8843 | 1KI 3:24 | Mfalme akasema, ''Nileteeni upanga.” Kwa hiyo wakaleta upanga kwa mfalme. |
9418 | 1KI 20:7 | Ndipo mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi pamoja akawaambia, ''Hebu angalieni jinsi huyu mtu anavyotafuta matatizo. Amenitumia ujumbe kwamba anataka kuchukua wake zangu, watoto wangu, fedha na dhahabu zangu, nami sijamkatalia.” |
9425 | 1KI 20:14 | Naye Ahabu akajibu, ''kwa nani? BWANA akamjibu akasema, “kwa kuwatumia viijana wanaotumikia maliwali wa wilaya.” kisha Ahabu akasema, “Ni nani atakayepewa hiyo vita?' BWANA akamwambia, “wewe.” |
17726 | ISA 1:2 | Sikia enyi mbingu, tega sikio ewe nchi; kwa kuwa Yahwe amesema: ''Nimewatunza na kuwalea watoto, lakini wamenigeuka. |
17735 | ISA 1:11 | ''Sadaka zenu ni nyingi kiasi gani kwangu?'' asema Yahwe. ''Nimesikia vya kutosha kuhusu sadaka yenu ya mwana kondoo, na mnyama alionona; na damu ya ng'ombe, ndama, au mbuzi si vifurahii. |
17791 | ISA 3:14 | Yahwe atakuja na hukumu juu ya wazee na watu wao na viongozi wao: ''Umeharibu shamba; nyara kutoka kwa masikni ziko kwenye nyumba zako. |
17804 | ISA 4:1 | Siku hiyo wanawake saba watamchukua mwanaume mmoja na kusema, ''Tutakula chakula chetu wenyewe, tutavaa nguo zetu wenyewe. lakini tunahitaji kuchukua jina lako ili tuondoe haibu zetu.'' |
17855 | ISA 7:3 | Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, ''Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi. |
17863 | ISA 7:11 | ''Omba ishara ya Yahwe Mungu wako; omba juu ya hilo kwa kina au kwa kiwango cha juu.'' |
17880 | ISA 8:3 | Nilienda kwa huyo nabii mwanamke alipata mimba na kumzaa mtoto. Halafu Yahwe akaniambia, ''Muite jina lake Shalal Hash Baz; |
17896 | ISA 8:19 | Watakuambia wewe, ''tafuta habari kwa watu wenye pepo na wachawi'', walio kama ndege na kunong'ona dua. Lakini hawataacha kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waenende kwa watu waliokufa badala ya walio hai? |
17933 | ISA 10:13 | Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake. |
17944 | ISA 10:24 | Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, ''watu wangu mhishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri. |
17971 | ISA 12:1 | Siku hiyo utasema, ''Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi, |
17974 | ISA 12:4 | Siku hiyo utasema, ''Mshukuru Yahwe na ita jina lake; tangaza matendo yake miongoni mwa watu, tangaza jina lake limeinuliwa. |
18002 | ISA 14:4 | mtaimba hii kauli wimbo juu ya mfalme wa Babeli, ''Ni kwa jinsi gani wayanyasaji wamefika mwisho, kiburi cha hasira kimekwisha! |
18053 | ISA 16:14 | Tena Yahwe amesema, ''Ndani ya miaka mitatu utukufuwa Moabu utatoweka; japo watu wake wengi, watakao bakia ni wachache, na wasionafaida. |
18071 | ISA 18:4 | Yahwe asema hivi, ''nitachunguza kimyakimya kutoka nyumbani kwangu, kama kupika joto kwenye jua, na kama ukungu kwenye joto la mavuno. |
18085 | ISA 19:11 | Wakuu wa Zoana ni wajinga kabisa. Washauri wenye busara wa Farao ni wapumbavu. Unawezaje kumwambia Farao, ''Mimi ni mtoto wa watu wenye busara, |
18086 | ISA 19:12 | ''Wako wapi hao watu wenye busara? mtoto wa mfalme wa zamani? Waache wakuambie? na ijulikane kitu ambacho Yahwe wa majeshi amekipanga kuhusiana na Misri. |
18101 | ISA 20:2 | Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, ''Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.'' Alifanya hivyo, tembeeni uchi na miguu wazi. |
18102 | ISA 20:3 | Yahwe asema, ''Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia— |
18114 | ISA 21:9 | Tazama gari linakuja na wakiwa wawili wawili. anaita, ''Babeli umeanguka, umeanguka, na sanamu za kuchonga za miungu yao zimevunjika chini.'' |
18117 | ISA 21:12 | Mlinzi akasema, ''Asubuhi itafika na vilevile usiku. Ikiwa unataka kuuliza basi uliza; na urudi tena.'' |
18121 | ISA 21:16 | Maana hili ndilo Bwana alichosema na mimi, ''Ndani ya mwaka mmoja, kama mtu aliyeajiriwa kwa mwaka ataona, utukufu wa Kedari utakwisha. |
18136 | ISA 22:14 | Hili limebanika kwenye masikio yangu na Yahwe wa majeshi: Hakika maovu haya hayatasamehewa, hata utakapokufa, ''Amesema Bwana wa majeshi. |
18137 | ISA 22:15 | Bwana, Yahwe wa majeshi, asema hivi, ''Nenda kwa huyu kiongozi, kwa Shebana, aliye juu ya nyumba, na umwambie, |
18141 | ISA 22:19 | ''Nami nitakuondoa katika ofisi yako na katika kituo chako. Na utavutwa chini. |
18151 | ISA 23:4 | Kuwa na aibu, Sidoni; maana bahari imenena, mkuu wa bahari. Amesema, ''Sijafanya kazi wala kuzaa wala kukuza vijana wadogo wala kuwalea mabinti. |
18152 | ISA 23:5 | ''Pale taarifa ilipofika Misri, watauzunika kuhusu Tire. |
18159 | ISA 23:12 | Amesema, ''Hamtofurahia tena, binti bikira wa Sidoni uliyenyanyasika; nyanyuka, pitia Kyprusi; lakini wala hapatakuwa na punziko.'' |
18181 | ISA 24:16 | Kutoka umbali wa sehemu ya dunia tumesika nyimbo, ''Utukufu kwa watu wenye haki! Lakini nikasema, ''Nimepita mbali, Ole juu wangu! Wasaliti walshulika na wenye hila; ndio, wasaliti walishuhulika na wenye hila.'' |
18197 | ISA 25:9 | Yatazungumzwa katika siku hiyo, ''Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.'' |
18224 | ISA 27:3 | ''Mimi Yahwe ni mlinzi wake; Ninalimwagia maji kila wakati; hivyo hakuna anayelimiza, Ninalilinda usiku na mchana. |
18274 | ISA 29:11 | Ufunuo wote umekuja kwako kama maneno ya kitabu kilichotiwa muhuri, ambacho watu wanaweza kumpa mtu anayejifunza, na kusema hivi, ''Soma hiki.'' na atasema, ''Siwezi maana imetiwa muhuri.'' |
18275 | ISA 29:12 | Kama kitabu kitapewa kwa mtu asiyeweza kusoma, na kumwambia, '''Soma hiki,'' na anasema, ''Siwezi kusoma.'' |
18276 | ISA 29:13 | Bwana asema, ''Watu hawa wananikaribia mimi na kunishimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbalii na mimi. Heshima yao kwangu ni kwa sababu tu ya amri waliofundishwa. |
18278 | ISA 29:15 | Ole wao wale wanaoficha mipango yao kwa Yahwe, na wale ambao matendo yao ni ya giza. Wanasema, ''Nani anayetuona sisi, na ni nani anayetutambua sisi? |
18279 | ISA 29:16 | Nyie mnaebadilisha vitu juu chini! Je mfinyanzi anaweza kufikiriwa kama udongo, hivyo basi vitu vinavyotengeneza vitasema kuhusu aliyevitengeneza, ''Hajanitengeneza mimi, ''au vitu vinavyotngenezwa viseme kuhusu aliyevitengeneza, Hajaelewa''? |
18285 | ISA 29:22 | Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu nyumba ya Yakobo- Yahwe aliyemkomboa Ibrahimu, ''Yakobo hataaibika tena, wala uso wake hautabadilika rangi yake. |
18288 | ISA 30:1 | Ole wa watoto waasi, ''Hili ni tamko la Yahwe. ''Wataweka mipango, lakini haitatoka kwangu; wataungana na mataifa mengine, lakini hawakuongozwa na Roho wangu, hivyo wanongeza dhambi baada ya dhambi. |
18297 | ISA 30:10 | Wanawambia waonaji, ''msiangalie; na kwa manabii, ''msitabiri yaliyoyakweli kwetu; zungumza maneno ya kujipendeza kwetu, tabiri udanganyifu. Geukeni katika njia, |
18299 | ISA 30:12 | Hivyo basi mtakatifu wa Israeli asema, ''Kwa sababu umekataa maneno haya na kujifunza ukandamizaji na udanganyifu, |
18302 | ISA 30:15 | Maana Bwana Yahwe, Mtakatifu wa Israeli asema hivi, ''Kwa kurudi na kwa kupumzika mtaokolewa; katika utulivu na imani itakuwa ni nguvu zako, Lakini hamkuwa tayari. |
18308 | ISA 30:21 | Masikio yako yatasikia maneno yanayosemwa nyuma, Hii ndio njia, pitia hii, ''utakapogeuka upande wa kulia au utakageuka upande wa kushoto. |
18309 | ISA 30:22 | Mtakinajisi kifuniko chenu mlichokiweka juu ya pesa na dhahabu na kukitupa. Mtakitupa mbali kama hedhi kali, '''utawambia wao, ''Ondokeni hapa.'' |
18359 | ISA 33:10 | ''Sasa nitanyanyuka, ''asema Yahwe; '' sasa nitanyanyuliwa juu; sasa nitainuliwa. |
18394 | ISA 35:4 | Waambie wenye moyo wa uwoga, ''Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.'' |
18404 | ISA 36:4 | Kamanda mkuu wa jeshi akawaambia wao, ''Mwambieni Hezekia kwamba mfalme mkuu, mfalme Asiria, asema, 'Nini chanzo cha ujasiri wako? |
18407 | ISA 36:7 | Lakini ikiwa utasema nami, ''Tunamwamini Yahwe Mungu wetu,''Je sio yeye ambaye Hezekia ameondosha mahali palipoinuka na madhebau, asema kwa Yuda na Yerusalemu, ''Lazima tuabudu mbele ya madhebau hii katika Yerusalemu''? |
18412 | ISA 36:12 | Lakini kamanda mkuu akasema, ''Je bwana wenu ametuma kwa bwana wako na kuzungumza haya maneno? Je hajanituma kwa watu walio kaa kwenye ukuta, ili wale kinyesi chaao mwenyewe na kunywa mkojo waomwenyewe? |
18414 | ISA 36:14 | ''Mfalme asema, ' Msimruhusu Hezekia awadanganye ninyi, maana hataweza kuwaokoa ninyi. |
18428 | ISA 37:6 | na Isaya akawambia, ''Mwambieni Bwana wenu: 'Yahwe amesma, ''Msiogope kwa maneno mliyoyasikia, maneno ambayo mfalme wa Asiria amenitusi mimi. |
18432 | ISA 37:10 | ''Mwambie Hezekia, mfalme wa Yuda, 'Usimruhusu Mungu unayemwamini akudanganye, ''Yerusalemu haitatiwa mikononi mwa mfalme wa Asiria.'' |
18444 | ISA 37:22 | Haya ndiyo maneno ambayo Yahwe amezungumza kuhusu yeye, ''Binti bikira wa Sayuni wanakudharau na kukucheka kwa dharau; mabinti wa Yerusalemu wanatingisha vichwa vyao kwa ajili yako. |
18455 | ISA 37:33 | Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu Asiria: ''Atakuja katika miji, wala kurusha mkuki hapa. Wala atakuja hapa mbele kwa ngao au kujenga uzio njia panda dhidi yao. |
18461 | ISA 38:1 | Siku zile Hezekia alikuwa anaumwa karibia na kufa. Hivyo Isaya mtoto wa Amozi, nabii alikuja kwake na kumwambia, ''Yahwe amesema, 'panga mambo yako maana utakufa, hautaishi.' |
18463 | ISA 38:3 | Na akasema, ''samahani Yahwe, kumbuka jinsi nilivyoenenda kwa uaminifu mbele zako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya matendo mema katika macho yako.'' Na Hezekia akalia kwa sauti. |
18465 | ISA 38:5 | ''Nenda ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ''Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yenu, amesema: Nimeyasikiliza maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Ona ninakaribia kuongeza miaka kumi na tano katika maisha yako. |
18470 | ISA 38:10 | ''Nimesema kwamba nusu ya maisha yangu nitapita katika mlango wa kuzimu; Nilitumwa pale miaka yangu yote. |
18481 | ISA 38:21 | Sasa Isaya alisema, ''Waacheni wachukue donge mitini na kuliweka kweye jipu naye atapona. |
18482 | ISA 38:22 | ''Hezekia pia alisema, ''Je ni ishara gan ya kwamba nitaiende juu katika nyumba ya Yahwe?'' |
18485 | ISA 39:3 | Basi Isaya nabii alikuja kwa mfalme Hezekia na kumuuliza, ''Je watu hawa wamekuambia nini? wametoka wapi?, ''Wamekuja kwangu kutoka mbali nchi ya Babeli.'' |
18486 | ISA 39:4 | Isaya akamuuliza je ni vitu gani walivyoviona katika nyumba yako? Hezekia akajibu, ''Wameona kila kitu katika nyumba nyangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.'' |
18487 | ISA 39:5 | Basi Isaya akamwambia Hezekia, ''Sikiliza neno la Yahwe wa majeshi: |
18490 | ISA 39:8 | Basi Hezekia akamwambia Isaya, ''Neno la Yahwe alilolizunumza ni zuri.'' Maana alifikiria, ''Patakuwa na amani na utulivu katika siku zangu.'' |
18492 | ISA 40:2 | ''Ongea kwa upole kwa Yerusalemu; na tangaza vita vimeisha, maana maovu yao yamesamehewa, maana alipokea mara mbili kutoka kwa mkono wa Yahwe kwa dhambi zao.'' |
18493 | ISA 40:3 | Sauti inalia nje, ''Katika jangwa tengeneza njia ya Yahwe; njoosha njia ya Araba katika njia kuu ya Mungu.'' |
18496 | ISA 40:6 | Sauti inasema, ''Lia.'' Jibu lingine, ''Kwa nini nilie?'' ''Mwili wote ni nyasi na maagano yaliyoaminika ni kama ua kwenye shamba. |
18499 | ISA 40:9 | Nenda juu ya mlima mrefu, Sayuni, mbeba taarifa njema. waambie miji ya Yuda, ''Hapa ni Mungu wako!'' |
18517 | ISA 40:27 | Kwa nini unasema, Yakobo, na kutangaza, Israeli, ''Njia yangu imefichwa Yahwe asione, na Mungu wangu hakuwekwa wazi kuhusiana na uthibitisho wangu''? |
18522 | ISA 41:1 | ''Sikilizeni mbele yangu kwa ukimya, enyi mkao pwani; wacha mataifa yapate nguvu kwa upya; waache waje karibu na kuzungumza; na tusogee karibu tujadili mgogoro. |
18528 | ISA 41:7 | Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, ''Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke. |
18542 | ISA 41:21 | Wakilisha keshi yako, '' asema Yahwe; ''wakilisha hoja zenu nzuri kwa sanamu yenu,'' asema Mfalme wa Yakobo. |
18547 | ISA 41:26 | Ni nani aliyetangaza hili tangu mwanzo, ili tuweze kujua? na kabla ya mda, ili tuseme, ''Yuko sawasawa''? Kweli hakuna hata mmoja aliyekiri hili, ndio hakuna hata mmoja aliyekusikia ukisema chochote. |
18548 | ISA 41:27 | Kwanza nilizungumza na Sayuni, ''Tazama hapo walipo;'' Nimemtuma mhubiri Yerusalemu. |
18567 | ISA 42:17 | Watageuka nyuma, wataabishwa sana, wale wote wanaoiamini sanamu ya kuchonga, wanaosema na kuziambia sanamu za chuma, ''Nyinyi ni miungu wetu.'' |
18585 | ISA 43:10 | Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu. |
18587 | ISA 43:12 | Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, ''Mimi ni Mungu. |
18589 | ISA 43:14 | Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: ''Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli' kuwa wimbo wa maombolezo. |
18609 | ISA 44:6 | Yahwe asema hivi—Mfalme wa Israeli na Mkombozi wake, Yahwe wa majeshi: ''Mimi ni mwanzo na ni mwisho; na hakuna mungu ila mimi. |
18620 | ISA 44:17 | Kwa kutumia mbao hutengeneza miungu, sanamu yake; huisujudu na kuhieshimu, huipa sifa na kusema, ''Niokoe mimi, maana wewe ni mungu wangu.'' |
18622 | ISA 44:19 | Hakuna anayefikiria, wala kuelewa na kusema, ''Nimechoma sehemu ya mbao kwenye moto; na pia nimewooka mkate kwa kutumia makaa yake. Nimechoma nyama kwa makaa yake nikala. Sasa Je ninaweza kutengeneza kitu kinachochukiza kwa ajili ya kuabudia kwa sehemu ya mbao iliyobakia? Je ninaweza kusujudia sanamu ya mbao?'' |
18623 | ISA 44:20 | Ni kama anayejilisha majivu; moyo wke mdanganyifu unampoteza yeye. Huwezi kujiokoa mwenyewe, wala hawezi kusema, ''Hiki kitu katika mkono wangu wa kulia sio mungu wa kweli.'' |
18627 | ISA 44:24 | Yahwe asema hivi, Mkombozi wako, yeye aliyekuumba wewe kutoka tumboni: ''Mimi ni Yahwe, niliyefanya kila kitu, mimi mwenyewe nizinyooshae mbigu, mimi peke niitngenezae nchi. |
18633 | ISA 45:2 | ''Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja vipandevivande milango ya shaba na kukuta vipandevipande nguzo za chuma, |
18649 | ISA 45:18 | Yahwe asem hivi, nani aliyeziumba mbingu, Mungu wa kweli ndiye aliyeiumbwa nchi na kuifaya, ndiye aliyeianzisha nchi. Aliiumba yeye, sio kama taka, aliimba ili pawe na wenyeji: ''mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine. |
18666 | ISA 46:10 | Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, ''Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.'' |
18676 | ISA 47:7 | Umesema, ''Nitaongoza daima kama malikia huru.'' Haukuvichukua vitu hivi katika moyo, wala hakutafakari jinsi hivi vitu vitakavyojeuka. |
18678 | ISA 47:9 | ''Lakini vitu hivi vitakuja kwako siku moja katika kipindi cha siku moja; kwa nguvu za kutosha yatakuja kwako, japo uchawi wako na dua zako na hirizi. |
18679 | ISA 47:10 | Umeweka imani katika mapungufu yako; na kusema, ''Hakuna anayeniona mimi''; hekima na maarifa yako yanakupoteza, lakini unasema katika moyo wako, ''Nipo na hakuna hata mmoja kama mimi.'' |
18687 | ISA 48:3 | ''Nimetangaza vitu kutoka siku nyingi; Wamekuja nje kutoka mdomoni mwangu, na nimewafanya wajulikane; halafu gafla nimewafanyia, na yakatimia. |
18701 | ISA 48:17 | Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, ''Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia. |
18709 | ISA 49:3 | Amesema na mimi, ''Wewe ni mtumishi wangu, Israeli, kupitia yeye nitaonyesha utukufu wangu.'' |
18710 | ISA 49:4 | Lakini nilimjibu, ''Japo nilifikiria nilifanya kazi bure, nimetumia nguvu zangu bure, ikiwa haki yangu iko pamoja na Yahwe, na zawadi yangu iko kwa Mungu wangu. |
18712 | ISA 49:6 | Asema hivi, ''Ni kitu kidogo sana kwa wewe kuwa mtumishi wangu ili kuanzisha ukoo wa Yakobo, na kuwarejesha wanaoishi Israeli. Nitakufanya wewe kuwa mwanga kwa Wayunani, ili uwe wokovu wangu katika mipaka ya nchi. |
18713 | ISA 49:7 | Yahwe asema hivi, Mkombozi wa Israeli, Mtatakatifu wao, kwa yeye ambae maisha yake yamedharauliwa, kuchukiwa na mataifa, na mtumwa wa viongozi, ''Mfalme atakuona wewe na nyanyuka, na wakuu watakuona wewe na inama chini, kwa sababu ya Yahwe ambae ni mwaminifu, hata mtakatifu wa Israeli, aliyewachagua ninyi.'' |
18714 | ISA 49:8 | Yahwe asema hivi, ''Kwa mda huu nimeamua kuwaonyesha neema yangu na nitawajibu ninyi, na siku ya wokovu nitawasaidi ninyi; Nitakulinda wewe; na nitawapa kama agano kwa watu, kuitengeneza tena nchi, kuwarihtisha urithi uliokuwa na ukiwa. |
18721 | ISA 49:15 | ''Je mwanamke anaweza kumsahau mtoto wake, aliyemnyonyesha, hivyo hana huruma na mtoto aliye mzaa? ndio, hawakusahau, lakini siwezi kukusahau wewe. |
18731 | ISA 49:25 | Lakini Yahwe asema hivi, ''Wafungwa watachukuliwa kutoka kwa shujaa, na maeteka watakombolewa; maana utampinga adui yako na kuwakomboa watoto wako. |