1 | GEN 1:1 | Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. |
2 | GEN 1:2 | Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji. |
3 | GEN 1:3 | Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru. |
4 | GEN 1:4 | Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza. |
5 | GEN 1:5 | Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza. |
6 | GEN 1:6 | Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.” |
7 | GEN 1:7 | Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo. |
8 | GEN 1:8 | Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili. |
9 | GEN 1:9 | Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. |
10 | GEN 1:10 | Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema. |
11 | GEN 1:11 | Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo. |
12 | GEN 1:12 | Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. |
13 | GEN 1:13 | Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu. |
14 | GEN 1:14 | Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka. |
15 | GEN 1:15 | Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo. |
16 | GEN 1:16 | Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia. |