17758 | ISA 2:3 | Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu. |
17842 | ISA 6:3 | Kila mmoja anaitana na mwenzake nakusema, ''Mtakakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. ni Yahwe wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.'' |
17846 | ISA 6:7 | Akaugusa mdomo wangu kwa makaa ya mawe na akasema, ''Ona, makaa ya mawe yameshika midomo yako; maovu yako yameondolewa, na dhambi zako zimelipiwa kwa hili.'' |
17850 | ISA 6:11 | Ndipo nikasema, ''Bwana, mda gani?'' Akanijibu, mpaka mji itakapopata ajali na kuharibiwa na pasipo wakazi, na nyumba hazina watu, na nchi imeanguka katika ukiwa mtupu, |
17865 | ISA 7:13 | Hivyo Isaya akajibu, ''sikilizen, nyumba ya Daudi. Je haijatosha kwa watu kuujaribu uvumilivu wa watu? Je ni lazima kuujaribu uvumilivu wa Mungu? |
18022 | ISA 14:24 | Yahwe wa majeshi ameapa, ''Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa: |
18111 | ISA 21:6 | Hiili ndilo Bwana aliloniambia, ''Nenda, baada ya mlinzi; lazima atoe taarifa kwa kile atakacho kiona. |
18113 | ISA 21:8 | Mlinzi analia nje, ''Bwana, ninasimama juu ya mnara siku zote, kila siku, na kwa nguzo yangu nitasimama usiku wote.'' |
18116 | ISA 21:11 | Tamko kuhusu Duma. Mtu mmoja amenita mimi kutoka Seiri, ''Mlinzi, ni kitu gani kilichobakizwa usiku? |
18491 | ISA 40:1 | ''Faraja, faraja watu wangu,'' amesema Mungu. |
18576 | ISA 43:1 | Lakini sasa haya ndio Yahwe asemayo, yeye aliyekuumba ewe, Yakobo, na yeye aliyekuumba ewe, Israeli: ''Usiogope, kwa maana nimekukomboa wewe; nmeikuita kwa jina lako, wewe ni wangu. |
18619 | ISA 44:16 | Huchoma sehemu ya kuni kwa moto, na huchoma nyama yake juu yake. hula na kushiba. huota moto na kusema, ''Ah, Nimepata joto, nimeouna moto.'' |
18728 | ISA 49:22 | Yahwe asema hivi, ''Tazama, nitanyanyua mkono wangu juu ya mataifa; Nitanyanyua bendera yangu ya ishara kwa watu. Watawaleta watoto wako kwenye mikono yao na watawabeba binti zako juu ya mabega yao. |
18755 | ISA 51:12 | ''Mimi, mimi ndiye niwapae faraja. Kwa nini uwaogope watu, ambao wanakufa, watatoto wa wanadamu, waliofanywa kama majani? |
18765 | ISA 51:22 | Bwana wenu Yahwe Mungu, anayewasihi watu wake, asema hivi, ''Tazama, Nimechukua kikombe cha ukubwa mkononi mwako- ukubwa wa kikombe cha hasira yangu - ili usiweze kunjwa tena. |
18772 | ISA 52:6 | Hivyo basi watu wangu watalijua jina langu; watajua kwamba siku hiyo kwamba mimi ndiye ninayesema ''Ndiyo, Ni Mimi!'' |
18794 | ISA 54:1 | ''Imba, ewe mwanamke tasa, ewe ambaye haujazaa; imba wimbo kwa furaha na lia kwa nguvu ewe ambaye hujapata uchungu wa kuzaa. Maana watoto walio katika ukiwa ni wengi kuliko watoto wa wanawake waliolewa,'' asema Yahwe. |
18811 | ISA 55:1 | ''Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama. |
18826 | ISA 56:3 | Usimuache mgeni yeyote aliyekuwa mfuasi wa Yahwe aseme, ''Yahwe atahakikisha ananiondoa kwa watu wake.'' Toashi ataweza kusema, ''tazama, mimi ni mti mkavu.'' |
18835 | ISA 56:12 | ''Njooni, ''Tunywe mvinyo na pombe. Kesho itakuwa kama leo, siku kubwa zaidi ya kipimo.'' |
18956 | ISA 64:1 | ''Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima inetikisika mbele yako, ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako! |
18979 | ISA 65:13 | Bwana Yahwe asema hivi, ''Tazama, mtumishi atakula, lakini atashikwa na njaa; tazama mtumishi wangu atakunywa lakini atakuwa na kiu; tazama mtumishi wangu atashangilia, lakini atatiwa katika aibu. |
19721 | JER 29:17 | Yahwe wa majeshi anasema hivi, ''Ona, niko karibu kutuma upanga, njaa, na ugonjwa juu yao. Kwa maana nitawafanya kuwa kama tini mbovu ambazo ni mbaya sana hazifai kuliwa. |
23724 | MAT 15:22 | Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, ''Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.'' |