1585 | EXO 3:5 | Mungu akasema, “Usinikaribie! Vua viatu katika miguu yako, kwa kuwa mahali uliposimama ni mahali palipowekwa wakfu kwa ajili yangu.” |
5988 | JOS 7:10 | Yahweh akamwambia Yoshua, “Inuka! kwanini umelala kifudifudi? |
6439 | JOS 22:11 | Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, “Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli.” |
6705 | JDG 7:9 | Usiku huo huo Bwana akamwambia, “Simama! Kavamie kambi, kwa maana nitakupa ushindi juu yake. |
6709 | JDG 7:13 | Gideoni alipofika huko, mtu alikuwa akimwambia mwenzake ndoto. Mtu huyo akasema, “Angalia! Niliota ndoto, na nikaona mkate wa shayiri umeanguka ndani ya kambi ya Midiani. Ukaja hemani, na kuipiga kwa nguvu sana hata ikaanguka chini ikapinduka na kulala chini. ' |
6711 | JDG 7:15 | Gideoni aliposikia habari ya ile ndoto na tafsiri yake, akainama chini na kuabudu. Alirudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Simameni! Bwana ametupa ushindi juu ya jeshi la Midiani.” |
6896 | JDG 13:10 | Basi mwanamke akakimbia haraka akamwambia mumewe, “Tazama! Yule mtu ameonekana kwangu-aliyekuja kwangu siku ile!” |
7004 | JDG 18:9 | Wakasema, “Njoo! Hebu tuwashambulie! Tumeona ardhi na ni nzuri sana. Je hamfanyi kitu? Msiwe wavivu kushambulia na kuchukua ardhi. |
7014 | JDG 18:19 | Wakamwambia, “Tulia! Weka mkono wako kwenye kinywa chako na uje nasi, na uwe kwetu baba na kuhani. Je, ni bora kuwa wewe kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuhani kwa kabila na jamaa katika Israeli?” |
7139 | RUT 1:10 | Wakamwambia, “Hapana! tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako.” |
8336 | 2SA 13:16 | Lakini yeye akamjibu, “Hapana! kwa maana uovu wa kunifanya ni uondoke ni mbaya zaidi ya kile ulichonitenda!” Lakini Amnoni hakumsikiliza. |
8447 | 2SA 16:18 | Hushai akamwambia Absalomu, “Hapana! badala yake, yule ambaye Yahwe, watu hawa na watu wote wa Israeli wamemchagua huyo ndiye nitakaye kuwa upande wake na ndiye nitakaye kaa naye. |
8492 | 2SA 18:11 | Yoabu akamwambia aliyemwambia kuhusu Absalomu, “Tazama! Ulimwona! Kwa nini haukumpiga hata chini. Ningekupa shekeli kumi za fedha na mkanda.” |
8711 | 2SA 24:16 | Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako sasa.” Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi. |
8824 | 1KI 3:5 | BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, “Omba! uanataka nikupe nini?” |
9217 | 1KI 13:30 | Akaulaza mwili kwenye kaburi lake, nao wakamwombolezea, wakisema, “Aa! ndugu yangu!” |
9847 | 2KI 11:14 | Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na manahodha na wapiga mabaragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!” |
10954 | 1CH 21:15 | Mungu akatuma malaika Yerusalemu kuiharibu. Wakati alipo taka kuiharibu, Yahweh akatazama na kubadili nia yake kuhusu shambulio. Akasema kwa malaika wa uharibifu, “Imetosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Yahweh alikua amesimama eneo la kupeta la Orinani Myebusi. |
11206 | 2CH 1:7 | Mungu akamtokea Selemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?” |
11674 | 2CH 23:13 | na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!” |
12417 | NEH 6:11 | Nikajibu, “Je! Mtu kama mimi ninaweza kukimbia? Na mtu kama mimi ninaweza kuingia hekaluni ili nipate kuishi? Sitaingia.” |
12503 | NEH 8:6 | Ezra akamshukuru Bwana, Mungu mkuu; na watu wote wakainua mikono yao, wakajibu, “Amina! Amina!” Wakainamisha vichwa vyao, wakamwabudu Bwana kwa nyuso zao zikiwa chini. |
12508 | NEH 8:11 | Basi Walawi wakawafanya watu kuwa na utulivu, wakisema, “Nyamazeni! kwa maana siku hii ni takatifu. Msiwe na huzuni.” |
12692 | NEH 13:17 | Kisha nikawaambia viongozi wa Yuda, “Je! ni ubaya gani huu mnafanya, kuinajisi siku ya Sabato? |
17038 | PRO 20:14 | “Mbaya! Mbaya!” anasema mnunuzi, lakini akiondoka anajisifu. |
19093 | JER 3:22 | “Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!” “Tazama! tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu! |
19106 | JER 4:10 | Kwa hiyo nikasema, “Ahaa! BWANA. Kwa hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kuwaambia, 'Kutakuwa na amani kwenu.'Wakati upanga unawaangukia dhidi ya maisha yao.” |
19292 | JER 10:22 | Taarifa imewadia, “Tazama! inakuja, tetemeko kubwa linakuja kutoka katika nchi ya kaskazini kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, na maficho ya mbweha. |
19827 | JER 32:27 | “Angalia! Mimi ni Yahwe, Mungu wa wanadamu wote. Kuna kitu cho chote kigumu sana kwangu kukifanya? |
20058 | JER 42:14 | Tudhani kwamba mnasema, “Hapana! Tutaenda kwenye nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita yoyote, ambayo hatutasikia sauti ya tarumbeta, na hatutaona njaa ya chakula. Tutaishi huko.” |
20593 | EZK 3:22 | Hivyo mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu huko, akanambia, “Inuka! nenda uwandani, na nitaongea na wewe huko!” |
20613 | EZK 4:15 | Ndivyo alivvyo niambia, “Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo.” |
20623 | EZK 5:8 | kwa hiyo Bwana asema hivi, “Tazama! Mimi mwenyewe nitatenda juu yenu. Nitato hukumu kati yenu ili mataifa waone. |
20776 | EZK 12:27 | “Mwanadamu! Tazama, nyumba ya Israeli imesema, 'Lile ono alionalo ni kwa siku nyingi kutoka sasa, na ametabiri kipindi kilicho mbali sana.' |
21141 | EZK 24:16 | “mwanadamu! Tazama, ninachukua tamaa ya macho yako kutoka kwako pamoja na tauni, lakini hutaomboleza wala kulia, na machozi yako hayatatoka. |
21144 | EZK 24:19 | Watu wameniuliza, “Ji! hautatuambia haya mambo yanamaana gani, mambo ambayo unayoyafanya?” |
21160 | EZK 25:8 | Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu Moabu na Seiri husema “Tazama! Nyumba ya Yuda ni kama kila taifa jingine.” |
22985 | ZEC 3:4 | Malaika akawaambia waliosimama mbele yake, “Mvulisheni hayo mavazi machafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama! nimeuondoa uovu wako na nitakuvika mavazi safi.” |
23427 | MAT 8:13 | Yesu akamwambia Jemadari, “Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako”. Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo. |
23911 | MAT 21:16 | Wakamwambia, “Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?” Yesu akawaambia, “Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, 'Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?'' |
23983 | MAT 22:42 | Akisema, “J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.” |
24178 | MAT 26:55 | Wakati huo Yesu akauambia umati, “Je! Mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi? Kila siku nilikaa hekaluni nikifundisha, na hamkunishika! |
24188 | MAT 26:65 | Ndipo Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Je, twahitaji tena ushahidi wa nini? Angalia, tayari mmesikia akikufuru. |
24209 | MAT 27:11 | Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, “Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu alimjibu, “Wewe wasema hivyo.” |
24718 | MRK 11:9 | Wale waliokwenda mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana. |
24730 | MRK 11:21 | Petro alikumbuka na kusema, “Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka”. |
24758 | MRK 12:16 | Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, “Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, “Ya Kaisari.” |
24766 | MRK 12:24 | Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?” |
24770 | MRK 12:28 | Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?” |
24777 | MRK 12:35 | Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi? |
24924 | MRK 15:29 | Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, “Aha! wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, |
25602 | LUK 13:15 | Bwana akamjibu na akasema, “wanafiki! Hakuna kila mmoja wenu kufungua punda wako au ng'ombe kutoka zizini na kuwaongoza kumpeleka kunywa siku ya Sabato? |
25997 | LUK 22:64 | Baada ya kumfunika macho, wakamuuliza, wakisema, “Tabiri! Ni nani aliyekupiga?” |
26662 | JHN 12:13 | walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli.” |
27331 | ACT 10:3 | Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia “Kornelio! |
27797 | ACT 22:25 | Hata walipokuwa wamemfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliye simama karibu naye, “Je! ni haki kwenu kumpiga mtu aliye Mrumi na bado hajahukumiwa?” |
30754 | JUD 1:14 | Enoko, wa saba katika orodha ya Adamu, alitabiri kuhusu wao, akisema, “Tazama! Bwana anakuja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake, |
30782 | REV 1:17 | Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho, |
30877 | REV 6:16 | Wakaiambia milima na miamba, “Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo. |
30890 | REV 7:12 | wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!” |
31030 | REV 16:7 | Nikasikia madhabahu ikijibu, “Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki.” |
31089 | REV 19:3 | Kwa mara ya pili walisema, “Haleluya! Moshi hutoka kwake milele na milele.” |
31092 | REV 19:6 | Ndipo nilisikia sauti kama sauti ya kundi kubwa la watu, kama sauti ya ngurumo ya maji mengi, na kama ngurumo ya radi, ikisema, “Haleluya! Bwana ni Mungu wetu, mtawala juu ya wote, hutawala. |
31125 | REV 21:3 | Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao. |
31127 | REV 21:5 | Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, “Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya.” Alisema, “Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli.” |
31156 | REV 22:7 | “Tazama! Ninakuja upesi! Amebarikiwa yeye anayeyatii maneno ya unabii wa kitabu hiki.” |
31161 | REV 22:12 | “Tazama! Naja upesi. Ujira wangu uko pamoja nami, kumlipa kila mmoja kulingana na alichokifanya. |
31169 | REV 22:20 | Yeye ashuhudiaye mambo haya asema, “Ndiyo! Naja upesi.” Amina! Njoo, Bwana Yesu! |