67 | GEN 3:11 | Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?” |
86 | GEN 4:6 | Yahwe akamwambia Kaini, “ kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana? |
87 | GEN 4:7 | Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde. |
90 | GEN 4:10 | Yahwe akasema, “umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini. |
317 | GEN 12:18 | Farao akamwita Abram na kusema, “Nini hiki ambacho umenifanyia? Kwa nini hukuniambia kuwa alikuwa mke wako? |
318 | GEN 12:19 | Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.” |
328 | GEN 13:9 | Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.” |
415 | GEN 17:17 | Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?” |
439 | GEN 18:14 | Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” |
443 | GEN 18:18 | Ikiwa kwa hakika Abraham atakuwa mkuu na taifa lenye nguvu, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? |
448 | GEN 18:23 | Kisha Abraham alikaribia na kusema, “Je utawafutilia mbali watakatifu pamoja na waovu? |
449 | GEN 18:24 | Huenda wakawepo wenye haki hamsini katika mji. Je utawakatilia mbali na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo? |
453 | GEN 18:28 | Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?” Akasema, “Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale.” |
463 | GEN 19:5 | Wakamwita Lutu, na kumwambia, “Wale wanaume walioingia kwako usiku wakowapi? watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao.” |
470 | GEN 19:12 | Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je una mtu mwingine yeyote hapa? wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa. |
500 | GEN 20:4 | Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, “Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki? |
505 | GEN 20:9 | Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, “Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa.” |
531 | GEN 21:17 | Mungu akasikia kilio cha kijana, na malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, “Nini kinakusumbua? Usiogope, kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha kijana mahali alipo. |
587 | GEN 23:15 | “Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako.” |
597 | GEN 24:5 | Yule mtumwa wake akamwambia, “Itakuwaje ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kufuatana nami hadi katika nchi hii? Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka?” |
615 | GEN 24:23 | akamuuliza, “wewe ni binti wa nani? Niambie tafadhali, Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako kwa ajili yetu kupumzika usiku?” |
623 | GEN 24:31 | Labani akasema, “Njoo, wewe uliye barikiwa na Yahwe. Kwa nini umesimama nje? nimekwisha andaa nyumba, pamoja na mahali kwa ajili ya ngamia.” |
703 | GEN 26:10 | Abimeleki akamwambia, “Ni jambo gani hili ulilotufanyia? Mmojawapo wa watu angeweza bila shaka kulala na mke wako, nawe ungeweza kuleta hatia juu yetu.” |
760 | GEN 27:32 | Isaka baba yake akamwambia, “U nani wewe? Akasema, “Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.” |
761 | GEN 27:33 | Isaka akatetemeka sana na kusema, “Alikuwa nani aliyewinda mawindo nakuniletea? Nilikula chote kabla haujaja, nami nimembariki. Atabarikiwa, kwa kweli.” |
764 | GEN 27:36 | Esau akasema, “Je hakuitwa Yakobo kwa haki? Kwa maana amenidanganya mara mbili hizi. Alichukua haki ya uzaliwa wangu wa kwanza, na tazama, sasa amechukua baraka yangu.” Na akasema, “Je haukuniachia baraka? |
765 | GEN 27:37 | Isaka akajibu na kumwambia Esau, “Tazama, nimemfanya kuwa bwana wako, na nimempa ndugu zake kuwa watumishi wake. Na nimempa nafaka na divai. Je nikufanyie nini mwanangu? |
766 | GEN 27:38 | Esau akamwambia babaye, “Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu? Nibariki nami, hata mimi pia, babangu.” Esau akalia kwa sauti. |
773 | GEN 27:45 | hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea, na kusahau ulivyomtenda. Kisha nitatuma na kukurudisha kutoka pale. Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja? |
811 | GEN 29:15 | Kisha Labani akamwambia Yakobo, “Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje? |
821 | GEN 29:25 | Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa? |
833 | GEN 30:2 | Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, “Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto? |
846 | GEN 30:15 | Lea akamwambia, “Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, “Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao. |
862 | GEN 30:31 | Hivyo Labani akasema, “Je nikulipe nini? Yakobo akasema, 'Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza. |
888 | GEN 31:14 | Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, “Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu? |
889 | GEN 31:15 | Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu. |
900 | GEN 31:26 | Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita? |
901 | GEN 31:27 | Kwa nini umekimbia kwa siri na kunihadaa kwa kutokuniambia? Ningekuruhusu uondoke kwa sherehe na kwa nyimbo, kwa matari na vinubi. |
904 | GEN 31:30 | Na sasa, umeondoka kwa sababu umeitamani sana nyumba ya baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu? |
910 | GEN 31:36 | Yakobo akakasirika na kuojiana na Labani. Akamwambia, “Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali? |
911 | GEN 31:37 | Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili. |
917 | GEN 31:43 | Labani akajibu na kumwambia Yakobo, “Mabinti hawa ni mabinti zangu, wajukuu ni wajukuu wangu, na wanyama ni wanyama wangu. Yote uyaonayo ni yangu. Lakini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa? |
946 | GEN 32:18 | Akamwagiza mtumishi wa kwanza, akisema, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, akasema, 'Ninyi ni wa nani? Mnakwenda wapi? Na wanyama hawa mbele yenu ni wa nani? |
976 | GEN 33:15 | Esau akasema, haya nikuachie baadhi ya watu wangu waliopamoja nami.” Yakobo akasema, “Kwa nini kufanya hivyo? Bwana wangu amekuwa mkalimu kwangu kiasi cha kutosha.” |
1004 | GEN 34:23 | Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu? Haya na tukubaliane nao, nao wataishi kati yetu.” |
1092 | GEN 37:8 | Ndugu zake wakamwambia, “Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu? Hata wakamchukia zaidi kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake. |
1094 | GEN 37:10 | Akamwambia baba yake vile vile alivyowambia ndugu zake, na baba yake akamkemea. Akamwambia, Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako na mimi na ndugu zako kweli tutakuja kukuinamia mpaka chini?” |
1097 | GEN 37:13 | Israeli akamwambia Yusufu, 'Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao.” Yusufu akamwambia, “nipo tayari.” |
1110 | GEN 37:26 | Yuda akawambia ndugu zake, “Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake? |
1114 | GEN 37:30 | Akarudi kwa ndugu zake na kusema, “Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?” |
1136 | GEN 38:16 | Akamwendea kando ya njia na kusema, “Njoo, tafadhari uniruhusu kulala nawe” - kwani hakujua kwamba alikuwa ni mkwewe - naye akasema, “Utanipa nini ili ulale nami? |
1159 | GEN 39:9 | Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanidhuiria chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu? |
1181 | GEN 40:8 | Wakamwambia, Sisi wote tumeota ndoto na hakuna wakuitafsiri.” Yusufu akawambia, “Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Niambieni, tafadhari.” |
1254 | GEN 42:1 | Basi Yakobo akafahamu kwamba kuna nafaka huko Misri. Akawambia wanawe, “Kwa nini mnatazamana? |
1275 | GEN 42:22 | Rubeni akawajibu, “Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu.” |
1298 | GEN 43:7 | Wakasema, “Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?'Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?” |
1318 | GEN 43:27 | Akawauliza juu ya hali zao na kusema,”Je baba yenu hajambo, yule mzee mliyemnena? Je bado yu hai?” |
1329 | GEN 44:4 | Walipokuwa wametoka mjini lakini hawajafika mbali, Yusufu akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Inuka, uwafuatie wale watu, na utakapowapata, wambie, 'Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema? |
1330 | GEN 44:5 | Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi? Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya.” |
1332 | GEN 44:7 | Wakasema, “Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya? Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili. |
1333 | GEN 44:8 | Tazama, pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu, tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani. Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu? |
1340 | GEN 44:15 | Yusufu akawambia, “Je ni nini hili mlilolifanya? Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi. |
1341 | GEN 44:16 | Yuda akasema, “Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe? Mungu ameona uovu wa watumishi wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, wote sisi na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake.” |
1359 | GEN 44:34 | Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami? Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu.” |
1362 | GEN 45:3 | Yusufu akawambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu. Je baba yangu ni mzima bado? Ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walitishwa na uwepo wake. |
1440 | GEN 47:19 | Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu. |
1483 | GEN 49:9 | Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je nana atakayejaribu kumwamsha? |
1526 | GEN 50:19 | Lakini Yusufu akawajibu, “Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu? |
1569 | EXO 2:14 | Lakini yule mtu alisema, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi juu yetu? Unataka kuniua na mimi kama ulivyomuua yule mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kusema, “Hakika niliyoyafanya yamejulikana.” |
1575 | EXO 2:20 | Kisha akawauliza binti zake, “Yu wapi sasa? Kwa nini mlimwacha? Mwiteni ili apate kula chakula pamoja nasi.” |
1613 | EXO 4:11 | Yahwe akamwambia, “Ni nani anayeumba mdomo wa mwanadamu? Ni nani amfanyaye mwanadamu kuwa bubu au aone au kipofu? Je si mimi Yahwe? |
1616 | EXO 4:14 | Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha. |
1635 | EXO 5:2 | Farao akasema, “Yahwe ni nani? Kwa nini mimi nisikiliz sauti yake na kuwaacha Israeli waende? Mimi simjui Yahwe; na la zaidi, sitawaacha Israeli waende.” |
1637 | EXO 5:4 | Lakini mfalme wa Misri aliwaambia, “Musa na Aruni, kwa nini mnawatoa watu kazini mwao? Nendeni kazini kwenu.” |
1648 | EXO 5:15 | Basi Wanyapara wa wana wa Israeli wakamwendea Farao na kumlilia. Walisema, “Kwanini unawatendea watumishi wako hivi? |
1655 | EXO 5:22 | Musa akarudi kwa BWANA na kumwambia, “Bwana, kwanini umewatenda mabaya watu hawa? Kwanini kunituma mimi kwanza? |
1737 | EXO 8:22 | Musa akasema, “Sio vyema sisi kufanya hivyo, kwa kuwa dhabihu tunazo mtolea Yahweh Mungu wetu zinachukiza kwa Wamisri. Kama tutatoa dhabihu mbele ya macho yao zilizo chukizo kwa Wamisri, hawata tupiga mawe? |
1781 | EXO 10:3 | Hivyo Musa na Aruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: 'Kwa muda gani utaendelea kukataa kujinyenyekesha mbele zangu? Acha watu wangu waenda ili wakaniabudu. |
1785 | EXO 10:7 | Watumishi wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mwanaume ata kuwa msumbufu kwetu? Acha Waisraeli waende wakamuabudu Yahweh Mungu wao. Bado haujatambua kuwa Misri imeharibiwa?” |
1901 | EXO 14:11 | Walimwambia Musa, “Ni kwasababu hakukuwa na makaburi Misri, hadi umetuleta tufe huku nyikani? Kwanini umetutendea hivi, kwa kututoa Misri? |
1902 | EXO 14:12 | Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, 'Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.' Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani.” |
1905 | EXO 14:15 | Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Kwanini wewe, Musa, unaendelea kuniita mimi? Waambie Waisraeli waendelee mbele. |
1932 | EXO 15:11 | Ni nani kama wewe, Yahweh, miongoni mwa miungu? Nani kama wewe, mtakatifu wa utukufu, katika sifa umetukuzwa, anaye fanya miujiza? |
1956 | EXO 16:8 | Musa pia akasema, “Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa tele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayo tamka dhidi yake. Nani ni Aruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh.” |
1976 | EXO 16:28 | Kisha Yahweh akamwambia Musa, Kwa muda gani utaendelea kukataa kushika amri zangu na sheria zangu? |
1986 | EXO 17:2 | Hivyo watu wakamlaumu Musa kwa hali yao na kusema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akasema, “Kwanini mnagombana na mimi? Kwanini mnajaribu Yahweh?” |
1987 | EXO 17:3 | Watu walikuwa na kiu sana, na waka mlalamikia Musa. Wakasema, “Kwanini umetutoa Misri? Ili utuue sisi na watoto wetu na mifugo yetu kwa kiu?” |
1988 | EXO 17:4 | Kisha Musa akamlilia Yahweh, “Nini ni fanya kwa hawa watu? Wako tayari ata kunipiga mawe.” |
2014 | EXO 18:14 | Baba mkwe wake Musa alipo ona yale yote aliyo yafanya kwa watu, alisema, “Ni nini unachofanya na watu? Kwanini unaketi peke yako na watu wote wamesimama kukuzunguka asubui hadi jioni?” |
2141 | EXO 22:26 | kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma. |
2450 | EXO 32:11 | Musa akamsihi sana Yahweh Mungu wake, na kusema,”Yahweh, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? |
2460 | EXO 32:21 | Musa akamwambia Aruni, “Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? |
2490 | EXO 33:16 | Au je, itajulikanaje niimepata upendeleo machoni pako, mimi na watu wako? Haitakuwa kuwa tu kama ukienda nasi mimi na watu wako tutakuwa na utofauti na watu wengine wote waliopo katika uso wa dunia?” |
2995 | LEV 10:17 | “Kwa nini hamjaila sadaka ya dhambi katika eneo la hema, kwa kuwa ni takatifu sana, na kwa kuwa Yahweh amishaitoa kwenu ili kuchukua uovu wa kusanyiko, ili kufanya upatanisho kwa aijli yao mbele zake? |
2996 | LEV 10:18 | Tazama, damu yake haikuletwa ndani ya hema, kwa hiyo iliwapasa kwa hakika kuwa mekwisha ila kwenye eneo la hema, kama nilivyoagiza? |
3490 | LEV 25:20 | Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu.” |
4029 | NUM 11:4 | Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, “Ni nani atakayetupatia nyama za kula? |
4036 | NUM 11:11 | Musa akasema na BWANA, “Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna hiyo? kwa nini hujapendezwa na mimi? unanifanya kubeba mizigo ya hawa watu. |
4037 | NUM 11:12 | Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia, “wabebe kwa ukaribu vifuani mwako kama baba abebavyo mtoto wake? Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ambayo uliwaahidi mababu zao kuwapa? |
4038 | NUM 11:13 | Naweza kupata wapi nyama za kuwapa watu wote hawa? Wanalia mbele zangu na wanasema, 'tupe nyama tule.' |