Wildebeest analysis examples for:   swh-swhulb   M    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

1  GEN 1:1  Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
2  GEN 1:2  Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.
3  GEN 1:3  Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru.
4  GEN 1:4  Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
6  GEN 1:6  Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.”
7  GEN 1:7  Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo.
8  GEN 1:8  Mungu akaita angambingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili.
9  GEN 1:9  Mungu akasema, maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo.
10  GEN 1:10  Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema.
11  GEN 1:11  Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo.
12  GEN 1:12  Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
14  GEN 1:14  Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
16  GEN 1:16  Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
17  GEN 1:17  Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi,
18  GEN 1:18  kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.
20  GEN 1:20  Mungu akasema, maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.”
21  GEN 1:21  Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
22  GEN 1:22  Mungu akavibariki, akisema, “zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.”
24  GEN 1:24  Mungu akasema, “ nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo.
25  GEN 1:25  Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaaho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwani vyema.
26  GEN 1:26  Mung akasema, “na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.”
27  GEN 1:27  Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba.
28  GEN 1:28  Mungu akawabariki na akawaambia, “zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,”
29  GEN 1:29  Mungu akasema, “tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.
31  GEN 1:31  Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita.
33  GEN 2:2  Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
34  GEN 2:3  Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
35  GEN 2:4  Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu.
36  GEN 2:5  Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.
38  GEN 2:7  Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.
39  GEN 2:8  Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba.
40  GEN 2:9  Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
41  GEN 2:10  Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne.
45  GEN 2:14  Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
46  GEN 2:15  Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
47  GEN 2:16  Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, “kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.
49  GEN 2:18  Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.”
50  GEN 2:19  Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.
51  GEN 2:20  Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.
52  GEN 2:21  Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.
53  GEN 2:22  Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu.
54  GEN 2:23  Mwanaume akasema, “kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume.
57  GEN 3:1  Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?”
58  GEN 3:2  Mwanamke akamwambia nyoka, “Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani,
59  GEN 3:3  lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'”
61  GEN 3:5  Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”
63  GEN 3:7  Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe.
64  GEN 3:8  Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu.
65  GEN 3:9  Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “ uko wapi?”
66  GEN 3:10  Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.”
67  GEN 3:11  Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?”
68  GEN 3:12  Mwanaume akasema, Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.”
69  GEN 3:13  Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.”
70  GEN 3:14  Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.
76  GEN 3:20  Mwanaume akaita mke wake jina Hawa kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.
77  GEN 3:21  Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha.
78  GEN 3:22  Yahwe Mungu akasema, “ sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele.”
79  GEN 3:23  Kwa hiyo Yahwe Mungu akamuondoa kutoka kwenye bustani ya Edeni, kwenda kulima ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa.
80  GEN 3:24  Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.
81  GEN 4:1  Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe.”
85  GEN 4:5  lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana.
98  GEN 4:18  Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki.
105  GEN 4:25  Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.”
106  GEN 4:26  Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe.
107  GEN 5:1  Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
108  GEN 5:2  Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
118  GEN 5:12  Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
119  GEN 5:13  Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
121  GEN 5:15  Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
122  GEN 5:16  Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
123  GEN 5:17  Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
127  GEN 5:21  Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
128  GEN 5:22  Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
130  GEN 5:24  Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
131  GEN 5:25  Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
132  GEN 5:26  Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
133  GEN 5:27  Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
140  GEN 6:2  wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.
142  GEN 6:4  Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
147  GEN 6:9  Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.
149  GEN 6:11  Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.
150  GEN 6:12  Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.
151  GEN 6:13  Mungu akamwambia Nuhu, “Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.
160  GEN 6:22  Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.
169  GEN 7:9  wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu.
172  GEN 7:12  Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.
176  GEN 7:16  Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango.
178  GEN 7:18  Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.
179  GEN 7:19  Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa.
180  GEN 7:20  Maji yakaongezeka dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima.
184  GEN 7:24  Maji haya kuzama chini ya nchi kwa muda wa siku miamoja na hamsini.
185  GEN 8:1  Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.