7 | GEN 1:7 | Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo. |
16 | GEN 1:16 | Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia. |
24 | GEN 1:24 | Mungu akasema, “ nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo. |
25 | GEN 1:25 | Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaaho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwani vyema. |
26 | GEN 1:26 | Mung akasema, “na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.” |
27 | GEN 1:27 | Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba. |
33 | GEN 2:2 | Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote. |
34 | GEN 2:3 | Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji. |
40 | GEN 2:9 | Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. |
48 | GEN 2:17 | Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.” |
49 | GEN 2:18 | Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.” |
50 | GEN 2:19 | Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake. |
51 | GEN 2:20 | Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye. |
52 | GEN 2:21 | Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu. |
53 | GEN 2:22 | Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu. |
54 | GEN 2:23 | Mwanaume akasema, “kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume. |
59 | GEN 3:3 | lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'” |
60 | GEN 3:4 | Nyoka akamwambia mwanamke, “hakika hamtakufa. |
61 | GEN 3:5 | Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” |
62 | GEN 3:6 | Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala. |
63 | GEN 3:7 | Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe. |
64 | GEN 3:8 | Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu. |
66 | GEN 3:10 | Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.” |
69 | GEN 3:13 | Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.” |
70 | GEN 3:14 | Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako. |
80 | GEN 3:24 | Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima. |
87 | GEN 4:7 | Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde. |
88 | GEN 4:8 | Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua). |
90 | GEN 4:10 | Yahwe akasema, “umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini. |
91 | GEN 4:11 | Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako kutoka mikononi mwako. |
94 | GEN 4:14 | Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.” |
100 | GEN 4:20 | Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama. |
101 | GEN 4:21 | Ndugu yake aliitwa Yubali. Huyu alikuwa baba yao na wale wapigao kinubi na filimbi. |
102 | GEN 4:22 | Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama. |
105 | GEN 4:25 | Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, “ Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.” |
107 | GEN 5:1 | Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe. |
109 | GEN 5:3 | Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi. |
111 | GEN 5:5 | Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki. |
114 | GEN 5:8 | Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki. |
117 | GEN 5:11 | Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki. |
120 | GEN 5:14 | Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki. |
123 | GEN 5:17 | Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki. |
126 | GEN 5:20 | Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki. |
133 | GEN 5:27 | Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki. |
135 | GEN 5:29 | Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.” |
137 | GEN 5:31 | Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki. |
138 | GEN 5:32 | Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi. |
142 | GEN 6:4 | Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. |
145 | GEN 6:7 | Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.” |
148 | GEN 6:10 | Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti. |
152 | GEN 6:14 | Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje. |
153 | GEN 6:15 | Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini. |
154 | GEN 6:16 | Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu. |
155 | GEN 6:17 | Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa. |
156 | GEN 6:18 | Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao. |
157 | GEN 6:19 | Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume. |
160 | GEN 6:22 | Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya. |
161 | GEN 7:1 | Yahwe akamwambia Nuhu, “Njoo, wewe na nyumba yako wote, katika safina, kwa kuwa nimeona kuwa wewe ni mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki. |
162 | GEN 7:2 | Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, lete wawili wawili, wakiume na wakike. |
163 | GEN 7:3 | Pia na kwa ndege wa angani, lete saba wa kiume na saba wa kike, ili kuhifadhi kizazi chao juu ya uso wa nchi yote. |
165 | GEN 7:5 | Nuhu alifanya yote ambayo Yahwe alimuagiza. |
167 | GEN 7:7 | Nuhu, watoto wake wa kiume, mke wake, na wake za watoto wake waliingia katika safina pamoja kwa sababu ya maji ya gharika. |
168 | GEN 7:8 | Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi, |
169 | GEN 7:9 | wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu. |
171 | GEN 7:11 | Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka. |
173 | GEN 7:13 | Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina. |
174 | GEN 7:14 | Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa. |
175 | GEN 7:15 | Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina. |
176 | GEN 7:16 | Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango. |
177 | GEN 7:17 | Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi. |
178 | GEN 7:18 | Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. |
179 | GEN 7:19 | Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa. |
181 | GEN 7:21 | Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu. |
182 | GEN 7:22 | Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa. |
183 | GEN 7:23 | Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa mchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia. |
185 | GEN 8:1 | Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini. |