Wildebeest analysis examples for:   swh-swhulb   k    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

2  GEN 1:2  Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.
3  GEN 1:3  Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru.
4  GEN 1:4  Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
6  GEN 1:6  Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.”
7  GEN 1:7  Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo.
8  GEN 1:8  Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili.
9  GEN 1:9  Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo.
10  GEN 1:10  Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema.
11  GEN 1:11  Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo.
12  GEN 1:12  Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
13  GEN 1:13  Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.
14  GEN 1:14  Mungu akasema, kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
15  GEN 1:15  Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo.
16  GEN 1:16  Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
17  GEN 1:17  Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi,
18  GEN 1:18  kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.
19  GEN 1:19  Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne.
20  GEN 1:20  Mungu akasema, “maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.”
21  GEN 1:21  Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
22  GEN 1:22  Mungu akavibariki, akisema, “zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.”
23  GEN 1:23  Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.