Wildebeest analysis examples for:   swh-swhulb   z    February 11, 2023 at 19:39    Script wb_pprint_html.py   by Ulf Hermjakob

1  GEN 1:1  Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
2  GEN 1:2  Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.
4  GEN 1:4  Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.
5  GEN 1:5  Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
14  GEN 1:14  Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
16  GEN 1:16  Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
17  GEN 1:17  Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi,
18  GEN 1:18  kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.
22  GEN 1:22  Mungu akavibariki, akisema,zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.”
28  GEN 1:28  Mungu akawabariki na akawaambia,zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,”
29  GEN 1:29  Mungu akasema, “tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.
30  GEN 1:30  Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai ni metoa kila mmea kwa ajili ya chakula.” ikawa hivyo.
31  GEN 1:31  Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita.
32  GEN 2:1  Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi.
33  GEN 2:2  Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
34  GEN 2:3  Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
38  GEN 2:7  Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.
40  GEN 2:9  Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
42  GEN 2:11  Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu.
43  GEN 2:12  Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. pia kuna bedola na jiwe shohamu.
46  GEN 2:15  Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
47  GEN 2:16  Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, “kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.
48  GEN 2:17  Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.”
49  GEN 2:18  Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.”
51  GEN 2:20  Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.
52  GEN 2:21  Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.
58  GEN 3:2  Mwanamke akamwambia nyoka, “Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani,
62  GEN 3:6  Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala.
63  GEN 3:7  Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe.
67  GEN 3:11  Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?”
70  GEN 3:14  Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.
71  GEN 3:15  Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.”
72  GEN 3:16  Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.”
73  GEN 3:17  Kwa Adam akasema, “kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, “ usile matunda yake', ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako.
74  GEN 3:18  Ardhi itazaa miiba na mbigili kwa ajili yako, na utakula mimea ya shambani.
77  GEN 3:21  Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha.
78  GEN 3:22  Yahwe Mungu akasema, “ sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele.”
80  GEN 3:24  Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.
81  GEN 4:1  Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, “ nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe.”
82  GEN 4:2  Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.
83  GEN 4:3  Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe.
84  GEN 4:4  Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,
88  GEN 4:8  Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
89  GEN 4:9  Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
92  GEN 4:12  Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.”
93  GEN 4:13  Kaini akamwambia Yahwe, “Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili.
94  GEN 4:14  Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.”
97  GEN 4:17  Kaini akamjua mke wake na akapata mimba. Akamzaa Henoko. Akajenga mji na akauita kwa jina la mwanae Henoko.
98  GEN 4:18  Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki.
100  GEN 4:20  Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama.
102  GEN 4:22  Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama.
103  GEN 4:23  Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua.
105  GEN 4:25  Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, “ Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.”
106  GEN 4:26  Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe.
107  GEN 5:1  Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
109  GEN 5:3  Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
110  GEN 5:4  Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
112  GEN 5:6  Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
113  GEN 5:7  Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.