2 | GEN 1:2 | Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji. |
238 | GEN 10:3 | Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama. |
242 | GEN 10:7 | Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. |
246 | GEN 10:11 | Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala, |
247 | GEN 10:12 | na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa. |
285 | GEN 11:18 | Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu. |
286 | GEN 11:19 | Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumza a Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
287 | GEN 11:20 | Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na miwili, alimzaa Serugi. |
288 | GEN 11:21 | Reu aliishi miaka207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
391 | GEN 16:9 | Malaika wa Yahwe akamwambia, “ Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake.” |
571 | GEN 22:23 | Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham. |
572 | GEN 22:24 | Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka. |
607 | GEN 24:15 | Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham. |
621 | GEN 24:29 | Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima. |
622 | GEN 24:30 | Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, “Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia,” alikwenda kwa yule mtu, na, Tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani. |
637 | GEN 24:45 | Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.' |
643 | GEN 24:51 | Tazama, Rebeka yu mbele yako. Mchukue na uende, ili awe mke wa mtoto wa bwana wako, kama Yahwe alivyosema.” |
645 | GEN 24:53 | Mtumwa akaleta vipande vya fedha na vipande vya dhahabu, na nguo, akampatia Rebeka. Akampatia pia kaka yake na mama yake zawadi zenye thamani. |
650 | GEN 24:58 | Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je utakwenda na mtu huyu?” Akajibu, “Nitakwenda.” |
651 | GEN 24:59 | Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka, pamoja na watumishi wake wa kike, kwenda njiani pamoja na mtumishi wa Abraham na watu wake. |
652 | GEN 24:60 | Wakambarikia Rebeka, na wakamwambia, “Ndugu yetu, na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu, uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia.” |
653 | GEN 24:61 | Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake kwa hesabu ya ngamia, na wakamfuata yule mtu. Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao. |
656 | GEN 24:64 | Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia. |
657 | GEN 24:65 | Akamwambia mtumwa, “mtu huyo ni nani anaye tembea shambani akija kutupokea?” Mtumwa akasema, “Ni bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika. |
659 | GEN 24:67 | Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake. |
679 | GEN 25:20 | Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami. |
680 | GEN 25:21 | Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba. |
687 | GEN 25:28 | Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo. |
700 | GEN 26:7 | Watu wa eneo hilo walipomwuliza juu ya mke wake, alisema, “Yeye ni dada yangu.” Aliogopa kusema, “Yeye ni mke wangu,” kwa kuwa alidhani, “Watu wa nchi hii wataniua ili wamchukue Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa uso.” |
701 | GEN 26:8 | Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake. |
715 | GEN 26:22 | Akatoka hapo na akachimba kisima kingine, lakini hicho hawakukigombania. Hivyo akakiita Rehobothi, na akasema, “Sasa Yahwe ametufanyia nafasi, na tutafanikiwa katika nchi.” |
728 | GEN 26:35 | Wakamhuzunisha Isaka na Rebeka. |
733 | GEN 27:5 | Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo. |
734 | GEN 27:6 | Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, “Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema, |
739 | GEN 27:11 | Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Tazama, Ndugu yangu Esau ni mtu mwenye manyoya, na mimi ni mtu laini. |
743 | GEN 27:15 | Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau, mwanawe mkubwa, alizokuwa nazo nyumbani mwake, na akamvika Yakobo, mwanawe mdogo. |
770 | GEN 27:42 | Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa. Hivyo akatuma na kumwita Yakobo mwanawe mdogo na kumwambia, “Tazama, Esau ndugu yako anajifariji juu yako kwa kupanga kukuuwa. |
774 | GEN 27:46 | Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechoka na maisha kwa sababu ya hawa binti za Hethi. Ikiwa Yakobo atachukua mmojawapo wa binti wa Hethi kuwa mkewe, kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi, maisha yatakuwa na maana gani kwangu?” |
779 | GEN 28:5 | Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau. |
802 | GEN 29:6 | Akawambia, “Je hajambo?” Wakasema, “Hajambo, na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo.” |
805 | GEN 29:9 | Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga. |
806 | GEN 29:10 | Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake. |
807 | GEN 29:11 | Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti. |
808 | GEN 29:12 | Yakobo akamwambia Raheli kwamba alikuwa ni ndugu wa baba yake, na kwamba alikuwa mwana wa Rebeka. Kisha yeye akakimbia kumwambia baba yake. |
812 | GEN 29:16 | Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli. |
813 | GEN 29:17 | Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano. |
814 | GEN 29:18 | Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, “Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo.” |
816 | GEN 29:20 | Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake. |
821 | GEN 29:25 | Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa? |
824 | GEN 29:28 | Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. |
825 | GEN 29:29 | Lakini pia Labani akampa Raheli binti yake Bilha, kuwa mjakazi wake. |
826 | GEN 29:30 | Hivyo Yakobo akalala na Raheli, pia, lakini akampenda Raheli zaidi ya Lea. Hivyo Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka saba mingine. |
827 | GEN 29:31 | Yahwe akaona kwamba Lea hakupendwa, hivyo akalifungua tumbo lake, lakini Raheli hakuwa na mtoto. |
828 | GEN 29:32 | Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, “Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda.” |
832 | GEN 30:1 | Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, sivyo nitakufa.” |
833 | GEN 30:2 | Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, “Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto? |
837 | GEN 30:6 | Kisha Raheli akasema, “Mungu ameamua kwa faida yangu. Ameyasikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita jina lake Dani |
838 | GEN 30:7 | Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili. |
839 | GEN 30:8 | Raheli akasema, “Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu na kushinda.” Akamwita jina lake Naftali. |
845 | GEN 30:14 | Siku za mavuno ya ngano Rubeni akaenda shambani na kuona tunguja. Akazileta kwa mama yake. Kisha Raheli akamwambia Lea, “Nipe baadhi ya tunguja za mwanao.” |
846 | GEN 30:15 | Lea akamwambia, “Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, “Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao. |
853 | GEN 30:22 | Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba. |
856 | GEN 30:25 | Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, “Niache niande, ili kwamba niende nyumbani kwetu na katika nchi yangu. |
877 | GEN 31:3 | Kisha Yahwe akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na ya ndugu zako, nami nitakuwa nawe.” |
878 | GEN 31:4 | Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwandani katika kundi lake la kondoo |
888 | GEN 31:14 | Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, “Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu? |
893 | GEN 31:19 | Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake, Raheli akaiba miungu ya nyumba ya baba yake. |
906 | GEN 31:32 | Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi. Mbele ya ndugu zetu, onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue.” Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba. |
907 | GEN 31:33 | Labani akaingia katika hema ya Yakobo, katika hema ya Lea, na katika hema za wale wajakazi wawili, lakini hakuviona. Akatoka katika hema ya Lea na kuingia katika hema ya Raheli. |
908 | GEN 31:34 | Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona. |
922 | GEN 31:48 | Labani akasema, “Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo.” Kwa hiyo jina lake likaitwa Galedi. |
926 | GEN 31:52 | Rundo hili ni shahidi, na nguzo ni shahidi, kwamba sitapita rundo hili kuja kwako, na kwamba wewe hautapita rundo hili kuja kwangu, kwa madhara. |
938 | GEN 32:10 | Yakobo akasema, “Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe, uliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha,' |
962 | GEN 33:1 | Yakobo akainua macho yake na, tazama, Esau alikuwa anakuja, na alikuwa na watu mia nne pamoja naye. Yakobo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli, na wale wajakazi wawili. |
963 | GEN 33:2 | Kisha akawaweka wajakazi na wanao mbele, wakifuatiwa na Lea na watoto wake, Raheli na Yusufu wakafuata mwisho wa wote. |
968 | GEN 33:7 | Akafuata Lea pia na watoto wake wakaja na kusujudia. Mwisho Yusufu na Raheli wakaja na kusujudia. |
1020 | GEN 35:8 | Debora, mlezi wa Rebeka, akafa. Akazikwa chini kutoka Betheli chini ya mwaloni, hivyo ikaitwa Aloni Bakuthi. |
1028 | GEN 35:16 | Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu. |
1031 | GEN 35:19 | Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). |
1032 | GEN 35:20 | Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo. |
1034 | GEN 35:22 | Yakobo alipokuwa akiishi katika nchi hiyo, Rubeni akalala na Bilha suria wa baba yake, na Israeli akasikia kuhusu hilo. Basi Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili. |
1035 | GEN 35:23 | Wanawe kwa Lea walikuwa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni. |
1036 | GEN 35:24 | Wanawe kwa Raheli walikuwa Yusufu na Benjamini. |
1037 | GEN 35:25 | Wanawe kwa Bilha, mjakazi wa Raheli walikuwa Dani na Naftali. |
1045 | GEN 36:4 | Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli. |
1051 | GEN 36:10 | Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau. |
1054 | GEN 36:13 | Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau. |
1058 | GEN 36:17 | Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau. |
1078 | GEN 36:37 | Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake. |
1105 | GEN 37:21 | Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, “Tusiuondoe uhai wake.” |
1106 | GEN 37:22 | Rubeni aliwambia, “Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake” - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake. |
1113 | GEN 37:29 | Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake. |
1234 | GEN 41:38 | Farao akawambia watumishi wake, “Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu?” |
1275 | GEN 42:22 | Rubeni akawajibu, “Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu.” |
1290 | GEN 42:37 | Rubeni akamwambia baba yake, kusema, “Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha Benjamini kwako. Mweke mikononi mwangu, nami nitamrudisha tena kwako.” |
1395 | GEN 46:8 | Haya ni majina ya watoto wa Israeli waliokuja Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo; |
1396 | GEN 46:9 | wana wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi; |
1406 | GEN 46:19 | Wana wa Raheli mkewe Yakobo walikuwa Yusufu na Benjamini. |