26 | GEN 1:26 | Mung akasema, “na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.” |
56 | GEN 2:25 | Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu. |
63 | GEN 3:7 | Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe. |
64 | GEN 3:8 | Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu. |
106 | GEN 4:26 | Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe. |
109 | GEN 5:3 | Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi. |
112 | GEN 5:6 | Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. |
115 | GEN 5:9 | Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. |
118 | GEN 5:12 | Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. |
131 | GEN 5:25 | Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki. |
134 | GEN 5:28 | Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. |
141 | GEN 6:3 | Yahwe akaema, “ roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.” |
154 | GEN 6:16 | Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu. |
168 | GEN 7:8 | Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi, |
174 | GEN 7:14 | Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa. |
176 | GEN 7:16 | Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango. |
201 | GEN 8:17 | Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi.” |
205 | GEN 8:21 | Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, “ Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya. |
206 | GEN 8:22 | Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.” |
224 | GEN 9:18 | Wana wa Nuhu ambao walitoka katika safina walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Na Hamu akamzaa kanaani. |
225 | GEN 9:19 | Watatu hawa walikuwa ndio wana wa Nuhu, na kutokea kwa hawa nchi yote ikajaa watu. |
236 | GEN 10:1 | Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika. |
237 | GEN 10:2 | Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi. |
239 | GEN 10:4 | Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu. |
241 | GEN 10:6 | Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani. |
242 | GEN 10:7 | Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. |
248 | GEN 10:13 | Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi, |
249 | GEN 10:14 | Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori. |
254 | GEN 10:19 | Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha. |
257 | GEN 10:22 | Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu. |
258 | GEN 10:23 | Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi. |
270 | GEN 11:3 | Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa. |
271 | GEN 11:4 | Wakasema, “njoni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote.” |
279 | GEN 11:12 | Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na mitano akamzaa Shela. |
281 | GEN 11:14 | Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. |
283 | GEN 11:16 | Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. |
285 | GEN 11:18 | Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu. |
287 | GEN 11:20 | Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na miwili, alimzaa Serugi. |
289 | GEN 11:22 | Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. |
291 | GEN 11:24 | Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. |
295 | GEN 11:28 | Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo. |
298 | GEN 11:31 | Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale. |
304 | GEN 12:5 | Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani. |
305 | GEN 12:6 | Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo. |
310 | GEN 12:11 | Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri. |
311 | GEN 12:12 | Wamisri watakapokuona watasema, huyu ni mke wake, na wataniua mimi, lakini watakuacha wewe hai. |
313 | GEN 12:14 | Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana. |
314 | GEN 12:15 | Wakuu wa Farao wakamuona, na kumsifia kwa Farao, na huyu mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao. |
326 | GEN 13:7 | Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo. |
342 | GEN 14:5 | Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu, |
343 | GEN 14:6 | na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa. |
344 | GEN 14:7 | Kisha wakarudi wakaja En Misifati (Pia ikiitwa Kadeshi), na kuishinda nchi yote ya Waamaleki, na pia Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari. |
347 | GEN 14:10 | Na sasa bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, na wafalme wa Sodoma na Gomora walipokimbia, wakaanguka pale. Wale waliosalia wakakimbilia milimani. |
368 | GEN 15:7 | Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi.” |
372 | GEN 15:11 | Wakati ndege walipokuja juu ya mizoga, Abram akawafukuza. |
377 | GEN 15:16 | Katika kizazi cha nne watakuja tena hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujafikia mwisho wake.” |
395 | GEN 16:13 | Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, “Wewe ni Mungu unionaye mimi,” kwa kuwa alisema, “je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?” |
399 | GEN 17:1 | Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu. |
403 | GEN 17:5 | Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi. |
414 | GEN 17:16 | Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye. |
434 | GEN 18:9 | Wakamwambia, “Mke wako Sara yuko wapi?” akajibu. “pale hemani.” |
463 | GEN 19:5 | Wakamwita Lutu, na kumwambia, “Wale wanaume walioingia kwako usiku wakowapi? watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao.” |
467 | GEN 19:9 | Wakasema, “Ondoka hapa!” Wakasema pia, huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao.” Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango. |
474 | GEN 19:16 | Lakini akakawia-kawia. Kwa hiyo watu wale wakamshika mkono wake, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa sababu Yahwe alimhurumia. Wakawatoa nje, na kuwaweka nje ya mji. |
475 | GEN 19:17 | Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, “jiponye nafsi yako! usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali.” |
487 | GEN 19:29 | Wakati Mungu alipoharibu miji ya bondeni, Mungu akamkumbuka Abraham. Akamtoa Lutu kutoka katika maangamizi alipoangamiza miji ambayo katika hiyo Lutu aliishi. |
495 | GEN 19:37 | Wa kwanza akazaa mwana wa kiume, na akamwita jina lake Moabu. Akawa ndiye baba wa wamoabu hata leo. |
496 | GEN 19:38 | Nayule mdogo naye akazaa mwana wa kiume, na akamwita Benami. Huyu ndiye baba wa watu wa Waamoni hata leo. |
509 | GEN 20:13 | Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, “Ni kaka yangu.”''' |
546 | GEN 21:32 | Walifanya agano hapo Bersheba, kisha Abimeleki na Fikoli, amiri wa jeshi, wakarudi katika nchi ya Wafilisti. |
548 | GEN 21:34 | Abraham akasalia kuwa mgeni katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi. |
557 | GEN 22:9 | Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. |
577 | GEN 23:5 | Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema, |
578 | GEN 23:6 | “Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako.” |
594 | GEN 24:2 | Abraham akamwambia mtumwa wake, ambaye alikuwa mkubwa kuliko wote wa nyumbani mwake na mkuu wa vyote alivyo kuwa navyo.”Weka mkono wako chini ya paja langu |
595 | GEN 24:3 | na nitakufanya uape kwa Yahwe, Mungu wa Mbingu na nchi, kwamba hutampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, miongoni mwao wale nikaao kati yao. |
625 | GEN 24:33 | Wakaandaa chakula mbele yake ale, lakini akasema, “Sitakula mpaka niseme kile ninacho paswa kusema.” Kwa hiyo Labani akmwambia, “Sema.” |
629 | GEN 24:37 | Bwana wangu aliniapisha, akisema, “Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi. |
639 | GEN 24:47 | Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake. |
649 | GEN 24:57 | Wakasema, “Tutamwita binti na kumuuliza.” |
652 | GEN 24:60 | Wakambarikia Rebeka, na wakamwambia, “Ndugu yetu, na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu, uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia.” |
662 | GEN 25:3 | Jokshani akamzaa Sheba na Dedani. Wana wa Dedani walikuwa ni Waashuru, Waletushi, na Waleumi. |
663 | GEN 25:4 | Wana wa Midiani walikuwa ni Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Hawa wote walikuwa ni wana wa Ketura. |