9544 | 2KI 1:7 | Ahazi akawaambia wajumbe wake, “'Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana na ninyi na akasema haya maneno kwenu?” |
9552 | 2KI 1:15 | Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, “'Nenda chini pamoja naye. Usimwogope.”' Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme. |
9560 | 2KI 2:5 | Kisha wana wa manabii ambao walikuwa Yeriko wakaja kwa Elisha na kumwambia, “'Je unajua kwamba Yahwe atamwondoa bwana wako kutoka kwako leo?” Elisha akajibu, “Ndiyo, nalijua hilo, lakini msilizungumzie hilo.” |
9596 | 2KI 3:16 | Akasema, “'Yahwe asema hivi, 'Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.' |
24431 | MRK 4:39 | Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, “'Iwe shwari, amani”. Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa. |