11226 | 2CH 2:9 | Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” (Maandishsi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula”). |
11617 | 2CH 20:25 | Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. (Badala ya “miongoni mwao”, baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa”). |
11902 | 2CH 32:22 | Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. (Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande”, baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande”). |
11959 | 2CH 34:21 | “Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maani ni kikuu, kwa sababu babu zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake”. (Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu”, baadhi ya matoleo yanasema “ ambayo yamemulikwa zidi yetu”). |
24001 | MAT 23:14 | (Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 “Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane”). |