33 | GEN 2:2 | Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote. |
57 | GEN 3:1 | Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?” |
82 | GEN 4:2 | Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo. |
99 | GEN 4:19 | Lameki akajitwalia wake wawili: jinala mmoja alikuwa Ada, na jina la yule mwingine alikuwa Sila. |
102 | GEN 4:22 | Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama. |
103 | GEN 4:23 | Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua. |
105 | GEN 4:25 | Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, “ Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.” |
106 | GEN 4:26 | Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe. |
109 | GEN 5:3 | Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi. |
110 | GEN 5:4 | Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake. |
112 | GEN 5:6 | Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. |
114 | GEN 5:8 | Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki. |
138 | GEN 5:32 | Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi. |
148 | GEN 6:10 | Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti. |
155 | GEN 6:17 | Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa. |
173 | GEN 7:13 | Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina. |
189 | GEN 8:5 | Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana. |
205 | GEN 8:21 | Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, “ Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya. |
224 | GEN 9:18 | Wana wa Nuhu ambao walitoka katika safina walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Na Hamu akamzaa kanaani. |
229 | GEN 9:23 | Kwa hiyo Shemu na Yafethi wakachukua kanzu wakaitanda juu ya mabega yao, na wakatembea kinyumenyume na wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zikiwa zimegeuka nyuma upande mwingine, kwa hiyo hawakuona uchi wa baba yao. |
232 | GEN 9:26 | Akasema pia, Yahwe, Mungu wa Shemu, abarikiwe, Kanaani na awe mtumwa wake. |
233 | GEN 9:27 | Mungu na apanuwe mipaka ya Yafethi, na afanye makazi yake katika hema za Shemu. Kanaani na awe mtumwa wake.” |
235 | GEN 9:29 | Siku zote za Nuhu zilikuwa ni miaka mia tisa na hamsini, na kisha alikufa. |
236 | GEN 10:1 | Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika. |
242 | GEN 10:7 | Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. |
245 | GEN 10:10 | Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari. |
250 | GEN 10:15 | Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi, |
254 | GEN 10:19 | Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha. |
256 | GEN 10:21 | Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi. |
257 | GEN 10:22 | Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu. |
259 | GEN 10:24 | Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber. |
261 | GEN 10:26 | Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, |
263 | GEN 10:28 | Obali, Abimaeli, Sheba, |
265 | GEN 10:30 | Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki. |
266 | GEN 10:31 | Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao. |
268 | GEN 11:1 | Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja. |
269 | GEN 11:2 | Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale. |
277 | GEN 11:10 | Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa miaka mia moja, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika. |
278 | GEN 11:11 | Shemu akaishi miaka miatano baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike. |
279 | GEN 11:12 | Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na mitano akamzaa Shela. |
280 | GEN 11:13 | Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
281 | GEN 11:14 | Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. |
282 | GEN 11:15 | Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
287 | GEN 11:20 | Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na miwili, alimzaa Serugi. |
288 | GEN 11:21 | Reu aliishi miaka207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
289 | GEN 11:22 | Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. |
290 | GEN 11:23 | Seregu aliishi miaka mia mbili baada ya kumzaa Nahori. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike. |
296 | GEN 11:29 | Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska. |
297 | GEN 11:30 | Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto. |
298 | GEN 11:31 | Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale. |
304 | GEN 12:5 | Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani. |
305 | GEN 12:6 | Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo. |
310 | GEN 12:11 | Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri. |
313 | GEN 12:14 | Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana. |
316 | GEN 12:17 | Kisha Yahwe akampiga Farao na nyumba yake kwa mapigo makuu kwa sababau ya Sarai, mke wa Abram. |
318 | GEN 12:19 | Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.” |
329 | GEN 13:10 | Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora. |
331 | GEN 13:12 | Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma. |
332 | GEN 13:13 | Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe. |
339 | GEN 14:2 | walifanya vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha, mfalme wa Gomora, Shinabu, mfalme wa Adma, Shemeberi, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela(pia ikiitwa Soari). |
340 | GEN 14:3 | Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi). |
342 | GEN 14:5 | Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu, |
343 | GEN 14:6 | na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa. |
345 | GEN 14:8 | Kisha mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari) walikwenda na kuandaa vita |
346 | GEN 14:9 | dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafme wanne dhidi ya wale watano. |
347 | GEN 14:10 | Na sasa bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, na wafalme wa Sodoma na Gomora walipokimbia, wakaanguka pale. Wale waliosalia wakakimbilia milimani. |
348 | GEN 14:11 | Kwa hiyo adui akachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, na wakaenda zao, |
349 | GEN 14:12 | walipoondoka, wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake na Abram ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote. |
354 | GEN 14:17 | Baada ya Abram kurudi kutoka kumpiga Kadorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae, mfalme wa Sodoma akatoka kuonana nae katika bonde la Shawe (pia iliitwa bonde la mfalme). |
355 | GEN 14:18 | Melkizedeki, mfalme wa Salem, akaleta mkate na divai. Alikuwa ni kuhani wa Mungu aliye juu sana. |
358 | GEN 14:21 | Mfalme wa Sodama akamwambia Abram, “Nipatie watu, na ujichukulie wewe mwenyewe mali.” |
359 | GEN 14:22 | Abram akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua juu mkono wangu kwa Yahwe, Mungu aliye juu sana, muumbaji wa mbingu na nchi, |
361 | GEN 14:24 | Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula na sehemu za watu waliokwenda nami. Aneri, Eskoli, na Mamre na wachukue sehemu zao.” |
379 | GEN 15:18 | Siku hiyo Yahwe akafanya agano na Abram, akisema, “Ninatoa nchi hii kwa uzao wako, kutoka mto wa Misri hadi kwenye mto mkuu, Frati - |
383 | GEN 16:1 | Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri. |
384 | GEN 16:2 | Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai. |
385 | GEN 16:3 | Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake. |
387 | GEN 16:5 | Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe.” |
388 | GEN 16:6 | Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka. |
389 | GEN 16:7 | Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri. |
390 | GEN 16:8 | Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?” Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai.” |
413 | GEN 17:15 | Mungu akamwambia Abraham, “kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara. |
415 | GEN 17:17 | Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?” |
417 | GEN 17:19 | Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake. |
419 | GEN 17:21 | Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.” |