9892 | 2KI 13:17 | Elisha akasema, “Fungua dirisha upande wa mashariki,” basi akalifungua. Kisha Elisha akasema, “Funga”, na akafunga. Elisha akasema, “Huu ndiyo mshale wa ushindi wa Yahwe, huu mshale wa ushindi juu ya Shamu, kwa kuwa utawapiga Washami katika Afeki hadi utakapowaangamiza.” |
11531 | 2CH 17:3 | Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. (Baadhi ya mandiko ya kale hayana “Daudi”, na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina “Daudi). |
11909 | 2CH 32:29 | Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alaikuwa amempa afya tele. (Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadji ya matoleo ya kisasa yanasema “punda”, na baadhi mengine ya kisasa yanaacaha neno nzima) |
19666 | JER 27:1 | Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema “Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema “Sedekia”, kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake). |