwalia wake wawili: jinala mmoja alikuwa Ada, na jina la yule mwingine alikuwa Sila. |
103 | GEN 4:23 | Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua. |
104 | GEN 4:24 | Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.” |
131 | GEN 5:25 | Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki. |
132 | GEN 5:26 | Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake. |
134 | GEN 5:28 | Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. |
136 | GEN 5:30 | Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake. |
137 | GEN 5:31 | Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki. |
146 | GEN 6:8 | Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe. |
156 | GEN 6:18 | Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao. |
210 | GEN 9:4 | Lakini msile nyama pamoja na uhai wake - yaani damu yake - ndani yake. |
211 | GEN 9:5 | Lakini kwa ajili ya damu yenu, uhai uliomo katika damu yenu nitataka malipo. Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka. Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo. |
254 | GEN 10:19 | Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha. |
257 | GEN 10:22 | Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu. |
294 | GEN 11:27 | Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera alimzaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu. |
298 | GEN 11:31 | Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale. |
303 | GEN 12:4 | Kwa hiyo Abram akaondoka kama vile Yahwe alivyo mwambia kufanya, na Lutu akaenda pamoja naye. Abram alikuwa na miaka sabini na mitano wakati alipotoka Harani. |
304 | GEN 12:5 | Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani. |
320 | GEN 13:1 | Kwa hiyo Abram akaondoka akatoka Misri na akaenda Negebu, Yeye, mke wake, na vyote alivyokuwa navyo. Lutu pia akaenda pamoja naye. |
326 | GEN 13:7 | Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo. |
327 | GEN 13:8 | Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia. |
329 | GEN 13:10 | Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora. |
330 | GEN 13:11 | Kwa hiyo Lutu akajichagulia yeye mwenyewe nchi tambarare ya Yorodani na akasafiri mashariki, na ndugu hawa wakatengana wao kwa wao. |
331 | GEN 13:12 | Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma. |
333 | GEN 13:14 | Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, “Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi. |
349 | GEN 14:12 | walipoondoka, wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake na Abram ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote. |
353 | GEN 14:16 | Kisha akarudisha mali zote, pia akamrudisha ndugu yake Lutu na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine. |
376 | GEN 15:15 | Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema. |
388 | GEN 16:6 | Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka. |
409 | GEN 17:11 | Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi. |
416 | GEN 17:18 | Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!” |
419 | GEN 17:21 | Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.” |
442 | GEN 18:17 | Lakini Yahwe akasema, Je ni mfiche Abraham kile ninacho kusudia kufanya, |
459 | GEN 19:1 | Malaika wawili wakaja Sodoma jioni, wakati ambao Lutu alikuwa amekaa langoni mwa Sodoma. Lutu akawaona, akainuka kuwalaki, na akainama uso wake chini ardhini. |
461 | GEN 19:3 | Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja nae, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala. |
462 | GEN 19:4 | Lakini kabla hawaja lala, wanaume wa mji, wa Sodoma, vijana kwa wazee wakaizunguka nyumba, wanaume wote kutoka kila kona ya mji. |
463 | GEN 19:5 | Wakamwita Lutu, na kumwambia, “Wale wanaume walioingia kwako usiku wakowapi? watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao.” |
464 | GEN 19:6 | Lutu akatoka nje na akafunga mlango. |
467 | GEN 19:9 | Wakasema, “Ondoka hapa!” Wakasema pia, huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao.” Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango. |
468 | GEN 19:10 | Lakini wale wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga mlango. |
469 | GEN 19:11 | Kisha wale wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume waliokuwa nje ya nyumba, vijana na wazee kwa pamoja, kiasi kwamba wakachoka wakati wakiutafuta mlango. |
470 | GEN 19:12 | Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je una mtu mwingine yeyote hapa? wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa. |
472 | GEN 19:14 | Lutu akatoka na akazungumza na wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake, akawambia, “Ondokeni upesi mahali hapa, kwa kuwa Yahwe anakaribia kuuangamiza mji.” Lakini kwa wakwe zake alionekana kuwa anawatania. |
473 | GEN 19:15 | Alfajiri, malaika wakamsihi Lutu, wakisema, ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili ambao wako hapa, ili kwamba usipotelee katika adhabu ya mji huu.” |
474 | GEN 19:16 | Lakini akakawia-kawia. Kwa hiyo watu wale wakamshika mkono wake, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa sababu Yahwe alimhurumia. Wakawatoa nje, na kuwaweka nje ya mji. |
476 | GEN 19:18 | Lutu akawambia, “Hapana, tafadhali bwana zangu! |
481 | GEN 19:23 | Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi wakati Lutu alipofika Soari. |
484 | GEN 19:26 | Lakini mke wa Lutu aliye kuwa nyuma yake, akatazama nyuma, na akawa nguzo ya chumvi. |
487 | GEN 19:29 | Wakati Mungu alipoharibu miji ya bondeni, Mungu akamkumbuka Abraham. Akamtoa Lutu kutoka katika maangamizi alipoangamiza miji ambayo katika hiyo Lutu aliishi. |
488 | GEN 19:30 | Lakini Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima akiwa pamoja na binti zake wawili, kwa sababu aliogopa kuishi Soari. Kwa hiyo akaishi pangoni, yeye na binti zake wawili. |
494 | GEN 19:36 | Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. |
499 | GEN 20:3 | Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.” |
503 | GEN 20:7 | Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujuwe kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika. |
508 | GEN 20:12 | Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu. |
526 | GEN 21:12 | Lakini Mungu akamwambia Abraham, “Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa. |
596 | GEN 24:4 | Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke.” |
600 | GEN 24:8 | Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari, ndipo utakuwa huru katika hiki kiapo changu. Cha muhimu tu ni kwamba usije ukamrudisha mwanangu huko.” |
621 | GEN 24:29 | Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima. |
623 | GEN 24:31 | Labani akasema, “Njoo, wewe uliye barikiwa na Yahwe. Kwa nini umesimama nje? nimekwisha andaa nyumba, pamoja na mahali kwa ajili ya ngamia.” |
625 | GEN 24:33 | Wakaandaa chakula mbele yake ale, lakini akasema, “Sitakula mpaka niseme kile ninacho paswa kusema.” Kwa hiyo Labani akmwambia, “Sema.” |
632 | GEN 24:40 | Lakini akaniambia, Yahwe, ambaye ninakwenda mbele yake, atatuma malaika wake pamoja nawe na atakufanikisha njia yako, kwamba utapata mke kwa ajili ya mwangu kutoka miongoni mwa ndugu zangu na kutoka katika ukoo wa baba yangu. |
633 | GEN 24:41 | Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu. |
641 | GEN 24:49 | Kwa hiyo, ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni. Lakini kama sivyo, niambieni, ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto.” |
642 | GEN 24:50 | Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, “Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri. |
648 | GEN 24:56 | Lakini akawambia, msinizuie, kwa kuwa Yahwe amefanikisha njia yangu. Niruhusuni niende kwa bwana wangu.” |
679 | GEN 25:20 | Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami. |
771 | GEN 27:43 | Kwa hiyo sasa, mwanangu, unisikie na kukimbilia kwa Labani, ndugu yangu, huko Harani. |
776 | GEN 28:2 | Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako. |
779 | GEN 28:5 | Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau. |
780 | GEN 28:6 | Basi Esau alipoona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, “Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani.” |
793 | GEN 28:19 | Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu. |
801 | GEN 29:5 | Akawambia, “Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?” Wakasema, “Tunamfahamu.” |
806 | GEN 29:10 | Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake. |
809 | GEN 29:13 | Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo mwana wa dada yake, akaenda kukutana naye, akamkumbatia, akambusu, na kumleta nyumbani kwake. Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote. |
810 | GEN 29:14 | Labani akamwambia, “Kwa hakika wewe ni mfupa wangu na nyama yangu.” Kisha Yakobo akakaa naye kama mwezi mmoja. |
811 | GEN 29:15 | Kisha Labani akamwambia Yakobo, “Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje? |
812 | GEN 29:16 | Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli. |
813 | GEN 29:17 | Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano. |
815 | GEN 29:19 | Labani akasema, Itakuwa vema kukupa wewe, kuliko kumpa mtu mwingine. Kaa nami.” |
817 | GEN 29:21 | Kisha Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe! |
818 | GEN 29:22 | Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe. |
819 | GEN 29:23 | Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye. |
820 | GEN 29:24 | Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea. |
821 | GEN 29:25 | Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa? |
822 | GEN 29:26 | Labani akamwambia, “Siyo utamaduni wetu kumtoa bindi mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza. |
824 | GEN 29:28 | Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. |