195 | GEN 8:11 | Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi. |
215 | GEN 9:9 | “Kwa ajili yangu, sikiliza! Ninakwenda kulithibitisha agano langu pamoja nawe na uzao wenu baada yenu, |
273 | GEN 11:6 | Yahwe akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Hivikaribuni halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya. |
362 | GEN 15:1 | Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” |
450 | GEN 18:25 | Hasha usifanye hivyo, kuwauwa watakatifu pamoja na waovu, ili kwamba watakatifu watendewe sawa na waovu. Hasha! Je muhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?” |
452 | GEN 18:27 | Abraham akajibu na kusema, “Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu! |
456 | GEN 18:31 | Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.” |
467 | GEN 19:9 | Wakasema, “Ondoka hapa!” Wakasema pia, huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao.” Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango. |
475 | GEN 19:17 | Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, “jiponye nafsi yako! usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali.” |
476 | GEN 19:18 | Lutu akawambia, “Hapana, tafadhali bwana zangu! |
480 | GEN 19:22 | Harakisha! toroka uende pale, kwa kuwa sitafanya chochote mpaka ufike pale.” kwa hiyo mji ule ukaitwa Soari. |
598 | GEN 24:6 | Abraham akamwambia, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule! |
655 | GEN 24:63 | Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija! |
791 | GEN 28:17 | Akaogopa na kusema, “Eneo hili linatisha kama nini! Hili sio kingine zaidi ya nyumba ya Mungu. Hili ni lango la mbinguni.” |
817 | GEN 29:21 | Kisha Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe! |
821 | GEN 29:25 | Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa? |
844 | GEN 30:13 | Lea akasema, “Nina furaha! Kwa maana mabinti wataniita furaha.” Hivyo akamwita jina lake Asheri. |
1436 | GEN 47:15 | Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?” |
1650 | EXO 5:17 | Lakini Farao akasema, “Ninyi ni wavivu! Wavivu ninyi! Ninyi mwasema, 'Turuhusu twende kumtolea Yahwe sadaka.' |
1761 | EXO 9:18 | Sikiliza! Kesho muda kama huu nita leta mvua ya mawe ya barafu kubwa, kama ambayo haijawai kuonekana Misri toka ilipo anza hadi sasa. |
1789 | EXO 10:11 | Hapana! Nenda, wanaume tu miongoni mwenu, na mmuabudu Yahweh, kwa kuwa hilo ndilo mnalo litaka.” Kisha Musa na Aruni wakaondolewa uweponi mwa Farao. |
1806 | EXO 10:28 | Farao alimwambia Musa, “Toka kwangu! Kuwa muangalifu na jambo moja, kwamba usinione tena, kwa kuwa siku utakapo uona uso wangu, utakufa.” |
2470 | EXO 32:31 | Musa akarejea kwa Yahweh akasema,” Oh! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. |
2997 | LEV 10:19 | Kisha Aroni akamjibu Musa, “ Tazama, leo walitoa sadaka yao ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa mbele za Yahweh, na jambo hili vilevile limetendeka kwangu leo. Ikiwa nimeshakula sadaka ya dhambi leo, Je! Isingekuwa imeshapendeza mbele za Yahweh?” |
3259 | LEV 18:7 | Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye. |
4111 | NUM 14:2 | Watu wote wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Watu wote wakawaambia, “Ni bora kama tungelifia katika nchi ya Misri, au katika hili! |
4140 | NUM 14:31 | Bali watoto wenu ambao mlisema kuwa watakuwa watumwa, wao ndio nitakaowapeleka katika nchi hiyo. Wao wataifurahia nchi ambayo nInyi mmeikataa! |
4198 | NUM 16:3 | Walikusanyika pamoja kumpinga Musa na Haruni. Wakawaambia, “Ninyi sasa mnatumia mamlaka zaidi ya uwezo wenu! Watu wote wamejitenga, kila mmoja wao, na BWANA yuko pamoja nao. Kwa nini mnajiinua sana juu ya watu wengine wa BWANA?” |
4205 | NUM 16:10 | Amewasogeza karibu, na ndugu zako, wa uzao wa Lawi pamoja nanyi, na sasa mnataka na ukuhani pia! |
4208 | NUM 16:13 | Kwani jambo dogo kwamba umetuleta mpaka kwenye nchi inayotiririka maziwa na asali, ili kutuua katika jangwa hili? Sasa unataka kujifanya kuwa mtawala wetu! |
4253 | NUM 17:23 | Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu! |
4257 | NUM 17:27 | Wana wa Israeli wakanena na Musa wakisema, “tutakufa hapa! Wote tutaangamia! |
4370 | NUM 21:29 | Ole wako, Moabu! umepotea, enyi watu wa Chemoshi. Amewafanya watu wake kuwa wakimbizi na binti zake kuwa wafungwa wa Sihoni mfalme wa Waamori. |
4452 | NUM 24:5 | Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli! |
4905 | DEU 1:11 | Yahwe aweza, Mungu wa baba zako, kukufanya wewe mara elfu moja zaidi ya ulivyo, na kukubariki, kama alivyokuahidi! |
4988 | DEU 3:11 | (Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.) |
5084 | DEU 5:29 | Oh, kulikuwa na moyo wa namba hiyo ndani yao, kwamba wataniheshimu na daima kushika amri zangu zote, ili iweze kuwa vizuri kwao na pamoja na watoto wao milele! |
5680 | DEU 28:67 | Asubuhi utasema, “Natamani ingekuwa jioni! ” na jioni utasema, “Natamani ingekuwa asubuhi! ” kwa sababu ya hofu mioyoni mwenu na vitu ambavyo macho yako italazimu kuona. |
5766 | DEU 32:6 | Je! Unamzawadia Yahwe kwa njia hii, enyi watu wapumbavu na msiojitambua? Je! yeye si baba yenu, yule ambaye aliwaumba? Aliwaumba na kuwaimarisha. |
5789 | DEU 32:29 | Ah laiti wangekuwa na hekima, wangeelewa hili, na kuzingatia ujio wa hatima yao! |
5841 | DEU 33:29 | Baraka zako ni nyingi, Israeli! Nani kama wewe, watu waliokombolewa na Yahwe, ngao ya msaada wako, na upanga wa utukufu wako? Maadui zako watakuja kwako kwa kutetemeka; utakanyanga sehemu zao zilizoinuka. |
5862 | JOS 1:9 | Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko. |
5885 | JOS 2:14 | Wanaume wakamjibu, “maisha yetu kwa ajili ya yenu, hata kifo! Kama hamtasema habari zetu, na Yahweh akisha kutupa nchi hii, tutakuwa wenye huruma na waaminifu kwenu.” |
5906 | JOS 3:11 | Tazama! Sanduku la agano la Bwana wa nchi yote litavuka mbele yenu katika Yordani. |
5967 | JOS 6:16 | Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, “Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahweh amewapa ninyi mji. |
5985 | JOS 7:7 | Kisha Yoshua akasema, “Oo, Yahweh Bwana, kwanini umewavusha watu hawa ng'ambo ya Yordani? Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza? ikiwa kama tulifanya maamuzi tofauti na tungekaa katika upande mwingine wa Yordani! |
5991 | JOS 7:13 | Inuka! Waweke watu wakfu kwangu, na uwaambie, 'Jiwekeeni wakfu ninyi wenyewe kesho. Kwa kuwa, Yahweh, Mungu wa Israeli asema hivi, “Kuna vitu vilitengwa ili kuteketezwa ambavyo bado viko miongoni mwenu, Israeli. Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu mpaka pale mtakapoviondoa miongoni mwenu vitu vyote ambavyo vilitengwa kwa ajili ya kuteketezwa.” |
6072 | JOS 10:6 | Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua na kwa jeshi huko Giligali. Walisema, “ Upesi! Msiuondoa mkono wenu kutoka kwa watumishi wenu. Kwaeni mje haraka na mtuokoe. Mtusaide, maana wafalme wote wa Waamori wanaoishi katika nchi ya milima wamekusanyika kwa pamoja ili watushambulie. |
6199 | JOS 14:10 | Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano. |
6450 | JOS 22:22 | “Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo |
6456 | JOS 22:28 | Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, “ Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi.” |
6466 | JOS 23:4 | Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi. |
6549 | JDG 2:2 | Nikasema, 'Sitakuvunja kamwe agano langu na wewe. Usifanye agano na wale wanaoishi katika nchi hii. Ziangushe madhabahu zao. Lakini hukusikiliza sauti yangu. Je! ni nini hiki ulichokifanya? |
6615 | JDG 4:14 | Debora akamwambia Baraka, Nenda! Kwa maana hii ndiyo siku ambayo Bwana amekupa ushindi juu ya Sisera. Je! si Bwana anayekuongoza? Basi Baraka akashuka kutoka mlima wa Tabori na watu kumi elfu wakamfuata. |
6627 | JDG 5:2 | 'Viongozi wanapoongoza mbele ya Israeli, watu wanapojitolea kupigana vita, tunamsifu Bwana! |
6628 | JDG 5:3 | Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi! Mimi nitamwimbia Bwana; Nami nitamsifu Bwana, Mungu wa Israeli. |
6632 | JDG 5:7 | Kulikuwa na mashujaa wachache huko Israeli, mpaka mimi, Debora, nilipochukua amri- mama alichukua amri katika Israeli! |
6634 | JDG 5:9 | Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli, pamoja na watu ambao walijitolea -tunambariki Bwana kwa ajili yao! |
6637 | JDG 5:12 | Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu. |
6646 | JDG 5:21 | Mto Kishoni uliwaondoa, mto ule wa kale, Mto Kishoni. Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu! |
6656 | JDG 5:31 | Naam, adui zako wote wataangamia, Ee Bwana! Lakini marafiki zako watakuwa kama jua wakati linapoongezeka kwa uwezo wake. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini. |
6668 | JDG 6:12 | Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nanyi, mpiganaji mwenye nguvu! |
6678 | JDG 6:22 | Gideoni alielewa kuwa yule alikuwa malaika wa Bwana. Gideoni akasema, “Ewe Bwana MUNGU! Kwa maana nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!” |
6679 | JDG 6:23 | Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope, huwezi kufa.” |
6713 | JDG 7:17 | Akawaambia, 'Niangalieni mimi na kufanya yale ninayoyafanya. Tazama! Ninapofika kwenye mwisho wa kambi, ni lazima mfanye kile ninachofanya. |
6723 | JDG 8:2 | Akawaambia, “Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi? Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri? |
6724 | JDG 8:3 | Mungu amewapa ushindi juu ya wakuu wa Midiani-Orebu na Zeeb! Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?” Hasira yao ikashuka chini aliposema hili. |
6742 | JDG 8:21 | Ndipo Zeba na Salmuna wakasema, simama mwenyewe, utuue! Kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Gideoni akasimama na kumwua Zeba na Salmuna. Pia aliondoa mapambo yaliyokuwa juu ya shingo za ngamia zao. |
6765 | JDG 9:9 | Lakini mti wa mizeituni ukawaambia, Je! Nitaacha mafuta yangu, ambayo hutumiwa kuheshimu miungu na wanadamu, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine? |
6784 | JDG 9:28 | Gaali mwana wa Ebedi, akasema, Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu! Kwa nini tunapaswa kumtumikia? |
6785 | JDG 9:29 | Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, 'liondoe nje jeshi lako lote.' |
6866 | JDG 11:35 | Mara tu alipopomwona, alirarua nguo zake akasema, 'Loo! Binti yangu! Umenivunja kwa huzuni, na umekuwa mtu anayenisababishia maumivu yangu! Kwa maana nimeapa kwa Bwana, wala siwezi kurudisha ahadi yangu. |
6898 | JDG 13:12 | Manoa akasema, Sasa maneno yako yatimike. Je! kuna maagizo gani kwa ajili ya mtoto, na kazi yake itakuwa nini? ' |
6904 | JDG 13:18 | Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona unauliza jina langu? Ni ajabu! ' |
6914 | JDG 14:3 | Baba yake na mama yake wakamwambia, “Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote? Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Samsoni akamwambia baba yake, “Nichukulie kwa ajili yangu, kwa maana wakati nilipomwangalia, alinipendeza.' |
6927 | JDG 14:16 | Mke wa Samsoni alianza kulia mbele yake; Akasema, 'Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi. Umesema kitendawili kwa baadhi ya watu wangu, lakini hujawaambia jibu. ' Samsoni akamwambia, 'Angalia hapa, kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe?' |
6942 | JDG 15:11 | Kisha watu elfu tatu wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Eatamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?” Samsoni akawaambia, “Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.” |
6979 | JDG 16:28 | Samsoni akamwita Bwana, akasema, “Bwana MUNGU, nipe nia! Tafadhali niimarishe mara moja tu, Mungu, ili nipate kulipiza kisasi kwa Wafilisti kwa kuchukua macho yangu mawili. |
6984 | JDG 17:2 | Akamwambia mama yake, “Shilingi 1, 100 za fedha ambazo zilichukuliwa kutoka kwako, ambazo ulizungumza kwa kiapo, na kuniambia-tazama hapa! Ninazo fedha pamoja nami. Nimeziiba.” Mama yake akasema, 'Na Bwana atakubariki, mwanangu!' |
7004 | JDG 18:9 | Wakasema, “Njoo! Hebu tuwashambulie! Tumeona ardhi na ni nzuri sana. Je hamfanyi kitu? Msiwe wavivu kushambulia na kuchukua ardhi. |
7005 | JDG 18:10 | Mnapoenda, mtakuta watu wanaofikiri wapo salama, na nchi ni pana! Mungu amewapa ninyi-mahali ambako hapajapungukiwa kitu chochote duniani. ' |
7046 | JDG 19:20 | Huyo mzee akawasalimu, “Amani iwe na wewe! Nitakupatia mahitaji yako yote. Usikae usiku tu katika njia kuu.” |
7049 | JDG 19:23 | Yule mtu, mwenye nyumba, akawajia, akawaambia, “Hapana, ndugu zangu, tafadhali msifanye jambo baya! Kwa kuwa mtu huyu ni mgeni nyumbani kwangu, musifanye jambo hili baya!” |
7056 | JDG 19:30 | Wote waliona hili wakasema, “Kitu hicho hakijawahi kufanyika au kuonekana tangu siku ambayo watu wa Israeli walikuja kutoka nchi ya Misri mpaka leo. Fikiria juu ya hili! Tupe ushauri! Tuambie nini cha kufanya!” |
7126 | JDG 21:22 | Wakati baba zao au ndugu zao watakapokuja kutupinga, tutawaambia, 'Tupeni neema! Waache wabaki kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita. Na ninyi hamna hatia juu ya ahadi, kwa sababu hamkuwapa wao binti zenu.'” |
7140 | RUT 1:11 | Lakini Naomi alisema, “Rudini, wanangu! Kwa nini mtakwenda na mimi? Kwani bado nina watoto katika tumbo langu kwa ajili yenu, ili kwamba waje wawe waume zenu? |
7142 | RUT 1:13 | Mtasubiri na msiolewe sasa? Hapana, wanangu! Ina nihuzunisha zaidi, kuliko inavyo wahuzunisha ninyi, kwa sababu mkono wa Yahweh umeenda kinyume na mimi.” |
7182 | RUT 3:8 | Panapo usiku wa manane Boazi alisituka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake! |
7185 | RUT 3:11 | Na sasa, mwanangu, usiogope! Nitakufanyia yote unayosema, kwa sababu mji wa watu wangu wote wanajua kuwa wewe ni mwanamke unayestahili. |
7240 | 1SA 1:26 | Akasema, “Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, Mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA. |
7306 | 1SA 4:7 | Wafilisti waliogopa sana, “Mungu ameingia kambini.” Wakasema, “Ole wetu! Jambo kama hili halijawahi kutokea huko nyuma! |
7307 | 1SA 4:8 | Ole wetu! Ni nani atatulinda dhidi ya nguvu za Mungu mwenye uwezo? Huyu ndiye Mungu aliyewashambulia Wamisri kwa aina tofauti za mapigo mengi jangwani. |
7410 | 1SA 9:17 | Samweli alipomuona Sauli, BWANA akamwambia, “Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu.” |
7417 | 1SA 9:24 | Basi mpishi alichukua paja lililokuwa limeinuliwa katika dhabihu na kile kilichokuwa pamoja nalo, akaitenga mbele ya Sauli. Kisha Samweli akasema, “Angalia kile kilichokuwa kimetunzwa kwa ajili yako! Kula, kwa sababu kilitunzwa hadi wakati maalum ufike kwa ajili yako. Na kwa sasa waweza kusema, 'Nimewaalika watu.”' Kwa hiyo Sauli alikula pamoja na Samweli siku hiyo. |
7555 | 1SA 14:45 | Basi watu wakamuuliza Sauli, “Je, inampasa Sauli afe, ni nani aliyetekeleza ushindi huu mkubwa kwa ajili ya Israeli? Mbali na hayo! Kama BWANA aishivyo, hata unywele mmoja wa kichwa chake hautaanguka chini, kwa maana leo amefanya kazi pamoja na Mungu.” Hivyo hao watu walimuokoa Yonathani ili asife. |
7575 | 1SA 15:13 | Samweli akamwendea Sauli, na Sauli akamwambia, “Umebarikiwa na BWANA! Nami nimetekeleza amri ya BWANA.” |
7616 | 1SA 16:19 | Hivyo Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, na kusema, “Nitumie mtoto wako Daudi, anayewatunza kondoo.” 1 Samweli! 6: 20-21 |
7686 | 1SA 18:8 | Sauli alikasirika sana, na wimbo huu haukumpendeza. Naye akasema, “Wamemsifia Daudi juu ya makumi elfu, lakini wamenisifia melfu tu mimi! Atapata kitu gani zaidi isipokuwa ufalme? |
7741 | 1SA 20:9 | Yonathani akasema, “La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?” |
7762 | 1SA 20:30 | Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, “Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako? |