57 | GEN 3:1 | Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?” |
318 | GEN 12:19 | Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.” |
360 | GEN 14:23 | kwamba sitachukua uzi wala gidamu ya kiatu, au kitu chochote ambacho ni chako, 'ili kwamba usiseme, nimemfanya Abram kuwa tajiri.' |
501 | GEN 20:5 | Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.” |
599 | GEN 24:7 | Yahwe, Mungu wa mbingu, ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu na kutoka katika nchi ya ndugu zangu, na ambaye aliniahidia kwa kiapo maalumu akisema, 'Nitawapa uzao wako nchi hii,' atatuma malaika wake mbele yako, na utapata mke kwa ajili ya mwanangu kutoka huko. |
634 | GEN 24:42 | Hivyo nimefika leo kisimani, na nikasema, 'O Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, tafadhari, ikiwa kweli umekusudia kuifanya safari yangu kuwa yenye kufanikiwa - |
637 | GEN 24:45 | Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.' |
639 | GEN 24:47 | Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake. |
702 | GEN 26:9 | Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, “Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?” Isaka akamwambia, “Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue.” |
735 | GEN 27:7 | 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.' |
862 | GEN 30:31 | Hivyo Labani akasema, “Je nikulipe nini? Yakobo akasema, 'Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza. |
882 | GEN 31:8 | Ikiwa alisema, 'Wanyama wenye mabaka watakuwa ujira wako,' ndipo kondoo wote walipozaa watoto wenye mabaka. Na aliposema, wenye milia watakuwa ujira wako,' ndipo kundi lote lilipozaa watoto wenye milia. |
885 | GEN 31:11 | Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.' |
886 | GEN 31:12 | Akasema, 'Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea. |
903 | GEN 31:29 | Iko katika uwezo wangu kukudhuru, lakini Mungu wa baba yako alisema nami usiku wa leo na kuniambia, 'Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari.' |
933 | GEN 32:5 | Aliwaagiza, kusema, “Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: 'Nimekuwa nikikaa na Labani, naye amekawilisha kurudi kwangu hata sasa. |
938 | GEN 32:10 | Yakobo akasema, “Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe, uliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha,' |
941 | GEN 32:13 | Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari, ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake.” |
946 | GEN 32:18 | Akamwagiza mtumishi wa kwanza, akisema, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, akasema, 'Ninyi ni wa nani? Mnakwenda wapi? Na wanyama hawa mbele yenu ni wa nani? |
947 | GEN 32:19 | Ndipo umwambie, 'Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu.” |
949 | GEN 32:21 | Mnapaswa pia kusema, 'mtumwa wako Yakobo pia anakuja nyuma yetu.” Kwani alifikiri, “nitamtuliza Esau kwa zawadi nilizozituma mbele yangu. Kisha baadaye, nitakapomwona, bila shaka atanipokea.” |
1097 | GEN 37:13 | Israeli akamwambia Yusufu, 'Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao.” Yusufu akamwambia, “nipo tayari.” |
1101 | GEN 37:17 | Yule mtu akasema, “Waliondoka mahali hapa, kwa maana niliwasikia wakisema, 'Haya twende Dothani.” Yusufu akawafuata ndugu zake na kuwaona huko Dothani. |
1104 | GEN 37:20 | Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje.” |
1142 | GEN 38:22 | Akarudi kwa Yuda na kusema, “Sikumwona. Pia watu wa eneo hilo wamesema, 'Hajawai kuwapo kahaba hapa.” |
1275 | GEN 42:22 | Rubeni akawajibu, “Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu.” |
1284 | GEN 42:31 | Tukamwambia, 'Tu watu wa kweli sisi. Sisi siyo wapelelezi. |
1286 | GEN 42:33 | Yule mtu, bwana wa nchi, akatwambia, 'Kwa hili nitajua kwamba ni watu wa kweli ninyi. Mwacheni mmojawapo wa ndugu zenu, chukueni chakula kwa ajili ya njaa katika nyumba zenu, na mwondoke. |
1294 | GEN 43:3 | Yuda akamwambia, “Yule mtu alituonya kwa ukali, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi.' |
1296 | GEN 43:5 | Lakini usipompeleka, hatutashuka. Kwa maana yule mtu alitwambia, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi.” |
1298 | GEN 43:7 | Wakasema, “Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?'Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?” |
1329 | GEN 44:4 | Walipokuwa wametoka mjini lakini hawajafika mbali, Yusufu akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Inuka, uwafuatie wale watu, na utakapowapata, wambie, 'Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema? |
1345 | GEN 44:20 | Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba, ni mzee, na mwana wa uzee wake, ni mdogo. Na ndugu yake alishakufa, na yeye peke yake ndiye amebaki kwa mama yake, na baba yake anampenda.' |
1346 | GEN 44:21 | Nawe ukawambia matumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.' |
1347 | GEN 44:22 | Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi kumwacha babaye. Kwani akimwacha babaye baba yake angekufa.' |
1348 | GEN 44:23 | Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.' |
1352 | GEN 44:27 | Mtumishi wako baba yetu akatwambia, 'Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili. |
1357 | GEN 44:32 | Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu na alisema, 'Ikiwa sitamleta kwako, ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu daima.” |
1368 | GEN 45:9 | Fanyeni haraka mwende kwa baba yangu na mmwambie, 'Hivi ndivyo asemavyo Yusufu mwanao, “Mungu amenifanya bwana kwa Wamisri wote. Shuka kwangu, usikawie. |
1376 | GEN 45:17 | Farao akamwambia Yusufu, “Wambie ndugu zako, 'Fanyeni hivi: Wapakieni wanyama wenu na mwende katika nchi ya Kanaani. |
1378 | GEN 45:19 | Basi mmeamriwa, 'Fanyeni hivi, chukueni mikokoteni kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na kwa ajili ya wake zenu. Mchukueni baba yenu na kuja. |
1418 | GEN 46:31 | Yusufu akawambia ndungu zake na nyumba ya baba yake, “Nitakwenda na kumwambia Farao, kusema, 'Ndugu zangu na nyumba ya baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia. |
1420 | GEN 46:33 | Itakuwa, Farao atakapowaita na kuwauliza, 'Kazi yenu ni ipi?' |
1421 | GEN 46:34 | mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa watunza wanyama tangu ujana wetu mpaka sasa, sisi, na baba zetu.' Fanyeni hivyo ili mweze kuishi katika nchi ya Gosheni, kwani kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri.” |
1512 | GEN 50:5 | 'Baba yangu aliniapisha, kusema, “Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika.” Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi.” |
1524 | GEN 50:17 | 'Mwambieni hivi Yusufu, “Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda.” Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yusufu akalia walipomwambia. |
1593 | EXO 3:13 | Musa akamwambia Mungu, “Nikienda kwa Waisraeli na kuwaambia, 'Mungu wa baba zenu amenituma mimi kwenu,' na kisha wakiniambia, 'jina lake nani?' nitawaambia nini?” |
1603 | EXO 4:1 | Musa akajibu, “Lakini itakuwaje wasiponiamini mimi au wasiponisikiliza na kusema, 'Yahwe hajakutokea wewe?” |
1624 | EXO 4:22 | Lazima umwambie Farao, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Israeli ni mtoto wangu, mzaliwa wa kwanza wangu, |
1634 | EXO 5:1 | Baada ya mambo haya kutokea, Musa na Aruni walienda kwa Farao na kumwambia, ““Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli anasema: 'Waache watu wangu waende, ili wapate kunifanyia karamu jangwani.'” |
1641 | EXO 5:8 | Ingawa wanapaswa kuleta hesabu sawa ya matofali watakayotengeneza kama ilivyokuwa awali. Msipokee pungufu, kwasababu wao ni wavivu. Ndiyo maana wanapiga kelele na kusema, 'turuhusu tuende tukamtolee sadaka Mungu wetu.' |
1643 | EXO 5:10 | Kwa hiyo viongozi wa watu na waangalizi wao waliwajulisha watu. Walisema, “Hivi ndivyo farao amesema: 'Sitawapeni tena malighafi. |
1650 | EXO 5:17 | Lakini Farao akasema, “Ninyi ni wavivu! Wavivu ninyi! Ninyi mwasema, 'Turuhusu twende kumtolea Yahwe sadaka.' |
1662 | EXO 6:6 | Kisha basi, sema kwa Waisraeli, 'Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu. |
1695 | EXO 7:9 | “Wakati Farao atakapo waambia, 'Fanya muujiza,' utamwambia Aruni, 'Chukuwa gongo lako na ulirushe chini mbele ya Farao, ililigeuke nyoka.”' |
1705 | EXO 7:19 | Kisha Yahweh akasema na Musa, “Mwambie Aruni, 'Chukuwa gongo lako na unyooshe mkono kwenye maji ya Misri, na juu ya mito yake, mifereji, visima, na madimbwi yote, ili maji yao ya damu. Fanya hivi ilikuwe na damu nchi nzima ya Misri, hadi kwenye vyombo vyote vya mbao na mawe.”' |
1712 | EXO 7:26 | Kisha Yahweh akazungumza na Musa, “Nenda kwa Farao na umwambie, 'Yahweh anasema hivi: Acha watu wangu waende hili wakaniabudu. |
1716 | EXO 8:1 | Yahweh akamwambia Musa, “Mwambie Aruni, 'Nyoosha mkono wako na gongo lako kwenye mito, mifereji, na kwenye mabwawa, na uwatoe vyura juu ya nchi ya Misri.”' |
1727 | EXO 8:12 | Yahweh akamwambia Musa, “Mwambie Aruni, 'Nyoosha gongo lako na upige udongo chini, iliuwe chawa kati nchi yote ya Misri.”' |
1731 | EXO 8:16 | Yahweh akamwambia Musa, “Inuka asubui mapema na usimame mbele ya Farao anapoenda mtoni. Umwambie, 'Yahweh anasema hivi: “Acha watu wangu waende wakaniabudu mimi. |
1781 | EXO 10:3 | Hivyo Musa na Aruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: 'Kwa muda gani utaendelea kukataa kujinyenyekesha mbele zangu? Acha watu wangu waenda ili wakaniabudu. |
1811 | EXO 11:4 | Musa akasema, “Yahweh asema hivi: 'Wakati wa usiku wa manane nitaenda Misri yote. |
1820 | EXO 12:3 | Liambie kusanyiko la Israeli, 'Siku ya kumi mwezi huu kila mtu lazima achukuwe mwana kondoo au mbuzi mdogo wa kwake, kila familia ifanye hivi, mwana kondoo kwa kila nyumba. |
1843 | EXO 12:26 | Watoto wako watakapo kuuliza, 'Hili tendo la ibada lina maana gani?' |
1844 | EXO 12:27 | kisha lazima useme, 'Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwasababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru.”' Kisha watu wakamsujudia Yahweh. |
1876 | EXO 13:8 | Hiyo siku utasema kwa watoto wako, 'Hii ni kwasababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipo taka Misri.' |
1882 | EXO 13:14 | Mwanae atakapo kuuliza baadae, 'Hii ina maana gani?' kisha utamwambia, 'Ni kwa mkono hodari Yahweh katutoa Misri, kutoka nyumba ya utumwa. |
1893 | EXO 14:3 | Farao atasema kuhusu Waisraeli, 'Wanaangaika kwenye nchi. Nyikani imewafunika.' |
1957 | EXO 16:9 | Musa akamwambia Aruni, “Sema kwa jamii yote ya watu wa Israeli, 'Njoo karibu ya Yahweh, kwa kuwa amesikia malalamishi yenu.'” |
1960 | EXO 16:12 | “Nimesikia malalamishi ya watu wa Israeli. Sema nao na useme, 'Jioni utakula nyama, na asubui utashiba mkate. Kisha utajua mimi ni Yahweh Mungu wako.'” |
1964 | EXO 16:16 | Hii ni amri Yahweh aliyotoa: 'Lazima ukusanye, kila mmoja wenu, kiasi unacho itaji kula, lita mbili kwa kila mtu. Hivi ndivyo utakavyo kusanya: Kusanya cha kutosha kula cha kila mtu anaye ishi hemani mwako.'” |
1971 | EXO 16:23 | Aliwaambia, “Hili ndilo Yahweh alililo lisema: 'Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyo baki, jihifadhie hadi asubui.”' |
1980 | EXO 16:32 | Musa akasema, “Hili ndilo Yahweh alilo amuru: 'Acha lita mbili ya manna ihifadhiwe kwa ajili vizazi vya watu wako ili kwamba uzao wako uone mkate niliyo kulisha nyikani, baada ya kukutoa kutoka nchi ya Misri. |
2039 | EXO 19:12 | Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, 'Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakaye shika mlima ata uawa.' |
2050 | EXO 19:23 | Musa akamwabia Yahweh, “Watu hawawezi kuja juu ya mlima, kwa kuwa umetuamuru: 'Eka mipaka kuzunguka mlima na utenge kwa ajili ya Yahweh.'” |
2074 | EXO 20:22 | Yahweh alimwambia Musa, “Ni lazima uwaambie hili Waisraeli: 'Wewe mwenyewe umeona niliongea na wewe kutoka mbinguni. |
2080 | EXO 21:2 | 'kama mtanunua mtumishi wa kiebrania, atatumikia kwa miaka sita, na mwaka wa saba ataachiwa huru bila kilipwa chochote. |
2434 | EXO 31:13 | “Waambie wana wa Israeli, 'Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. |
2447 | EXO 32:8 | Wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu. Wakasema, 'Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. |
2451 | EXO 32:12 | Kwa nini Wamisri kusema, 'Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi?' Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. |
2452 | EXO 32:13 | Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, 'Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.'” |
2462 | EXO 32:23 | Maana waliniambia, 'Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu. Kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.' |
2463 | EXO 32:24 | Nikawaambia, 'Mtu ye yote aliye na dhahabu na aivue; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.” |
2466 | EXO 32:27 | Akawaambia, Yahweh, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.'” |
2475 | EXO 33:1 | Yahweh anasema na Musa, “Nenda kutoka hapa, wewe na watu ulio watoa kutoka nchi ya Misri. Nenda kwenye nchi nilio fanya nadhiri na Ibrahimu, Isaka, Yakobo, nilipo sema, 'Nitakupa wewe na uzao wako'.' |
2479 | EXO 33:5 | Yahweh alisema kwa Musa, “Waambie Waisraeli, 'Ninyi ni watu wakorofi. Kama ningeenda miongoni mwenu ata kwa muda kidogo, nigewaharibu ninyi. Hivyo sasa, toa mikufu yenu ili niamue nini cha kufanya kwenu.”' |
2486 | EXO 33:12 | Musa alisema na Yahweh, “Ona, umekuwa ukisema na mimi, 'Chukuwa watu hawa safarini,' lakini hauja niambia nani utamtuma na mimi. Umesema, 'Nina kujua kwa jina, na umepata upendeleo kwangu.' |
2748 | LEV 1:2 | “Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi.” |
2798 | LEV 4:2 | “Waambie wana wa Israeli 'mtu yeyote akifanya dhambi bila kukusudia, kufanya chochote ambacho Bwana ameagiza kutofanya, na kama akifanya chochote kilichozuiliwa, yafuatayo lazima yatatendeka. |
2859 | LEV 6:2 | “Mwagize Haruni na wanawe, kusema, 'hii ni sheria ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa lazima iwe juu ya makaa ya madhabahu usiku wote hata asubuhi, na moto wa madhabahu utaendelea kuwaka. |
2875 | LEV 6:18 | “Sema na Haruni na watoto wake kwamba, 'Hii ni sheria ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi lazima kuchinjwa mahali pa sadaka ya kuteketezwa itachinjwa mbeleya Bwana. Ni takatifu sana. |
2903 | LEV 7:23 | “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi. |
2909 | LEV 7:29 | “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh. |
2949 | LEV 8:31 | Kwa hiyo Musa akawambia Aruni na wanawe, “Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyoamriwa, kusema, 'Aroni na wanawe wataila.' |
2957 | LEV 9:3 | Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Twaeni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi na ndama na mwana-kondoo, hawa wawili wawe na umri wa mwaka mmoja na bila dosari, ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; |
2981 | LEV 10:3 | Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'” Naye Aroni hakusema neno lolote. |
3000 | LEV 11:2 | “Sungumzeni na watu wa Israeli muwaambie, 'Hivi ndivyo viumbe vyenye uhai ambavyo mwaweza kula miongoni mwa wanyama walioko juu ya nchi. |
3047 | LEV 12:2 | “zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi. |
3147 | LEV 14:35 | ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.'” |
3171 | LEV 15:2 | “Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, 'Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi. |